Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kuzaliwa kwa vituo vipya vya kupigia kura tofauti na vilivyotumika kuandikisha imetajwa kuwa sababu ya wananchi kutoona majina yao katika sehemu walizojisajili.
Hilo limesemwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kata ya Mtoni, Nobert Kamugisha baada ya kuwapo kwa malalamiko ya baadhi ya watu kutoona majina yao katika mitaa waliojiandikishia.
Ametoa kauli hiyo leo Novemba 27, 2024 baada ya kumaliza kufanya ukaguzi wa vituo vya kupigia kura katika eneo lake.