HOJA Dar: Mtaa wa kidosho - Mikocheni uchafuzi wa daraja linalopitisha maji taka ni chanzo cha malaria

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Wananchi wanaoishi mtaa wa Kidosho Mikocheni jijini Dar es salaam wanawalalamikia baadhi ya watu wanaotumia daraja linalo pitisha maji taka mpaka baharini kama sehemu ya kutupa takataka, hali inayopelekea daraja hilo kusongamana na uchafu na kufanya maji yatuame kwa muda mrefu.

Aidha wamelalamika kuwepo na mbu wengi wanaosababishwa na kutuama kwa maji hayo kwa muda mrefu na kufanya kuuguwa malaria mara kwa mara.

Soma pia: KERO Dar es Salaam: Mtaa wa Darajani - Mikocheni A, maji ya kinyesi yanasambaa tu mtaani

Tunatoa wito kwa viongozi na mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kutatua tatizo la uchafu unaoziba daraja na kuweka sheria kwa wanaotupa takataka kwenye daraja hilo.

​

Pia Soma
~
Rais Samia: Dar es Salaam ni kuchafu, ni aibu
~ DC Mpogolo: Atakaye tupa taka Ganda la Ndizi na Pipi faini Milioni 1, Dar
 
Mikochen hii niliwah kupita siku flan hiv nilichoka! Wakat nasoma kipind hilo ilkuwaga ndoto yangu kabisa kuja kuishi mikocheni au kijitonyama K
 
Dar yote ni chafu, harufu mbaya, hewa nzito.....ovyo kbs!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…