Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Saleh Ayoub ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Green Acres iliyopo maeneo ya Mbezi Beach Africana, Dar es Salaam amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kusomewa shtaka la ulawiti.
Katika kesi hiyo namba Cc 32444/24 iliyotajwa kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa, Mshtakiwa amekana shtaka ambalo amesomewa.
Hata hivyo, Wakili Jaquline kutoka upande Jamhuri amesema kuwa upelelezi wa tuhuma zinazomkabili mshtakiwa tayari umekamilika kwa asilimia 100.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Novemba 26, 2024, ambapo mtuhumiwa ameendelea kuwa nje kwa dhamana.
Itakumbukwa mshtakiwa huyo amepandishwa kizimbani siku moja baada ya Mdau wa Jamiiforum.com kuhoji sababu za kutofikishwa Mahakamani kwa Watuhumiwa aliodai wanahusika na tuhuma hizo.
Kutokana taarifa ya Mdau Mwalimu huyo anatuhumiwa kumlawiti Mtoto wa darasa la tano (jina linahifadhiwa) kwa nyakati tofauti katika mazingira ya Shule hiyo.
Awali, mama wa mtoto huyo alizungumza na JamiiForums na kusema kuwa suala lake lilikuwa likizungushwa kufikishwa Mahakamani, ambapo kila alipoenda Kituo cha Polisi Oysterbay kuulizia aliambiwa "Faili lipo kwa Mwanasheria kuwa mpole kwa kuwa kule kuna mafaili mengi."
Muda mfupi baada ya taarifa hiyo ya Mdau kuandikwa Novemba 12, 2024, kesho yake akajulishwa kuwa suala lake litafikishwa Mahakamani.
Kusoma Hoja ya Mdau, bonyeza hapa:
~ Walimu wa Shule ya Green Acres (Dar) wanaotuhumiwa kulawiti na kuwadhalilisha Wanafunzi, wanalindwa na nani?
~ Watu 6 kutoa ushahidi Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake
~ Dar: Kesi ya Mwalimu Saleh Ayoub anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi yaahirishwa hadi Februari 17, 2025
~ Shahidi: Mwalimu Mkuu anayedaiwa kumlawiti Mwanangu alimwambia 'ukisema nitakupiga nikuvunjevunje'
~ Kesi inayomkabili Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti mtoto yaahirishwa hadi Machi 24, 2025
Pia soma ~ Mwalimu wa Shule ya Kingdom (Banana – Dar) anatuhumiwa kumbaka Mwanafunzi wake wa Darasa la Saba