Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Siku ya tatu ya Mkutano wa Nchi za Afrika zinazotekeleza Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu (EHPMP) ambapo leo Tarehe 6 Novemba 2024 umelenga kujadili namna bora ya kudhibiti taka za kielektroniki ili kulinda Mazingira na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkundwe Mwasaga leo Novemba 6, 2024 amefungua mkutano wa kudhibiti taka za kielektroniki unaoshirikisha nchi za Ghana,Senegal,Kenya,Zambia na Tanzania
Mgeni rasmi katika ufunguzi huo ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Tanzania Dr. Nkundwe Mwasaga aliyemuwakilisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa(Mb.)
Akiongea kwenye Mkutano huu, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Tanzania Dr. Nkundwe Mwasaga amesema, "Leo hii tunajadiliana kuhusiana taka za vifaa vya Elektroniki (e-Weste) Tanzania na Nchi nnyingine Duniani tupo katika hatua za Mapinduzi ya Kidigitali. Mapinduzi ya kidigitali yanahitaji Vifaa. Kwa Tanzania kwa mfano Simu janja zinazoonekana kwenye Mifumo yetu zinaoneka Milioni 21, Baada ya muda hivyo vifaa vitakuwa vimeisha umri wake wa kufanya kazi, vikishaisha Umri wake wa kufanya kazi inatakiwa iwangaliwe namna bora ya hizotaka kuchukuliwa. Kuna njia mbili. Moja kurejeleza na mbili ni kuchukua hiyo taka na kuiteketeza."
Ameongeza kwamba "Mkutano huu ni mkubwa na tunajadili ni jinsi gani tunaweza kutengeneza mfumo ambao umekaa vizuri wa kurudisha kama kifaa kikiisha muda wake. Kuna kapuni zipo zinachukua. Huu Mkutano umekutanisha wataalam mbalimbali. Tunajadiliana tunajifunza na kuangalia jinsi gani tunaweza kupata Fursa kwa kuvijana kupata kipato. Kanuni za kudhibiti hizi kata zipo, hili swala la vifaa vya elektroniki ni Mtambuka. Idadi ya vifaa vya Elektroniki ni nyingi. Hivyo ni jukumu kuangalia mnyororo wa kuziondoa taka hizo. Tanzania inazalisha tani laki mbili kila mwaka ya Taka za Elektroniki."
Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira Bi. Lilian Lukambuzi wa NEMC
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Sware Semesi, aliwakilishwa na Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira wa NEMC Bi. Lilian Lukambuzi.
Akiongea kwenye Mkutano huo, Bi. Lilian Lukambuzi, amesema "Mkutano huu Umewakusanya wadau mbalimbali ambao wanafanya shughuli za kudhibiti taka za elektroniki. Kama mnavyofahamu, sasa hivi tumehamia kwenye matumizi ya Tehama ambapo matumizi ya vifaa vya elektroniki Majumbani na maisha yetu ya kwaida yamekuwa yakiongezeka kila siku. Na kadili idadi ya watu inavyoongezeka na matumizi yake yanazidi kuongezeka. Changamoto sasa ni tuna vifaa vya elektroniki ambavyo muda wake wa matumizi unaisha na pia ndani yake kuna vitu vina adhari ya kiafya na kimazingira. Sasa tunaangalia namna ya njia salama ya kuteketeza au kuona namna tukawa na matumizi mbadala ya Vifaa hivi vya elektroniki baada ya kuondoa vile vitu ambavyo vinaleta madhara kwenye mazingira. Tayari sisi kama Tanzania tulifanya maboresho kwenye sera ya mazingira iliyolrnga kuangalia ni mambo gani ambayo yameibuka Ulimwenguni ambayo sasa yanaleta changamoto, Moja wapo ilikuwa ni udhibiti wa taka za kietroniki."
Amesema baraza hilo limeshaandaa andiko kwaajili ya kuomba fedha WB za kutekeleza mradi wa kudhibiti taka za kielektroniki. Amesema matumizi ya vifaa vya kielektroniki yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku hali ambayo inasababishwa na ongezeko kubwa la watu. Vifaa hivyo ambavyo vimekuwa vikiisha muda wake wa matumizi visipowekewa mpango wa njia salama ya kuziteketeza vina athari kubwa ya afya ya binadamu na mazingira.
“Tayari Tanzania tulifanya maboresho kwenye sera ya mazingira mwaka 2007 na mwaka 2021 tukaja na sera mpya iliyoangalia mambo gani yaliyoibuka ulimwenguni ambayo yanaleta changamoto ikiwemo namna ya kudhubiti taka za kielektroniki, 2021 tulitunga pia kanuni ya kudhibiti taka za kielektroniki kwa hiyo tuna sera na kanuni za kushughulikia changamoto hiyo,” amesema Bi. Lilian Lukambuzi.
Naye Mwakilishi wa benki ya dunia, Jane Kibbassa, wakati akizungumza kwenye mkutano wa kudhibiti matumizi ya zebaki na taka za kielektroniki ili kulinda Mazingira, amesema benki ya dunia inatekeleza mradi wa kudhibiti zebaki kwenye nchi tano Afrika ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Senegal na Ghana kupitia mfuko wa Global Environment Facility (GEF) ambapo Benki ya Dunia (WB) imeahidi kuipatia Tanzanian fedha za kutekeleza mradi huu.
“Kwa sasa Tanzania inatekeleza mradi wa kudhibiti zebaki na imefanya vizuri sana kwa hiyo kwenye mradi wa kudhibiti taka za kielektroniki tuko kwenye mchakato wa kuwapatia fedha kama tulizotoa kwenye nchi zingine ili watekeleze mradi huu. Nchi za Kenya, Uganda, Senegal na Ghana zilipewa fedha za kutekeleza miradi yote miwili ule wa kudhibiti zebaki na taka za kielektroniki, Tanzania inashughulikia mradi mmoja wa kudhibiti zebaki lakini iko kwenye mchakato wa kuomba fedha za kutekeleza mradi wa kudhibiti taka za kielektroniki,” amesema
Mradi huo unatekelezwa katika Nchi 5 barani Afrika ambazo ni Tanzania, Kenya, Senegal, Zambia na Ghana na umelenga kupata suluhu na namna bora ya udhibiti wa Kemikali ya zebaki (mercury) na taka za hatarishi za kielektroniki ili kutunza Mazingira na Afya ya viumbe hai kwa kushirikishana Teknolojia na Mikakati ya utekelezaji.
Ni muendelezo wa mkutano uliojadili namna ya kudhibiti matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu kwa nchi husika ulioanza Novemba 4, 2024 na kutarajiwa kuhitimishwa Novemba 12, 2024. Mkutano huo unafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.