DAR: Polisi yapiga marufuku mazoezi ya kukimbia 'Jogging' barabarani bila kupata vibali

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267

Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar es salaam, kimepiga marufuku vikundi vyovyote vinavyoathiri vikiwemo vile vya mazoezi ya kukimbia bila kupata kibali.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa huo Marison Mwakyoma ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza katika mahojiano ya ana kwa ana na HabariLeo, jijini Dar es salaam leo Jumanne.

Ameshauri kuwa ili kikundi kiweze kufanya jambo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine litaathiri matumizi ya barabara ni lazima kipate kibali kutoka kwa mkuu wa Jeshi la Polisi.

Marufuku hiyo imetolewa baada ya uwepo wa vikundi maarufu vya Jogging ambavyo vimekuwa vikifanya mazoezi katikati ya barabara jambo ambalo linaathiri matumizi ya barabara.

Chanzo: Habarileo
 
Jamani ....,sasa hii Miili yetu hasa kina dada bila mazoezi itakuwaje!!‍♀️
 
Reactions: lun
Sawa kabisa... Tusipozingatia utaratibu wa matumizi sahihi ya barabara ni rahisi kusababisha ajali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…