Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewafungia leseni madereva 30 kati ya 179 waliokamatwa katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya 2025.
Madereva hao 30 walikamatwa katika operesheni maalumu na walipopimwa walikutwa na ulevi kwa kiwago cha zaidi ya miligramu 80.
Soma Pia: Mbeya: Madereva wa mabasi ya New Force, Zanuni, Rungwe Express, Super Rojas, Abood Bus Service na Kyela Express wafungiwa leseni kwa muda
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Murilo leo Alhamisi, Januari 2, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya usalama jijini Dar es Salaam.
Kamanda Murilo amesema madereva hao walikamatwa na jeshi hilo kabla na baada ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya 2025.