LGE2024 Dar: Prof. Kitila Mkumbo ashiriki kupiga kura, asema wananchi wasichukulie poa uchaguzi huu

LGE2024 Dar: Prof. Kitila Mkumbo ashiriki kupiga kura, asema wananchi wasichukulie poa uchaguzi huu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Manzese Mtaa wa Kilimani, Manispaa ya Ubungo Dar Es Salaam.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Baada ya kupiga kura Prof. Kitila ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki zoezi hilo ambalo ni haki yao kikatiba na wauchukulie uchaguzi huu kwa uzito kwani ni wa muhimu kama ilivyo kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Aidha Prof.Kitila amepongeza wasimamizi wa uchaguzi pamoja na wananchi wa eneo hilo kwa kuendelea kutunza hali ya amani huku akielezea matumaini yake ni uchaguzi kuisha kwa amani na matokeo kutangazwa kwa haki.
 
Mkutano wake wa juzi Manzese ulikuwa aibu tupu
 
Back
Top Bottom