Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Manzese Mtaa wa Kilimani, Manispaa ya Ubungo Dar Es Salaam.
Baada ya kupiga kura Prof. Kitila ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki zoezi hilo ambalo ni haki yao kikatiba na wauchukulie uchaguzi huu kwa uzito kwani ni wa muhimu kama ilivyo kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Aidha Prof.Kitila amepongeza wasimamizi wa uchaguzi pamoja na wananchi wa eneo hilo kwa kuendelea kutunza hali ya amani huku akielezea matumaini yake ni uchaguzi kuisha kwa amani na matokeo kutangazwa kwa haki.