Dar: Rais Samia Suluhu ahudhuria mechi ya Simba na Yanga

Leo kwenye derby ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba rais Samia amehudhuria mechi hiyo huku akiwa na tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa Corona ikiwemo kuvaa barakoa na kufanya social distance.

Cha ajabu mashabiki wengine wamejazana huku wakimshangilia rais Samia na mpira bila kuvaa barakoa wala tahadhari yoyote dhidi ya ugonjwa wa Corona.
 
Hivi walisema sababu za kuahirisha ile ya kwanza? SSH alikuwepo Dar?

Ni sawa lakini.
 
Nimeitafuta hiyo mechi, sijaipata inaonyeshwa Chanel gani? natumia Azamtv
 
Hivi wazungu wanapomuona anafanya hivyo anafikiri wanamuelewaje?
 
Kwa hiyo...
 
Leo Chama na serikali vilikua uwanjani ndio maana tukafungwa.
 
Unapoandika humu ni lazima ujipe muda wa kufikiria mkuu jamiiforum inatofauti na facebook mkuu.
 
Ndomana tunataka Katiba mpya. Hapa Kuna Rais Samia na Rais Karia, nini hiki Sasa? Katiba mpya itamke kua Rais ni mmoja tu, kiongozi wa mhimili wa Serikali. Hao Marais wengine wabadilishwe majina waitwe hata Wenyeviti.

Mwishowe hata Mimi nitajiita Rais wa Nyumba yangu Sasa.
 
Serikali imshonee rais pamoja na viongozi wa serikali mask nzuri; siyo kumvalisha mask za kumfanya aonekane kimbe cha ajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…