Dar: RC atangaza usafi wa nyumba kila mwisho wa mwezi

Dar: RC atangaza usafi wa nyumba kila mwisho wa mwezi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam (RC), Amos Makalla ametangaza kuwa kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi itakuwa siku maalumu ya kufanya usafi kwa wakazi wa mkoa huo.

Makalla ametoa agizo hilo leo Jumatatu Novemba 22, 2021 kwenye uzinduzi wa mkakati wa usafi na uhifadhi mazingira wa mkoa huo uliopewa jina la 'Safisha Pendezesha Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo watendaji kuanzia ngazi ya Serikali za mitaa wamesaini mkataba wa utekelezaji wake kwa kusaini fomu maalumu kila mmoja.

Katika mkakati huo Makalla amesema moja ya mambo yaliyopo ni kuifanya siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku rasmi ya kufanya usafi.

Makalla amesema katika siku hiyo, kila mmoja anapaswa kutekeleza wajibu wake kuanzia ngazi ya kaya, ili wananchi kujumuika katika kufanya usafi.

'Wewe Mwenyekiti Serikali ya Mtaa, Mtendaji hamasisha watu wako kufanya usafi na Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kwa kuwa ndio itakuwa rasmi ya kufanya usafi katika mkoa huu,

"Pia Mkuu wa Wilaya ndio atakuwa mratibu wa shughuli hiyo na kuwa mgeni rasmi katika shughuli mbalimbali za ufanyaji usafi katika maeneo yake kwa namna watakavyojipangia"amesema Makalla.

Katika mkakati huo pia amesema baadhi ya nyumba za watu binafsi, mashirika na kampuni yanapaswa kupakwa rangi na tayari ameshawapa baadhi barua ya kufanya hivyo.

Amewaonya watu ambao wamekuwa wakingoa na kuondoa urembo mbalimbali zilizowekwa kupendezesha mji na kueleza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

RC Makalla amewataka mameya na wakurugenzi kwenda kuziangalia upya sheria ndogondogo za usimamizi wa mazingira na usafi kuona namna gani wanaziboresha ili ziweze kufanya kazi kulingana na wakati wa sasa.

MWANANCHI
 
Kwa taarifa yako tu Mr Makala, lile daraja la waendao kwa miguu kuvuka barabara pale Mbezi Magufuri bus terminal halijapakwa rangi na limegeuzwa kuwa dampo na sehemu ya kujisaidia haja ndogo.

Ukilazimisha nyumba ya bi kidude ipakwe rangi ilihali bi kidude amelipa kodi ili kukamilisha ujenzi wa barabara za jiji hili, hela yote kamaliza nadhani utakuwa umejitakia laana mwenyewe, so usije laumu wenye jiji
 
Watengeneze sheria ndogo mtu yyte atakaetupa taka akamatwe alipe fain 50,000 aliyemkamata anapewa 25,000 iliyobaki inakwenda serikalin.
Hapo kila mtu atakuwa mlinzi wa mwingine. Kongole Makalla.
 
Usafi wa majumbani kweli 🙄🙄🙄

Haya...na wale wanaofanya kila siku wanapewa zawadi gani?🤔
 
Milori imewashinda kuondoa kariakoo,
Watu wote wamehama sasa mutayaambia malori yasafishe?
Mji umekuwa kama gereji
Mumeonea bure wamachinga
 
Tembea baba makala kariakoo ujionee malori yanavyochafua na kuziba njia na kuharibu mandhari nzuri ya jiji la kariakoo
Kariakoo upande wa kata ya misheni kota ni gereji mzee wala sio jiji tena
Hizi ndio shida za kushuhulikia sio usafi ambao kajenjere wanajitahidi kusimamia na raia wanalipa hela sio bure
 
Akumbushe watu kupamda miti pembezoni mwa barabara na kila mwenye duka hausike kuutunza huo mti mpaka ukue.
 
Pale wananchi wanapotaka kiongozi wao asikike akizungumzia changamoto zao za msingi kama maji,umeme,masoko,usafiri etc,then unasikia minor issues kama hizi,hili linchi ni la kuondoka tu sasa mss!
 
Niache kwenda kanisani eti nifanye usafi ngoja nimsubirie huyo mjumbe wa kuja kuniambia hayo
Nakumbuka enzi za bashite na magu.. mjumbe alikuja kuniamsha eti usafi nilimtoa nduki ukizingatia nilikuwa bado nipo vyombo wikiendi hiyo
 
Ahsante kwa taarifa...

Hivi hakuna mambo ya maana ya kuhimizana...
 
Back
Top Bottom