Dar: Simba yafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba SC 3-1 Nkana FC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Ni mechi ya kupindua matokeo na kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, leo Disemba 23, 2018 kwa wawakilishi wa Tanzania, Simba SC watakapokuwa wakikwaruzana na Nkana FC kutoka nchini Zambia katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kaa pamoja na Timu ya JF kukuletea mtanange huu wa kukata na shoka kuanzia saa 10: 00 jioni. Usikose Ukaambiwa.
Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Taifa ni dakika 90 za mchezo Ligi ya Mabingwa Afrika

Naam mpira umeanza uwanja wa Taifa

Simba wameanza kwa kulishambulia lango la Nkana FC..ambapo shuti la Bocco linadakwa na golikipa wa Nkana FC

10' Ligi ya Mabingwa Afrika hakuna timu imepata bao

Simba 0-0 Nkana FC

17' Gooooooooaaal Walter Bwalya anaipatia Nkana FC bao la kwanza kwa kichwa kufuatia krosi iliyopigwa.

Simba imeamka inaamua kutumia mashuti ya mbali sasa

Simba SC 0-1 Nkana FC

Nyoni anajaribu kupiga shuti kali goo laaaa..Mpira unagonga mwamba na kurudi uwanjani.

Pamoja na kuwa nyuma ya bao moja bado Simba wanaliandama lango la Nkana FC

29' Gooooooooooaaal Gooooooooooaaal..Jonas Mkude anaisawazishia Simba bao kwa shuti la umbali mrefu na kwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha golikipa wa Nkana Chibwe, akiruka bila mafanikio, kumbuka ni pasi safi kutoka kwa Cleoutus Chama

Simba SC 1-1 Nkana FC

Nkana wanajaribu kutumia mashambulizi ya kushtukiza hapa uwanja wa Taifa.

40' Ligi ya mabingwa Afrika uwanja wa Taifa, Simba wanapanga mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Nkana

Simba 1-1 Nkana FC

45+2 kuelekea kuwa mapumziko Simba wanaliandama lango la Nkana huku Nkana wakijaribu kuzuia

45+1' Gooooooooooaaal Gooooooooooaaal Mk14 Mfumba Jicho Meddie Kagere anaipatia Simba bao la pili kwa kichwa safi kufuatia mpira wa Krosi ya Nicholas Gyan iliyotokana na kona fupi iliyopigwa na Cleoutus Chama

Simba SC 2-1 Nkana FC

Naaaaaaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wanatoka uwanjani wakiwa mbele ya mabao mawili dhidi Ya bao moja la Nkana FC


Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Taifa na hakuna mabadilko kwa pande zote mbili

Simba SC 2-1 Nkana FC

49' Simba wanapanga mashambulizi kuelekea lango la Nkana FC

Wanachukua Nkana sasa..Lakini wanapoteza anachukua Wawa upande wa Simba

Kona kuelekea lango la Nkana FC..Bocco gooo laaa, ilikuwa hatari lango la Nkana

53' Anatoka Nicholas Gyan anaingia Juuko upande wa Simba

57' mpira ni mkali kwa pande zote mbili..huku Simba wakihitaji goli moja tu kuweza kufuzu michuano hii ya mabingwa afrika.

87' Simba wanapoteza nafasi nzuri ya kufunga..ilikuwa ni hatari sana

88' Gooooooooooaaal Gooooooooooaaal
Mwamba wa Lusaka Cleoutus Chota Chama, Triple C, anaipatia Simba bao la tatu akipiga kwa kisigino kufutia pasi safi Hassan Dilunga hivyo kuihakikishia Simba inafuzu michuano hii Ligi ya Mabingwa ya Afrika

89' Ligi ya Mabingwa Afrika uwanja wa Taifa kuelekea kumalizika mchezo huu

Simba SC 3-1 Nkana FC
(Agg) 4-3

90+3' Naaaaaaaam mpira umekwisha uwanja wa Taifa. Simba wanaibuka kwa ushindi wa mabao matatu dhidi ya moja la Nkana FC

Kwa matokeo hayo Simba imefuzu hatua ya makundi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao manne kwa matatu kufuatia mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Zambia ambapo Nkana FC waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Simba SC

Simba SC 4-3 Nkana FC

Asante sana wote mlioshiriki hapa JF

Ghazwat...

SIMBA YAFUZU KUCHEZA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA

Klabu ya Simba imefuzu kuingia hatua ya makundi michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuifunga klabu ya Nkana FC ya Zambia goli 3-1

Magoli ya Simba yamefungwa na Mkude 29', Kagere 45+1' na Chama 88' huku goli la Nkana likifungwa na Bwalya 17'. Hivyo Simba inasonga kwa jumla ya magli 4-3

Timu kutoka Tanzania inafuzu kucheza Klabu Bingwa Afrika ikiwa ni baada ya miaka 15


Habari zaidi.

Dar es Salaam. Timu ya Simba imetinga hatua ya makundi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Nkana mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Nkana imetolewa kwa jumla ya mabao ya mabao 4-3 huku ikiangukia kwenye Kombe la Shirikisho.

Licha ya kufunga bao lililoifanya Simba kuwa mbele ya Nkana Red Devels kipindi cha kwanza kwa mabao 2-1, mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere alipiga pasi nne.

Kagere ambaye mara kadhaa alikuwa akipoteza mipira ameifungia Simba bao hilo mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kuanzwa kwa kona fupi.

Simba ilianza kutanguliwa kwenye kipindi hicho cha kwanza kabla ya muda mchache baadaye kusawazisha kwa shuti kali la kiungo, Jonas Mkude.

Ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza aliyrpiga pasi nyingi kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba ni Mganda Emmanuel Okwi mwenye pasi 11, John Bocco alipiga sita zilizowafikia walengwa.

Aliyepiga pasi chache zaidi kwenye kikosi cha Simba ni mlinda lango wao, Aishi Manula ambaye ameruhusu nyavu zake kuguswa mara moja.
 
Gyan na Wawa sina imani nao labda wajirekebishe ,kila la heri SIMBA
 
ADUI MWOMBEE NJAA, sitaki unafiki niliwahi kuiombea heri SIMBA Kwa moyo wangu wote Mechi yake na ATLETICO SPORTS AVIACAO ya Angola mwaka 1993 Ile ya Kina Kanka wemba, Yanda, Abilio, Amanali, Bravo(c), libenge nk LEO NIKO NA NDUGU ZANGU TUNAOUNGANISHWA NA TAZARA.
 
Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Taifa...Timu zote zipo uwanjani tayari kwa ukaguzi. Ambapo mgeni rasmi Waziri wa Viwanda.
 
Waamuzi wanatoka Kenya,
Kenya ni Jirani na Tanzania kuliko Zambia,
 
Naaaaaaaam mpira umeanza uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Simba SC 0-0 Nkana FC
 
05' Bocco anapiga shuti kali..Lakini golikipa anadaka.

Simba SC 0-0 Nkana FC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…