Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Ukipita Morogoro Road, njia ambayo mabasi ya mwendokasi ndiyo yalianza kufanya kazi zake hapa Dar es Salaam, utagundua kwamba vituo vya daladala za kawaida ukiachana na mwendo kasi, hakuna sehemu ambayo abiria anaweza kusubiri daladala akiwa sehemu tulivu.
Vituo vyote katika barabara hiyo, hakuna sehemu ya abiria kupumzika kama ilivyo kwa vituo vingine vya Mandela Road, Nyerere Road, Kawawa Road, Bagamoyo Road.
Mvua ikinyesha, jua likiwaka, vyote vinaishia mwilini mwa abiria wakiwa wanasubiri gari.
Tunaomba mamlaka husika, liliangalie suala hili kwa sababu imekuwa kero ya muda mrefu.