Yaani hao jamaa inatakiwa waminywe mambupu wataje mtandao wao wote wakamatwe ,zamani mimi nilikuwa natumia mtungi wa gesi kwa miezi miwili fresh ila kwasasa ni mwezi tu unaisha.
Wafanyabiashara wawili pamoja na mitungi zaidi ya 451 ya gesi ya kupikia wanadaiwa kukamatwa katika operesheni iliyofanywa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za uchakachuaji na kupunguza ujazo wa gesi kwenye mitungi kabla ya kuiuza kwa wananchi.
Katika eneo la Maramba Mawili, jijini Dar es Salaam, maafisa wa mamlaka za Serikali walibaini nyumba inayodaiwa kutumika kwa shughuli za uchakachuaji wa mitungi ya gesi.
Afisa wa Ufundi na Mafunzo wa TZLPGA, Huruma Msigwa, amesema shughuli hizo zilikuwa zikifanyika katika eneo hilo huku baadhi ya majirani wakisema hawakuwa na taarifa kuhusu kinachoendelea ndani ya nyumba hiyo.
Pia soma:
~EWURA na TBS tunaomba mlifuatilie suala la ujazo wa gesi za kupikia
~Kuna uchakachuaji wa ujazo wa mitungi ya Gesi kwa baadhi ya Kampuni; Wananchi tunaumia
Wakiwa matajiri tunaambiwa tupambane kama wao, wakikamatwa tukishangilia tunaambiwa tuna roho mbaya, ukweli nimefurahi sana.
Wafanyabiashara wawili pamoja na mitungi zaidi ya 451 ya gesi ya kupikia wanadaiwa kukamatwa katika operesheni iliyofanywa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za uchakachuaji na kupunguza ujazo wa gesi kwenye mitungi kabla ya kuiuza kwa wananchi.
Katika eneo la Maramba Mawili, jijini Dar es Salaam, maafisa wa mamlaka za Serikali walibaini nyumba inayodaiwa kutumika kwa shughuli za uchakachuaji wa mitungi ya gesi.
Afisa wa Ufundi na Mafunzo wa TZLPGA, Huruma Msigwa, amesema shughuli hizo zilikuwa zikifanyika katika eneo hilo huku baadhi ya majirani wakisema hawakuwa na taarifa kuhusu kinachoendelea ndani ya nyumba hiyo.
Pia soma:
~EWURA na TBS tunaomba mlifuatilie suala la ujazo wa gesi za kupikia
~Kuna uchakachuaji wa ujazo wa mitungi ya Gesi kwa baadhi ya Kampuni; Wananchi tunaumia
Yaani dunia hii vituko Tu, wakifanikiwa wanatunanga Sisi wavivu, wakifulia n Sisi tumawananga tunaitwa Wachawi kwa kufurahia anguko laoWakiwa matajiri tunaambiwa tupambane kama wao, wakikamatwa tukishangilia tunaambiwa tuna roho mbaya, ukweli nimefurahi sana.