Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kusimamia mkakati wake maalum wa kuzuia vitendo vyote vya kihalifu katika Jiji la Dar es Salaam. Kazi hii maalum ya kuzuia vitendo vya kihalifu ni muendelezo wa kazi hiyo iliyoanza mwezi Aprili 2024 na inayoedelea kulenga, kufuatilia, kuchunguza na kukamata wahalifu mbalimbali pamoja na wanaopanga njama za kuiba, kuvunja nyumba, wanaouza, kusafirisha na kutumia dawa za kulevya.
Katika hatua hiyo tarehe 21 Mei 2024 maeneo ya Kipunguni B, Ukonga Jeshi la Polisi lilimkamata Hassan Yahya cobra na wenzake watatu wakitumia dawa za kulevya aina ya bangi huku wakipanga njama za kufanya vitendo vya kihalifu yakiwemo makosa ya unyang’anyi.
Watuhumiwa hao walikutwa na pistol toy 7, AK47 toy 2, Jambia toy 2, shoka toy 2, kama sehemu ya maandalizi ya kufanya kuhalifu.
Jeshi la Polisi litaendelea kujikita katika kuzuia matukio ya kihalifu kwa kuafutilia kwa karibu makundi yote ya watu na hasa wanatumia dawa za kulevya na kufanya matukio ya kihalifu.
Jumla ya watuhumiwa 13 wanaohusika na kuuza, kusafirisha na kutumia dawa za kulevya ikiwemo bangi walikamatwa ikiwa ni pamoja na Hamis Seif (18) Mkazi wa Mbondole na Bosco Bosco (18) Mkazi wa Kipunguni Ilala.
Watuhumiwa hao wamekamatwa na Puli 531 na kete 2,639 na misokoto 158 ambayo ilikuwa tayari kutumiwa wakiwa pia na viroba vinne vya bangi pia pikipiki mbili MC 673 CKM na MC 591 CUW zilizokuwa zinatumika kusambaza bangi hizo pia zimekamatwa.
Kwa upande wa usalama wa barabarani Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kuwafuatilia, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani madereva wasiotii Sheria na Kanuni za usalama barabarani wakiwemo walevi na makosa hatarishi ya wapanda pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu.
Kwa kipindi cha mwezi Aprili hadi Mei 2024 Jumla ya makosa 67 ya pikipiki yalikamatwa yakihusisha kutokuwa na leseni, kuzidisha abiria na kuendesha pikipiki wakiwa wamelewa ambapo madereva 21 walifikishwa mahakamani, na wengine walitozwa faini za papo hapo.
Madereva wa magari 6 walikamatwa kwa makosa ya kuendesha wakiwa wamelewa ambapo madereva 2 walifikishwa mahakamani na wengine 4 walitozwa faini papohapo.
Vilevile katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Mei 2024, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam katika kusimamia mifumo ya haki jinai lilifanikiwa kupata matokeo Mahakamani ya watuhumiwa mbalimbali.
Ikiwa ni pamoja na Agustino Daniel (22) Mkazi wa Vingunguti alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kulawiti kwenye Mahakama ya Wilaya Kinyerezi. Conradi Nnkuru (43) mkazi wa Msongola kwenye Mahakama hiyo hiyo ya Kinyerezi alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.
Unyang’anyi wa kutumia silaha washtakiwa 3 kwenye Mahakama ya Wilaya Temeke walipata adhabu ya kifungo miaka 30 jela akiwemo Mikidadi Juma (40) mkazi wa Mbagala.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za kweli zitakazo pelekea kukamatwa kwa halifu haraka kabla hawajatekeleza uhalifu wao.
Imetolewa na;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam