LGE2024 Dar: Wananchi Mtaa wa Sinza B walalamika majina kutobandikwa kituoni

LGE2024 Dar: Wananchi Mtaa wa Sinza B walalamika majina kutobandikwa kituoni

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,



Wananchi wa Mtaa Sinza B, Wilaya ya Ubungo Dar Es Salaam wamelalamikia kutokubandikwa kwa majina yao nje ya kituo cha kupiga kura cha Shule ya Sekondari Mashujaa jambo linalopekea wao kusumbuka mpaka kupata majina.

Jambo TV imezungumza na baadhi ya wananchi waliofika kituoni hapo akiwemo Hekima Mwasipu ambaye amesema toka saa mbili asubuhi lakini mpaka kufikia saa tatu(muda tuliofika Jambo TV) majina hayakuwa yamebandikwa.

Wananchi wengine wameendelea kulalamikia kadhia hiyo huku wengine wakifikia maamuzi ya kuondoka ili kwenda kuendelea na shughuli zao.

Jambo TV imefanya jitihada ya kuzungumza na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kituoni hapo lakini hawakuwa tayari kutoa ushirikiano.
 
Back
Top Bottom