Dar: Wanne mbaroni kwa Uchochezi wa Kidini!

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,423
Reaction score
3,297
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za uchochezi wa kidini.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema watu hao walikamatwa katika msako maalum unaoendeshwa na jeshi hilo katika hali ya kukabiliana na hatua zozote zenye lengo la kuleta chuki na ubaguzi wa kidini nchini.

Aliwataja watu hao kuwa ni Kombo Hassan (32), mkazi wa Mburahati Barafu, Basote Hassani (24) Mkazi wa Gongo la Mboto, Mohamed Hassan (33) Mkazi wa Tabata Bima na Salum Athuman (46) Mkazi wa Tunduma.

"Mtuhumiwa wa kwanza ambaye ni Kombo Hassan, tulimkamata akiwa na nyaraka nyingi za aina mbalimbali alizokuwa akisambaza na wenzake jijini Dar es Salaam pamoja na mikoani kwa makusudi ya kuleta mfarakano wa kidini nchini.

"Baadhi ya nyaraka hizo ni pamoja na nyaraka zinazochochea chuki na vurugu dhidi ya Serikali na taasisi nyingine, kundi hili pamoja na watu wengine ambao bado wanatafutwa limebaini kuwa na mtandao wa mawakala sehemu mbalimbali nchini," alisema.

Kamanda Kova alisema jeshi la Polisi litaendelea na msako mkali nchi nzima, ili kuwabaini wote wanaojihusisha na uchochezi kwa lengo la kuleta vurugu na uvunjifu wa amani.

Alisema upelelezi wa shauri hilo unaendelea sanjari na jalada la kesi kupelekwa kwa Wakili wa Serikali, ambaye atathibitisha kiwango cha tuhuma hizo na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa makosa yatakayobainika.

Kamanda Kova alisema, Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua wale wote wanaoleta uchochezi kupitia shughuli za kidini au kisiasa pia amewataka wananchi wote wapenda amani bila kujali dini au itikadi yoyote kuungana kwa pamoja, ili kuhakikisha kwamba watu wachache wenye nia mbaya wasifanikiwe kuharibu amani ya nchi yetu ambayo imezoeleka.

Katika hatua nyingine, alisema jeshi la Polisi linashirikiana na benki mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Benki Kuu ili kudhibiti mianya ya wizi katika mashine maalum za kuchukulia fedha (ATM).

Alisema hivi karibuni kuna wahalifu kutoka ndani na nje ya nchi ambao wametengeneza mtandao wa wizi katika ATM.

"Baadhi ya watu hao tumeshawakamata na kuwafikisha mahakamani na mashauri yao yanaendelea," alisema Kamanda Kova.

Chanzo: Gazeti la Mtanzania

Maoni yangu:
Watu wote wanaokamatwa kwa uchochezi wa aina yoyote wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine na pia hili tatizo lifike kikomo.
 
usisahahu kuwakamata waliotuibia fedha zetu na kuzificha Uswis au kauli hii nayo ni ya uchochezi?
 
Tunataka isiwe moto wa mabua! Uwe wa makaa ya mawe ya kudumu. Kamata wote hata wanauza DVD! Magazeti yanayoiandika habari za uchochezi na radio za kidini ikibaini ka imerusha kipindi chenye nia ya uchohezi zote zifungiwe. Serikali isione aibu kwa hilo!
 
mmmh hao kina HASANI ni dugu moja!!!
 
Wachochezi au wasema kweli? Kuweni wazi ukweli hautakiwi! Ujinga ndo amani au sio? Haya bhanaa!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ee Mungu tuponye na huyu Ibilisi anayetuchochea Watz tuchukiane kwa tofauti za dini. Tusiichezee hii amani tuliyonayo ndugu zangu, tutakuja juta baadaye. Na tukumbuke siku zote "Majuto ni Mjukuu"
 
naombeni namba ya kova kuna vibanda vya maustadhi bugurun chama, tandika na hapa mbagala. Vinavyohasisha chuki na umoja wa watz.
 
Wakamateni wote na wachukuliwe hatua za kisheria, lkn sio kesho tunawona mitaani wakiendelea na uchochezi.
 
Nampongeza KAMANDA KOVA,silaha kama zingekuwa zinazagaa hovyo tungekuwa tunashuhudia mauaji ya kujitoa mhanga tulipofika
 
:rockon:Jeshi la Polisi Dsm linawashikilia watu wanne kwa uchochezi wa kidini. source Mwananchi News paper
 

Gazeti la Al-NUUR bado lipo?
 
naombeni namba ya kova kuna vibanda vya maustadhi bugurun chama, tandika na hapa mbagala. Vinavyohasisha chuki na umoja wa watz.
Nenda kituo chochote cha polisi na utoe taarifa kwa siri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…