Dar: Waziri Aweso amemsimamisha Meneja wa DAWASA, Kinyerezi Burton Mwalupaso Kwa kushindwa kutekeleza vyema majukumu yake

Dar: Waziri Aweso amemsimamisha Meneja wa DAWASA, Kinyerezi Burton Mwalupaso Kwa kushindwa kutekeleza vyema majukumu yake

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
AWESO AMUWEKA PEMBENI MENEJA DAWASA KINYEREZI, MALALAMIKO YA WANANCHI YACHANGIA

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemsimamisha Meneja wa DAWASA Kinyerezi Burton Mwalupaso Kwa kushindwa kutekeleza vyema majukumu yake ikiwa ni pamoja na kushindwa kujua Takwimu kamili za mahitaji ya Maji kwenye eneo hilo sambamba na malalamiko mengi ya wananchi.

Waziri Aweso ametoa maelekezo hayo Leo Julai 1, 2024 wakati akizungumza na Wananchi wa Tabata Kinyerezi katika ziara yake ya kukagua hali ya huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam.

Awali Waziri Aweso alimuhoji Meneja huyo kutoa Takwimu za mahitaji ya Maji na uzalishaji katika Kata ya Kinyerezi ambapo awali alijibu kuwa Kata hiyo Ina watu takribani 62,304, huku mahitaji ya Maji yakiwa ni Lita 600,081 (Laki sita na themanini na Moja) kwa mwezi, na baada ya kuulizwa Tena akaeleza kuwa mahitaji ni Lita 22,704 Kwa siku, huku akishindwa kueleza namna alivyopata Takwimu hiyo.

Waziri Aweso Leo Julai 1, 2024 ameanza rasmi ziara ya kikazi katika mikoa ya huduma ya Maji inayotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) akiwa na lengo la kufuatilia hali ya huduma ya Maji na kusikiliza changamoto za wananchi.

---
Pia soma
 
Maji ya DAWASA yanatoka machafu sana siku hizi, huyo meneja anastahili kilichompata.
 
Wale mafundi walio chepusha maji na kuuza kimagendo wamemponza.
Nayeye ilikuaje akashindwa kusimamia eneo lake la kazi kwa weledi hadi haya yote yanayokea, tena wateja wakihudumiwa maji machafu..??
 
Maji ya DAWASA yanatoka machafu sana siku hizi, huyo meneja anastahili kilichompata.
Meneja anatoa peda yake mfukoni kununua dawa za kusafisha maji kule Ruvu chini na Juu ? Vipi serikali kama haitoi pesa kununua madawa hayo ? Ukiwekwa wewe leo utapata wapi pesa madawa kama serikali imeuchuna? Achana na wanasiasa
 
Wewe ndie msemaji wa meneja au mfanyakazi wa Dawasa?

Hilo jibu lako umeegemea kwa meneja bila kuwa na uhakika wa unachojibu, ndio maana umeishia kuniuliza maswali.

Nataka maji safi na salama, sio tope linalotoka siku ya tatu sasa.
 
Huyu aweso aende yeye kuwa Mkurugenzi wa duwasa tuone atafanya Nini, wanasiasa wanajua kubwabwaja tu
 
Back
Top Bottom