Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akunjua Makucha. DAWASA Waanza kulimia meno. Aendelea na Utumbuaji kwa Mameneja Wazembe.
Ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake Mkoani Dar na maeneo yote yanayo hudumiwa na DAWASA, Waziri Aweso ameendelea kuchukizwa na utendaji Mbovu wa DAWASA.
"Ukicheka na nyenyere anayekutambalia kwenye Mapaja, atakung'ata Pabaya". Amesema Aweso.
DAWASA KATA YA MAKONGO WATOA HAMASA KWA WAZIRI WA MAJI
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) kata ya makongo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam wametoa hamasa kwa Waziri wa Maji Juma Aweso kufanya kazi bila kuchoka katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma muhimu ya maji safi na salama.
Wametoa hamasa hiyo leo Julai 2, Katika ziara ya Waziri Aweso Jijini humo ambapo alipata wasaa wa kukutana na kuzungumza na DAWASA katika kata hiyo
Waziri Aweso ameitaka menejimenti hiyo kufuatilia na kutatua changamoto ya maji kwa Wanannchi kwa kuwashirikisha viongozi wa serikali za mitaa.
WAZIRI AWESO AFURAHISHWA NA HUDUMA KWA WATEJA WA MAJI
Waziri Aweso amefurahishwa na kauli njema kutoka mmoja wa wahudumu kwa wateja wa maji wakati alipopiga namba hiyo ambayo ni 0800110064 inayo patikana bila malipo na kuongea na mhudumu huyo kwa lengo la kuhakikisha kama wananchi wanapata huduma bila usumbufu.
Amefanya zoezi hilo akiwa katika ziara yake Julai 2 jijini Dar es salaam alipotembelea Mtaa wa Kibululu Kata ya Goba Wilayani Ubungo alipokutana na wananchi na kusikiliza malalamiko na kero zao juu ya huduma hiyo muhimu.
“Huduma kwa wateja tuwasikilize wananchi na kutatua kero zao na eneo la maunganisho ya Maji lifanyiwe kazi ipasavyo.
Kuna mabadiliko makubwa yanakuja DAWASA”
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiwa Katika Mkutano na wananchi wa Makongo eneo la Goba Center Zahanati.
AWESO AWASHA MOTO MANUNUZI DAWASA KUHUSU VIFAA VYA MAUNGANISHO
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) makao Makuu kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kushuka ngazi za chini na kufuatilia changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo uunganishaji maji, pamoja na kuhakikisha wanawaunganishia maji Wananchi wote ambao tayari wameshalipia huduma hiyo Kwa muda mrefu.
Waziri Aweso ametoa maelekezo hayo Leo Julai 2, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wananchi Kata ya Goba Wilayani Ubungo, katika mkutano uliofanyika Mtaa wa Kibululu muda mfupi baada ya kumpigia simu Mkurugenzi wa Manunuzi DAWASA Makao Makuu Bi. Hellen Lubogo ambaye alitakiwa kuwepo kwenye ziara hiyo, baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu changamoto hiyo ya Wananchi kulipia huduma bila kufungiwa mabomba yao.
Amesema kuwa tangu kuanza Kwa ziara yake kumekuwepo na malalamiko mengi ya Wananchi kuhusu changamoto hiyo, ambapo takribani watu 30,000 (Elfu Thelathini) wameomba kuunganishiwa maji lakini hawajaunganishwa, huku akiwasisitizia watendaji wa Mamlaka hiyo kufanya kazi Kwa moyo wa kuwasaidia Wananchi kila mmoja Kwa nafasi yake.
“WAMAMA TUMEJAA UTI NA FANGASI”
“Kila kukicha tunaogea maji ya kisima wamama tumejaa UTI na fangasi waziri tukisema utukague huku utalia Vizazi vinaisha lete maji safi”
Hiyo ni kauli ya mmoja wa wananchi waliokuwa wanatoa malalamiko na kero za maji mbele ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa katika ziara yake Jijini Dar es salaam leo Julai 2, 2024 katika kata ya kibamba mtaa wa Malamba mawili wilayani Ubungo.
MALAMBA MAWILI YAKATISHA KIBARUA CHA MENEJA DAWASA KIBAMBA
Waziri wa maji Jumaa Aweso amemsimamisha kazi
Meneja wa DAWASA Kibamba anaye julikana kwa jina la Elizabeth Sankere, kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji katika eneo hilo changamoto iliyodumu kwa muda mrefu.
“Eliza umefanya kazi kwa muda mrefu hapa kwahiyo mimi nikiondoka naomba tuondoke pamoja, sasa mimi niombe kwakuwa katibu mkuu wetu wa Wizara ya Maji ni mama naomba hii kazi usimamie mwenyewe katibu mkuu” Aweso
Ametoa uamuzi huo Julai 2 wakati wa ziara yake Jijini Dar es salaam katika mtaa wa Malamba mawili, kata ya Kibamba wilayani Ubungo baada ya Wananchi wa eneo hilo kutoa malalamiko kwa meneja huyo aliehudumu eneo hilo kwa kipindi cha miaka minne kuhusu adha ya maji wanayoipata.
AWESO: NI MARUFUKU KUKATA MAJI "SIKU YA SIKUKUU au WEEKEND"
MWANANCHI: DAWASA WENIITIA POLISI WAKANIWEKA NDANI BAADA YA KUDAI MAJI,. WAZIRI AWESO: HAYA WEWE INGIA KWEYE GARI YANGU TUTAONDOKA WOTE