Daraja la Ileje kubomoka: Uhandisi Tanzania umeshuka Viwango?

Unafaamu daraja lilijengwa na watu gani? Usiwe unaongea vitu usivyo na uhakika navyo.
Soma hiyo post! Whether injinia alikuwa mchina au mkolea, alijenga kwa standards zilizoidhinshwa na mainjinia wa kitanzania. Limefunguliwa March 14, likabomoka March 16; uhandisi gani huo!
 
Na wewe unaamini kuwa kuwa injinia huyo hakujali uwekaji foundation, bali yeye alikimbilia kuweka beam tu; nimekuelewa? Hiyo ni engineering gani sasa!
kuna vitu vigumu kuainishwa. mfano ubora au hali halisi ya uwezo wa nguzo kubeba uzito mkubwa hasa zilizojengwa kwa mawe miaka mingi iliyopita. huwa hazionyeshi uharibifu wake. Hivyo mhandisi aliamini uwezo wa nguzo hizo na hivyo kuendelea kuzitumia na kupitisha magari mazito. inaonekana yeye aliamini maji ndiyo yaliyokuwa sababu ya daraja la mwanzo kuharibika NA SIO UWEZO WA NGUZO.HIVYO KUAMUA KUWEKA DARAJA JUU YA NGUZO IMARA KUMBE SIO. NAMSIKITIKIA KWA JANGA HILI.
 
That is not engineering mzee wangu! Kazi kama hiyo hata babu yangu angeweza kuifanya. Kama wewe ni injinia, ukiangalia picha hiyo ya failure vizuri kama Exhibit A; ni kwamba daraja lile limefeli kwa sababu nyingi, siyo kudidimia kwa msingi tu.
 
Tz bado hatuna uwezo. Kuna kampuni Moja ya Ujenzi ya MEKO na Wahindi.....NYANZA ROADS CONSTRUCTION. Ina jenga barabara zote Kanda ya Ziwa na Kgm kwa jina la Mkubwa. Barabara zake ni mbovu na kichefuchefu tupu
Faivu tena.
 
Its possible to say that matumizi mabovu ya infrastructure pia yanaweza sababisha haya kutokea..
Engineer ame design daraja kwa ajili ya kupitisha mizigo isiyozidi tani 2, anakuja mtu anaruhudu semitrailer kama hiyo kupita,unategemea nini?
So hatuishii ku assess kazi ya Engineer tu bali hata wale wanaowekwa kusimamia hiyo miradi inapokamilika
 
Hilo daraja lilikuwa designed kupitisha crane??
Naangalia hiyo picha naona kama ni suala la uzito ndiyo limevunja daraja. Kama mzigo uliopitishwa ulikuwa mkubwa, labda ndiyo tatizo!
Kwa uelewa wangu mdogo madaraja hata barabara kuna MAX weight allowed.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Waambie wahusika wakupatie taarifa za namna gani walijenga hilo daraja.
 
Yes hoja yako ni kweli kabisa kuwa kam daraja lilikuwa designed kwa tani 2 halafu mtu akaruhusu tani 5 kupita, basi daraja litafeli. Ila katika planning process ya ujenzi wowote, huwa kunafanyika survey ya possbile load capacity, halafu injinia anapiga safety factory kama 2.5 au 3, kwa hiyo kosa dogo la gari zaidi ya uwezo kupita mara moja haliwezi kuporomosha daraja lilijengwa siku mbili tu zilizopita. Ni kama vile hiyo preliminary capacity analysis haikufanyika iwapo argument yako ni sahihi.
 
Unaweza kutuonesha hilo lililosombwa kabla ya hili kujengwa?
 
Unaweza kutuonesha hilo lililosombwa kabla ya hili kujengwa?
Soma hiyo post vizuri; modereta aliongeza vitu ambavyo sikuwa nimeandika lakini vinasaidia sana kuelewa hoja yangu. Kuna daraja la zamani lililokuwepo lilifeli, kwa hiyo akaja mkandarasi kulijenga upya, alipomaliza ujezi wake March 14, bado likafeli tena Machi 16.
 
Uko sawa mkuu lakini Engineer hajengi madaraja kutoka mfukoni mwake.
Hapo tunaona source of failure na tunaona vizuri kuwa hilo Bailey bridge lilivyo structurally sound.

Serikali haikuwekeza katika abbutment supports.
Ni kama yameegeshwa mawe au gabions na daraja likachukuliwa store na kuwekwa juu.

Fedha ya kuweka abbutments haikuwepo kwa mantiki hiyo.
Sasa tumlaumu engineer kwa lipi.
Na sidhani kama hapo alikuwepo Consulting Engineer wala Contractor, bali Client mwenyewe kajenga hilo-Force Account.
 
Tz bado hatuna uwezo. Kuna kampuni Moja ya Ujenzi ya MEKO na Wahindi.....NYANZA ROADS CONSTRUCTION. Ina jenga barabara zote Kanda ya Ziwa na Kgm kwa jina la Mkubwa. Barabara zake ni mbovu na kichefuchefu tupu
Dar ndo usiseme, hio kampuna imekuka tenda kibao na bado Kuna ambazo zinaendelea. Sasa Kama ilikuwa ya mkubwa naiona ikifa kifo cha mende
 
Uko sahihi sana.
Ila nature of failure ya hilo daraja ni kwenye abutments,.means structure ni stable ila bearing capacity ya ile soil ndo imeshindwa ku resist ile load.
 
Hili la FORCE ACCOUNT kama ilivyokuwa kwa TASK FORCE linaenda kuisha kama si kesho basi muda utasema.
Force account imeondoa ajira nyingi na mzunguko wa fedha mtaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…