Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amesema Daraja la JP MAGUFULI (Kigongo-Busisi), linalounganisha mkoa wa Mwanza na Geita, linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.Akikagua Ujenzi wa Daraja hilo leo tarehe 24 Januari 2025 mkoani Mwanza, Waziri Ulega amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi bilion 611 kugharamia daraja hilo hadi sasa.
View: https://youtu.be/2X2mAhcsi0I?si=bFR7smY17nKI01dE
Mradi wa kihistoria wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) unaendelea kusonga mbele kwa kasi kubwa, ambapo hadi sasa umefikia asilimia 96.3 ya utekelezaji wake. Daraja hili linatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 2025.
Daraja hili, ambalo litakuwa refu zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki likiwa na urefu wa kilomita 3.2, limekuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa mikoa ya Mwanza na Geita na maeneo ya jirani. Kwa sasa, wananchi wanategemea huduma za kivuko ambazo zimekuwa changamoto kubwa hasa wakati wa msongamano wa magari na mizigo.
Lengo kuu la mradi huu ni kuhakikisha kuwa mawasiliano kati ya mikoa ya Kanda ya Ziwa yanaboreshwa, kupunguza gharama za usafirishaji, na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa maeneo yanayohusika.