Daraja la Langai, Simanjiro: Mkandarasi amesimama ujenzi, Wakazi Walia hatari ya maisha

Isack888

Member
Joined
May 16, 2024
Posts
27
Reaction score
43
Wakazi wa Langai wapo katika hali ya wasiwasi kutokana na kusimama kwa ujenzi wa daraja ambalo lilitarajiwa kuwa kiunganishi muhimu cha usafiri na usalama wa wakazi wa eneo hilo. Mwananchi mmoja ameibua hofu kubwa baada ya mtu kusombwa na maji kwenye daraja hilo, ambalo ujenzi wake haujakamilika.

Changamoto Zinazoendelea

Daraja hilo lilianza kujengwa kwa nia ya kuboresha miundombinu ya eneo hilo, lakini kwa mujibu wa wakazi wa Langai, mkandarasi aliyekuwa akihusika na ujenzi amesimama kazi bila kutoa maelezo yoyote. Hali hii imeacha daraja likiwa nusu ujenzi. Picha zilizopigwa eneo hilo zinaonyesha uharibifu wa udongo na uwezekano mkubwa wa athari zaidi kwa jamii, hasa msimu wa mvua unapoongezeka.

Mwananchi mmoja, ambaye sauti yake imerekodiwa kutoka katika Group la Whatsapp, ameeleza kwamba serikali inapaswa kuchukua hatua haraka ili kuhakikisha ujenzi wa daraja hilo unakamilika. “Daraja hili ni muhimu sana kwa sisi wakazi wa Langai. Kukwama kwa ujenzi wake sio tu kwamba linatuathiri kiuchumi, lakini pia linahatarisha maisha yetu,” alisema.

daraja-1.jpg

TARURA/TANROADS pakavu huko hakuna hela kabisa wakandarasi wengi wamekimbia site
 
View attachment 3173907

Dah aisee nimekumbuka mbali sana,
Henzi hizo upo kwenye simanjiro express full unatoka zako chuga kupitia Mererani ukifika hapo Langai dukani kwa Sauti ya Dume babu upo na vumbi full .....ukishuka unakutana na wamasai full mashuka wao wanakushangaa wewe ulivyovaa suruali, dah aiseee.....!!!
 
  • Thanks
Reactions: al1
Wakazi wa Langai wapo katika hali ya wasiwasi kutokana na kusimama kwa ujenzi wa daraja ambalo lilitarajiwa kuwa kiunganishi muhimu cha usafiri na usalama wa wakazi wa eneo hilo. Mwananchi mmoja ameibua hofu kubwa baada ya mtu kusombwa na maji kwenye daraja hilo, ambalo ujenzi wake haujakamilika.

Changamoto Zinazoendelea

Daraja hilo lilianza kujengwa kwa nia ya kuboresha miundombinu ya eneo hilo, lakini kwa mujibu wa wakazi wa Langai, mkandarasi aliyekuwa akihusika na ujenzi amesimama kazi bila kutoa maelezo yoyote. Hali hii imeacha daraja likiwa nusu ujenzi. Picha zilizopigwa eneo hilo zinaonyesha uharibifu wa udongo na uwezekano mkubwa wa athari zaidi kwa jamii, hasa msimu wa mvua unapoongezeka.

Mwananchi mmoja, ambaye sauti yake imerekodiwa kutoka katika Group la Whatsapp, ameeleza kwamba serikali inapaswa kuchukua hatua haraka ili kuhakikisha ujenzi wa daraja hilo unakamilika. “Daraja hili ni muhimu sana kwa sisi wakazi wa Langai. Kukwama kwa ujenzi wake sio tu kwamba linatuathiri kiuchumi, lakini pia linahatarisha maisha yetu,” alisema.

View attachment 3173907

Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom