Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Daraja la Mto Tegeta linalounganisha maeneo ya Salasala na Tegeta Machinjioni limekuwa kikwazo kikubwa kwa Wananchi wa maeneo hayo tangu lisombwe na maji ya mvua mapema Mwaka 2024.
Licha ya umuhimu wake kwa mawasiliano na uchumi wa eneo hilo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kulikarabati daraja hilo, jambo ambalo linaendelea kuzua sintofahamu na changamoto kwa wakazi.
Daraja hilo, maarufu kama 'Daraja la Gwajima,' lilijengwa kwa juhudi binafsi za Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, lakini halikudumu hata miezi miwili baada ya kusombwa na maji, lilikuwa msaada mkubwa, sasa wananchi tunalazimika kupita bondeni au kufanya mzunguko mrefu kufika upande wa pili.
Wakazi wameonyesha wasiwasi mkubwa hasa kuelekea kipindi hiki mvua zikitarajiwa kuanza tena, wakihofia kukosa kabisa mawasiliano ya moja kwa moja.
Wito kwa Mbunge Askofu Gwajima na Serikali kuingilia kati na kuhakikisha daraja hilo linajengwa kwa ubora unaostahili, likiwekwa juu zaidi na kutanuliwa ili maji na uchafu vinapopita visiliharibu tena.
Daraja hilo, lililo karibu na Ofisi za TANESCO, ni kiungo muhimu kwa Wakazi wanaohitaji huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Hii hali sio salama kabisa, mvua zikianza hakuna pa kupita. Hatua za haraka zinahitajika kabla ya athari kubwa zaidi kuwakumba.
Hii hali sio salama kabisa, mvua zikianza hakuna pa kupita. Hatua za haraka zinahitajika kabla ya athari kubwa zaidi kuwakumba.