DOKEZO Daraja lasombwa na maji wilayani Kilindi Tanga

DOKEZO Daraja lasombwa na maji wilayani Kilindi Tanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nguva Jike

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2018
Posts
1,226
Reaction score
1,757
Habari za asubuhi.

Mvua kubwa iliyonyesha jana usiku wa tarehe 15.12.2024 wilayani Kilindi Tanga imesababisha daraja linalounganisha vitongoji viwili muhimu katika Kijiji cha Mgera kata ya kisangasa kusombwa na maji.

Kitongoji cha Shule kina shule ya msingi na shule ya sekondari na Zahanati.Kukatika kwa daraja hilo kumesababisha watu washindwe kuvuka upande wa pili.

Wananchi pia wana hofu kubwa ya watoto wao watapata shida kwenda shuleni shule zitakapofunguliwa January 2025.Huduma za afya pia zitatetereka ikiwemo wakulima na mifugo yao.

Viongozi wa serikali wameombwa kufanya juhudi ili huduma ziendelee kupatikana.Pia daraja la kibereshi limekatika kutokana na mvua hizo.
 
Mnaposema viongozi wa serikali wameombwa kufanya juhudi kwa kitu ambacho ni haki ya wananchi hii haijakaa sawa, maana wanalipwa mishahara na posho kwa kodi za wananchi hao hao.
 
Back
Top Bottom