Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Wananchi wa kata ya Lemara na Sinoni mkoani Arusha katika wilaya ya Arusha wamekosa mawasiliano kwa kipindi cha miaka minne tangu daraja linalounganisha Kata ya Themi Lemara na Sinoni lisombwe na mvua.
Kwa muda wote huo wananchi wamekuwa wakilalamika wawekewe daraja lakini viongozi kutoka serikali za mitaa walikuja mara moja kuangalia na hawakurudi tena na wananchi hawajui kinachoendelea hadi sasa.
Kipindi cha mvua ambako maji ni Mengi kuna watu hujitolea na kuweka daraja la mianzi na hivyo wananchi hao hulipia sh mbili( 200) kuvuka,hivyo basi kwenda na kurudi hutumia Mina nne(400) .
Na kipindi ambacho sio cha mvua basi wananchi hulazimika kuruka juu ya mawe ili kuvuka ng'ambo ya pili.
Daraja hili ni kiunganishi muhimu sana kutokana na kwamba kata ya Themi na Lemara ndiko kuliko na idadi kubwa ya shughuli za Kiuchumi kama vile viwanda hivyo hivyo basi idadi ya wananchi wanaovuka kutoka Sinoni kuelekea katika Kata za Themi na Lemara.
mmoja wa wananchi akikatiza katika mto huo kutokea kata ya Lemara kuelekea kata ya sinoni