SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kwenye suala la jezi, moja ya kitu cha kuzingatia unapoangalia uwezo wa jezi kuhimili joto siyo tu material iliyotumika kama baadhi ya watu wanavyodhani lakini pia rangi. Hii ni kwa sababu rangi zina uwezo tofauti wa kuhimili au kupitisha joto.
Rangi nyeupe ndiyo rangi ya kwanza ambayo ina uwezo mkubwa wa kuzuia joto kupita. Hii inasaidia wachezaji wasipate moja kwa moja joto la jua maana linagonga kwenye jezi bila kupenya. Angalia mechi ambazo Simba inavaa jezi nyeupe utaona jezi zinaloana kuliko kawaida. Hii ina msaada wa kutunza energy ya wachezaji.
Rangi nyeusi ndiyo rangi ya kwanza inayooongoza kupenyeza joto kupita katika nguo. Hii ina maana katika mazingira yetu ya joto, ukivalisha wachezaji wako rangi nyeusi unawatesa maana joto la jua linapenya moja kwa moja kwenye jezi zao na kuifanya miili yao ihitaji kupambane zaidi ili kutengeneza energy anayohitaji mchezaji.
Mtiririko wa rangi kulingana na uwezo wake wa kuzuia joto kupita katika nguo uko hivi (kuanzia yenye uwezo sana hadi yenye uwezo mdogo):
1. Nyeupe
2. Nyekundu
3. Machungwa
4. Njano
5. Kijani
6. Blue
7. Nyeusi
Ndiyo maana duniani kote utaona timu nyingi zinavaa jezi nyeupe na/au nyekundu zaidi na chache saaana zinavaa njano, kijani au nyeusi. Kuna sababu nyingine lakini hii ni mojawapo.
Kwa maana hiyo, Yanga kwa upeo mdogo wa viongozi wao kuanzia kihistoria hadi leo wamerithishana, ilienda kuchagua rangi zote ambazo zinaongoza kwa uwezo mdogo wa kuzuia joto kupita. Halafu bado wanashangaa kwa nini timu yao imekuwa haifanyi vizuri miaka nenda rudi.
Simba kihistoria na mpaka leo ni klabu inayoongozwa na watu wenye upeo wa hali ya juu sana. Yanga kihistoria na mpaka leo inaongozwa na kuwa na mashabiki ambao tuseme tu kwa kulinda heshima yao, upeo wao ni wa kawaida.
Leo Deportivo la Utopolo nimewasanua, basi msibaki tena na umbumbumbu wenu.