Darasa huru katika kesi dhidi ya Mbowe

Darasa huru katika kesi dhidi ya Mbowe

S.M.P2503

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
2,421
Reaction score
4,344
Hii kesi ina ya Ugaidi ya makomandoo wa jeshi na kiongozi wa upinzani inayoendelea ina maajabu yake mpaka sasa, mimi nitataja machache, mengine ongezeeni.

1. Ni darasa huru la kuwafundisha polisi namna ya kufanya kazi zao kimaridadi sana, kama ule wimbo wa sigara mkononi, lakini hawana fedha mfukoni- PGO ingaliwe upya na polisi wafundishwe au kupigwa msasa mara kwa mara namna ya kutumia- iwe kama continous learning – CPD hivi.

2. Ni darasa huru kwa wanasheria wa makampuni kujifunza namna ya kufanya kazi na taasisi za umma, kujua namna ya kutunza faragha za wajeta na kwa makampuni kuhakikisha yanafanya due diligence wakati wanajibu barua toka huko mamlakani kama police etc. Yaani mtu yeyote anaweza kuandika barua kwenda kwenye hizi kampuni mradi tu ameandika toka polisi, wao mbio kwenda kuzijibu na kutoa taarifa za wateja bila kujiridhisha, sijui haya makampuni yalijifunza nini kwenye kesi ya Jamii forum (Maxence) vs Jamhuri juu ya kulinda taarifa za wateja.

3. Ni kesi inayoamsha hisia za watu juu ya uweledi wa watoa haki kama kweli wana uwezo stahiki wa kuwapa watu haki zao.

4. Ni kesi inayowafanya watu wafikilie na kujiuliza waalimu wa hawa majaji wetu ni akina nani, uwezo wao, machapisho yao na mambo mengineyo mengi kama hayo.

5. Inatoa maswali mengi badala ya majibu, hivi hawa mashahidi huwa wanalipwa kiasi gani wanapokuja kutoa ushahidi wao, maana nahisi ni kama kuna motisha fulani hivi, mfano hivi hawa Airtel wakiamua kumfukuza mtu kazi kwa kutofuata due deligence huko airtel na kutolinda faragha za mteja, huyu mtu (shahidi) atafidiwaje na serikali? Je, watamlipa hadi kiinua mgongo kwa kutofuata miongozo yake ya kazi huko kwenye kampuni yake?

6. Ya nini kushupaza shingo na kuwashuhudia wengine uongo hapo kizimbani? Mbona judge ni muoga sana kuwakalipia wanaoidanganya mahakama mchana kweupe au na yeye ni sehemu ya washitaki badala ya kuwa neutral na kuweka mambo sawa anapoona mambo hayafuati sheria?

7. Kama nchi safari bado ni ndefu, asante Mungu kwa kututoa upofu watanzania na kutupa darasa huru katika kesi hii.

Mengineyo ongezeeni. Povu ruksa.
 
Hata wewe hauko huru yote haya unayaona kwakuwa upo bias na tayari unahukumu yako mkononi.Haki ya kusikiliza pande zote na kutoa hukumu IPO mikono mwa chombo kinachoruhusiwa kisheria kila kesi ikiingiliwa kila mmoja atatoa hukumu kwa kujipendelea.

Tatizo kubwa zaidi ni kujiona unaelewa kila fani duniani na kwasababu unajilinganisha na hewa huwezi kujua kama hujui na kwakuwa hutaki kujua kwamba hujui utabakia hivyo hivyo na hutapata mtu wa kukujibu.
 
Ushahidi wa haya yote uko wapi ndugu yangu?
 
Hoja yako ni nini hapa we dogo?
 
Hawezi kufukuzwa kwani serikali ni bosi wa Airtel, mfanyakazi wao.
Sasa wateja wakirudi nyuma je. Kuna wakati Pepsi walipata shida sana baada ya zawadi kutoonekana kwenye soda zao...
 
Hii kesi ina ya Ugaidi ya makomandoo wa jeshi na kiongozi wa upinzani inayoendelea ina maajabu yake mpaka sasa, mimi nitataja machache, mengine ongezeeni.

1. Ni darasa huru la kuwafundisha polisi namna ya kufanya kazi zao kimaridadi sana, kama ule wimbo wa sigara mkononi, lakini hawana fedha mfukoni- PGO ingaliwe upya na polisi wafundishwe au kupigwa msasa mara kwa mara namna ya kutumia- iwe kama continous learning – CPD hivi.

2. Ni darasa huru kwa wanasheria wa makampuni kujifunza namna ya kufanya kazi na taasisi za umma, kujua namna ya kutunza faragha za wajeta na kwa makampuni kuhakikisha yanafanya due diligence wakati wanajibu barua toka huko mamlakani kama police etc. Yaani mtu yeyote anaweza kuandika barua kwenda kwenye hizi kampuni mradi tu ameandika toka polisi, wao mbio kwenda kuzijibu na kutoa taarifa za wateja bila kujiridhisha, sijui haya makampuni yalijifunza nini kwenye kesi ya Jamii forum (Maxence) vs Jamhuri juu ya kulinda taarifa za wateja.

3. Ni kesi inayoamsha hisia za watu juu ya uweledi wa watoa haki kama kweli wana uwezo stahiki wa kuwapa watu haki zao.

4. Ni kesi inayowafanya watu wafikilie na kujiuliza waalimu wa hawa majaji wetu ni akina nani, uwezo wao, machapisho yao na mambo mengineyo mengi kama hayo.

5. Inatoa maswali mengi badala ya majibu, hivi hawa mashahidi huwa wanalipwa kiasi gani wanapokuja kutoa ushahidi wao, maana nahisi ni kama kuna motisha fulani hivi, mfano hivi hawa Airtel wakiamua kumfukuza mtu kazi kwa kutofuata due deligence huko airtel na kutolinda faragha za mteja, huyu mtu (shahidi) atafidiwaje na serikali? Je, watamlipa hadi kiinua mgongo kwa kutofuata miongozo yake ya kazi huko kwenye kampuni yake?

6. Ya nini kushupaza shingo na kuwashuhudia wengine uongo hapo kizimbani? Mbona judge ni muoga sana kuwakalipia wanaoidanganya mahakama mchana kweupe au na yeye ni sehemu ya washitaki badala ya kuwa neutral na kuweka mambo sawa anapoona mambo hayafuati sheria?

7. Kama nchi safari bado ni ndefu, asante Mungu kwa kututoa upofu watanzania na kutupa darasa huru katika kesi hii.

Mengineyo ongezeeni. Povu ruksa.
Unatumika weledi wakitanzania sehemu nyingi ndio maana tunaona sarakasi zote hizi🤸.
 
Back
Top Bottom