Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hamisi Hababi: Assalaam Alaikum, jana nilikuwa na Mzee Kissinger na nikamsimulia andiko lako mtandaoni kuhusiana yeye na Hafidh Kido, na akafurahi sana nilimpomwambia yeye ni Mwalim na wewe ni mwanafunzi, akaishia kusema "Mohamed mtundu sana" mimi sina digrii yeye ana madgrii.
Waleikum Salaam Warahmatullah Wabarakatuh,
Ingekuwa dunia imeegemeza elimu katika karatasi za shahada ulimwengu ungegubikwa na ujinga na watu wajinga.
Allah kwa rehema zake kaiweka elimu ndani ya ubongo wa viumbe wake mfano wa mwalimu wangu Mzee Kissinger, marehemu Sheikh Ali Abbas na wengineo.
Nilialikwa Kenyatta University, Nairobi kutoa mada kuhusu mchango wa Uislam Afrika ya Mashariki.
Kichwa changu kitupu lakini kwa mbali nina jina la sheikh mmoja alikuwa na msaada mkubwa sana kwa maraisi wawili waliotawala Tanzania.
Tatizo sikuwa najua ilikuwaje huyu sheikh awe makhsusi kwa viongozi hawa. Siku hizo niko Tanga.
Nikaja Dar es Salaam kwa Mzee Kissinger kumweleza nilipokwama. Subhanallah.
Kwanza kacheka. Alianza na maisha ya sheikh, mtoto mdogo lakini ana ari kubwa ya kusoma.
Katiwa chuoni kwao Bagamoyo na baba yake akasoma lakini akaona pale ataishia hapo hapo yeye alitaka aipate elimu iliyokuwa ndani ya vyuo vikuu vya dunia.
Aliingia ndani ya jahazi kuja mjini, Dar es Salaam na miaka hiyo majahazi yanatia nanga Msasani.
Alipofika Msasani akauliza atafikaje Kariakoo?
Miaka hiyo ni enzi ya mabasi ya Dar es Salaam Motor Transport (DMT) hakuna basi linalokwenda Msasani.
DMT inakwenda Ilala, Buguruni, Temeke, Kinondoni na Oysterbay kwa ajili ya wafanyakazi Waafrika mashambaboi na wapishi wa Wazungu.
Akaonyeshwa barabara ya vumbi inayopita katikati ya pori akaambiwa aifuate hiyo barabara aulize mbele ataelekezwa lilipo soko la Kariakoo.
Kafika Kariakoo masikini mtoto mdogo wa kishamba kavaa kanzu na kabeba kifurushi cha nguo zake kasimama pale sokoni hajui pa kwenda.
Msamaria Mwema akamuona muda mrefu yule mtoto kazubaa pale anashangalia mabasi ya DMT (kwani hapo kulikuwa na kituo chake) na wapita njia.
Akamwendea kumuuliza anapokwenda. Hajui aendako. Ila kaja mjini anasema anataka kusoma.
Haukuchukua muda mrefu yule bwana kutambua kuwa huyu mtoto anaezungumzanae ana msingi mzuri wa elimu.
Akamchukua hadi kwa Sheikh Uwesu Mtaa wa Gogo na si mbali na hapo mwendo wa dakika tano tu kwa miguu.
Sheikh Uwesu alikuwa Khalifa wa Quadiriyya na hapo Mtaa wa Gogo mtaa mdogo si zaidi ya nyumba 20 ndipo ilipokuwa Zawiyya yake.
Sheikh Uwesu alikuwa na kundi la wanafunzi anawasomesha hapo. Akampokea mtoto yule akamwambia aunge mstari nyuma kwa wenzake aanze masomo.
Bagamoyo taharuki. Baba yake hajui mwanae kapotelea wapi isiwe kazama pwani.
Wavuvi wakamwambia wamemuona mwanae na kimzigo chake kapanda jahazi.
Kufupisha kisa. Baba yake alimkuta chuoni kwa Sheikh Uwesu.
Mzee Kissinger anasema alipomtazama bwana mkubwa yule anaingia mlangoni pale chuoni alijua ni baba wa mwanafunzi wake mpya kwa jinsi walivyoshahabiana.
Sheikh Uwesu akamwambia baba wa mtoto asimchukue anwache pale kwani keshaanza kusoma.
Kijana alikuwa katoka Bagamoyo kwenye shina la Qadiriyya na zilipokuwa zikisomwa nyuradi aliiona hifdhi yake na kuisikia sauti ya mwanafunzi wake ikiongoza.
Alimpenda mwanafunzi wake huyu.
Zawiyya hii ya Sheikh Uwesu mimi nimeiona kwa macho yangu udogoni kwani tulikuwa na nyumba yetu Mtaa wa Gogo No. 6.
Huyu mtoto alisoma na akaendelea na masomo yake Pakistan wakati wa Alama Abdu Ala Maudud na aliathiriwa sana na msomi huyu.
Kubwa Allah alichojaaliwa huyu sheikh kijana ilikuwa sudi.
Ukimsikia akizungumza utampenda achilia mbali kuwa Allah alimpa sura jamil na haiba kali.
Aliporejea Tanganyika Shariff Abdulkadir Juneid Imam wa Msikiti wa Kitumbini akamchukua kama msaidizi wake.
Hakuna mlango ambao hakufunguliwa huyu sheikh kijana hata bila miadi pamoja na mlango wa Ikulu na nyumbani kwa Nyerere Msasani.
Jina lake likitajwa mawaziri watatoka ndani za ofisi zao kumlaki na kumkaribisha ndani.
Hivi ndivyo alivyokuja kuwatumikia maraisi wawili waliotawala nchi hii.