Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074

Mzee Kissinger
Nimefika kwenye walima wa harusi ya bint wa ndugu zangu akina Tambaza aliyenipokea Sheikh Ali Sindo.
Uwanja umejaa lakini badala ya kunitafutia mahali pa kukaa ananipeleka kwa Mzee Kissinger nikamuamkie ndipo anionyeshe mahali pa kukaa.
Kissinger kaka pembeni kidogo katika kiti si jamvini akiwa pamoja na Mwinyikhamis Mussa na Muharram Kobe.
Baada ya kutoa salaam tu Mzee Kissinger ananiambia, ‘’Mohamed kuna mambo katika mkasa wa Sharif Mwinyibaba hukuandika katika kitabu cha marehemu Abdul…’’
Hapo hapo nikapiga Bismillah na kushukuru, Alhamdulillah… kimoyomoyo.
Nilitambua kuwa nimekuja na mguu mzuri kwanza nitakula biriani na vilevile nitasomeshwa.
Baada ya kumaliza kula karamu haraka nimemkimbila Mzee Kissinger nipige goti kalamu na karatasi mkononi nisomeshwe.
Lakini siku hizi kalamu na karatasi hazina kazi tena zetu za mkononi zinamaliza kila kitu. Zinachukua picha na sauti kwa wakati mmoja.
Mzee Kissinger baada ya miaka 16 kupita toka ilipotoka tafasiri ya Kiswahili cha kitabu cha Abdul Sykes ndiyo kwanza kakisoma sasa na ananieleza kuwa amekuwa akikisoma usiku hadi amekimaliza.
Lakini kuna kipande katika historia ya Sharif Badawy na kaka yake Sharif Hussein sikueleza chote kwa ukamilifu wake.
Shariff Hussein Badawy
Inawezekana kuwa Shariff Hussein Badawy na nduguye Mwinyibaba wakawa ndiyo Waafrika wa kwanza Tanganyika kupigwa PI yaani Prohibited Immigrants – Wahamiaji Wasiotakiwa.
Nini kisa cha ndugu hawa wawili kufukuzwa Tanganyika mwaka wa 1963, miaka miwili tu baada ya Tanganyika kupata uhuru wake?
Katika Maulid ya Mfungo Sita mwaka wa 1963 Mwinyibaba alipanda jukwaani kujibu hotuba ya sheikh mmoja maarufu na kiongozi wa juu katika TANU ambae katika hotuba yake vijana waliona kama vile alijikomba sana kwa serikali.
Majibu kutoka kwa kijana mdogo Mwinyibaba yalikuwa makali sana kama ilivyo ada ya vijana. Damu zao zinachemka na hawachagui maneno lile linalokuja ndipo hilo litatoka kinywani.
Mzee Kissinger alikuwapo katika maulid yale pale Mnazi Mmoja usiku ule na yeye pia kama alivyokuwa Mwinyimababa, pia alikuwa kijana.
Katikati ya khutba ya Mwinyibaba iliyokuwa inaunguruma katika vipasa sauti vilivyoenea pale uwanjani ilisikika sauti ikitokea sehemu ya nyuma karibu ya Hospitali ya Mnazi Mmoja ikipiga ukelele, ‘’Unachanganya dini na siasa.’’
Shariff Mwinyibaba akiwa Maulidini Lamu 2007
Sauti hii ilikuwa sauti maarufu hakuna katika mji wa Dar es Salaam mtu ambae alikuwa haijui sauti hii.

Wakwanza kushoto mbele ni Iddi Tosiri, watatu ni Julius Nyerere akifuatiwa na Kaluta Amri Abeid, Mstari wa mwisho wapili kulia ni Rashid Sisso. Picha hii ilipigwa miaka ya mwishoni 1950 New Street mbele ya ofisi ya TAPA (Tanganyika African Parents Association)
Hii ilikuwa sauti ya Rashid Sisso.
Mpigania uhuru, mmoja wa vijana wa mwanzo kuingia TANU na kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha wananchi kujiunga na TANU na kubwa zaidi Rashid Sisso alikuwa rafiki wa Mwalimu Nyerere.
Katika watu waliokwenda uwanja wa ndege kumsindiza Mwalimu Nyerere katika safari yake ya kwanza UNO, Rashid Sisso alikuwa mmojawapo pamoja na Idd Faiz Mafungo, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed, John Rupia, Zuberi Mtemvu, Robert Makange, kuwataja wachache.
Katika mikutano ya TANU Rashid Sisso akisimama nyuma ya Mwalimu Nyerere wakati akihutubia. Mwalimu Nyerere akampachika jina akawa anamwita, ‘’Afisa,’’ Hakuna ajuaye kwa nini alimpa jina hilo.
Sauti ya Rashid Sisso ili ilikuwa sauti ya onyo kali na Rashid Sisso hakuwa mtu wa kupuuzwa. Mwinyibaba alipuuza zauti ile na aliendelea na khutba yake kali hadi alipomaliza.
Watu walijua kuwa Mwinyibaba tayari alikuwa matatani.
Baada ya Maulid kumalizika walimwendea wakamwambia asisubiri hadi asubuhi akimbie aende kwao usiku ule ule kwani asubuhi taarifa itafika katika vyombo vya usalama na hakuna shaka yoyote askari watamfuata kumkamata.
Mwinyibaba hakupuuza ushauri ule.
Usiku ule ule majira ya saa sita usiku Mwinyibaba akapanda lori la mizigo lililokuwa linakwenda Tanga na hata kabla jua halijapanda siku ya pili Mwinyibaba alikuwa keshavuka mpaka wa Horohoro anaelekea kwao Mombasa.
Asubuhi siku ya pili mapema Mzee Kissinger anapita Msikiti wa Badawy Kisutu anaelekea kazini kwake African Printers, anawaona maofisa wa Uhamiaji Wazungu wawili wanaingia na viatu ndani ya msikiti wa Badawy kuwatafuta Sharif Hussein na nduguye Mwinyibaba kuwapa notisi za PI kuwa wanafukuzwa Tanganyika hawatakiwi kuwapo nchini.
Mzee Kissinger akasimama pembeni na watu wengine wakistaajabu kuwaona maofisa Wazungu wakiwa katika sare zao za kazi wakiingia msikitini bila ya kuvua viatu.
Notisi ile aliipokea Sharif Hussein peke yake.
Ilikuwa siku ya Ijumaa na alikwenda Msikiti wa Kitumbini kusali sala ya Ijumaa na baada ya sala alisimama na kuwaaga Waislam.
Hali ilikuwa ya simanzi sana kwani Sharif Hussein alikuwa na madras maarufu hapo msikitini akisomesha vijana na watoto na sifa kubwa ya madras ile ilikuwa usomaji wa tajwid, nyuradi na kasda za kupendeza katika maulid.
Kundi kubwa la Waislam lilimsikindikiza hadi kutoka Msikiti wa Kitumbini Masjid Badawy na baada ya hapo Sharif Hussein akaondoka kurudi kwao Kenya.
Haya ndiyo aliyonieleza mwalimu wangu Mzee Kissinger ambayo alinambia yalistahili niyaeleze katika kitabu cha Abdul Sykes.
MASAHIHISHO
Nimefika kwenye walima wa harusi ya bint wa ndugu zangu akina Tambaza.
Aliyenipokea Sheikh Ali Sindo.
Uwanja umejaa lakini badala ya kunitafutia mahali pa kukaa ananipeleka kwa Mzee Kissinger nikamuamkie ndipo anionyeshe mahali pa kukaa.
Kissinger kakaa pembeni kidogo katika kiti si jamvini akiwa pamoja na Mwinyikhamis Mussa na Muharram Kobe.
Baada ya kutoa salaam tu Mzee Kissinger ananiambia, ‘’Mohamed kuna mambo katika mkasa wa Sharif Mwinyibaba hukuandika katika kitabu cha marehemu Abdul…’’
Hapo hapo nikapiga Bismillah na kushukuru, Alhamdulillah… kimoyomoyo.
Nilitambua kuwa nimekuja na mguu mzuri kwanza nitakula biriani na vilevile nitasomeshwa.
Baada ya kumaliza kula karamu haraka nimemkimbila Mzee Kissinger nipige goti kalamu na karatasi mkononi nisomeshwe.
Lakini siku hizi kalamu na karatasi hazina kazi tena simu zetu za mkononi zinamaliza kila kitu.
Zinachukua picha na sauti kwa wakati mmoja.
Mzee Kissinger baada ya miaka 16 kupita toka ilipotoka tafasiri ya Kiswahili ya kitabu cha Abdul Sykes ndiyo kwanza kakisoma.
Mzee Kissinger akanieleza kuwa amekuwa akikisoma kitabu usiku hadi amekimaliza.
Lakini kuna kipande katika historia ya Sharif Badawy na kaka yake Sharif Hussein sikueleza chote kwa ukamilifu wake.
Inawezekana kuwa Sharif Hussein Badawy na nduguye Mwinyibaba wakawa ndiyo Waafrika wa kwanza Tanganyika kupigwa PI yaani Prohibited Immigrants – Wahamiaji Wasiotakiwa.
Nini kisa cha ndugu hawa wawili kufukuzwa Tanganyika mwaka wa 1963, miaka miwili tu baada ya Tanganyika kupata uhuru wake?
Katika Maulid ya Mfungo Sita mwaka wa 1963 Mwinyibaba alipanda jukwaani kujibu hotuba ya sheikh mmoja maarufu na kiongozi wa juu katika TANU ambae katika hotuba yake vijana waliona kama vile alijikomba sana kwa serikali.
Majibu kutoka kwa kijana mdogo Mwinyibaba yalikuwa makali sana kama ilivyo ada ya vijana.
Damu zao zinachemka na hawachagui maneno lile linalokuja ndilo hilo litatoka kinywani.
Mzee Kissinger alikuwapo katika maulid yale pale Mnazi Mmoja usiku ule na yeye kama alivyokuwa Mwinyibaba, pia alikuwa kijana.
Katikati ya khutba ya Mwinyibaba iliyokuwa inaunguruma katika vipasa sauti vilivyoenea pale uwanjani ilisikika sauti ikitokea sehemu ya nyuma karibu ya Hospitali ya Mnazi Mmoja ikipiga ukelele, ‘’Unachanganya dini na siasa!'’
Sauti hii ilikuwa sauti maarufu hakuna mtu katika mji wa Dar es Salaam ambae alikuwa haijui.
Hii ilikuwa sauti ya Rashid Sisso.
Kijana wa Bantu Group.
Mpigania uhuru, mmoja wa vijana wa mwanzo kuingia TANU na kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha wananchi kujiunga na TANU na kubwa zaidi Rashid Sisso alikuwa rafiki wa Mwalimu Nyerere.
Katika watu waliokwenda uwanja wa ndege kumsindiza Mwalimu Nyerere katika safari yake ya kwanza UNO, Februari 1955 Rashid Sisso alikuwa mmojawapo.
Wengine ni Idd Faiz Mafungo, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed, John Rupia, Zuberi Mtemvu, Robert Makange kwa kuwataja wachache.
Katika mikutano ya TANU Rashid Sisso akisimama nyuma ya Mwalimu Nyerere wakati akihutubia.
Mwalimu Nyerere akampachika jina akawa anamwita, ‘’Afisa."
Hakuna ajuaye kwa nini alimpa jina hilo.
Sauti ya Rashid Sisso ili ilikuwa sauti ya onyo kali na Rashid Sisso hakuwa mtu wa kupuuzwa.
Mwinyibaba alipuuza sauti ile na aliendelea na khutba yake kali hadi alipomaliza.
Watu wote waliokuwa pale maulidini walijua kuwa Mwinyibaba tayari alikuwa matatani.
Baada ya Maulid kumalizika walimwendea wakamwambia asisubiri hadi asubuhi akimbie aende kwao Mombasa usiku ule ule kwani asubuhi taarifa itafika katika vyombo vya usalama na hakuna shaka yoyote askari watamfuata kumkamata.
Mwinyibaba hakupuuza ushauri ule.
Usiku ule ule majira ya saa sita usiku Mwinyibaba akapanda lori la mizigo lililokuwa linakwenda Tanga na hata kabla jua halijapanda siku ya pili Mwinyibaba alikuwa keshavuka mpaka wa Horohoro anaelekea kwao Mombasa.
Asubuhi siku ya pili mapema Mzee Kissinger anapita Msikiti wa Badawy Kisutu anaelekea kazini kwake African Printers, anawaona maofisa wa Uhamiaji Wazungu wawili wanaingia na viatu ndani ya msikiti wa Badawy kuwatafuta Sharif Hussein na nduguye Mwinyibaba kuwapa notisi za PI kuwa wanafukuzwa Tanganyika hawatakiwi kuwapo nchini.
Mzee Kissinger akasimama pembeni na watu wengine wakistaajabu kuwaona maofisa Wazungu wakiwa katika sare zao za kazi wakiingia msikitini bila ya kuvua viatu.
Notisi ile aliipokea Sharif Hussein peke yake.
Ilikuwa siku ya Ijumaa na alikwenda Msikiti wa Kitumbini kusali sala ya Ijumaa na baada ya sala alisimama na kuwaaga Waislam.
Hali ilikuwa ya simanzi sana kwani Sharif Hussein alikuwa na madrasa maarufu hapo msikitini akisomesha vijana na watoto na sifa kubwa ya madrasa ile ilikuwa usomaji wa tajwid, nyuradi na kasda za kupendeza.
Kundi kubwa la Waislam lilimsikindikiza kutoka Msikiti wa Kitumbini hadi Masjid Badawy na baada ya hapo Sharif Hussein akaondoka kurudi kwao Kenya.
Haya ndiyo aliyonieleza mwalimu wangu Mzee Kissinger ambayo alinambia yalistahili niyaeleze katika kitabu cha Abdul Sykes.