Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
DARASA LA TANO C: WAZEE WA KUENGUA
Na, Robert Heriel
Leo nitasimulia kwa mtindo wa Filamu. Hii ni filamu ya maandishi. Karibu sana Mpenzi Msomaji.
Picha letu linaanzia katika maeneo ya shule ya Msingi CHIMBAUNYE huko katika kijiji cha SIWATUBORA. Huko ndipo simulizi hii inaanzia, nami Taikon nipo hapa kukusimulia yale yote yaliyojiri huko. (Ndandandanda..."Sauti ya beat kunogesha filamu inasikika).
Sasa nilikuwa nimeanza maisha mapya, maisha mageni katika eneo geni. Kama kuku mgeni asiyekosa kamba mguuni niliingia katika Shule ya CHIMBAUNYE, Ndiko huko SIWATUBORA.
Jinsi nilivyotembea kila aliyeniona alitambua kuwa mimi ni mgeni, wanafunzi wa Chimbaunye hawakuwa wanatembea kama mimi. Sare nilizokuwa nimevaa zilinitambulisha kama mgeni kwani Sare za Chimbaunye zilikuwa mbali sana na zangu. Si kwa kutokufanana rangi hasha! Bali Sare zangu zilikuwa nzuri sana, mpya na bora. Nilivalia shati jeupe nzuri lenye kung'aa, chini nikiwa nimevalia kaptura ya rangi ya kaki iliyovutia, chini nilivalia soksi za punda milia mpya kabisa na kiatu cheusi kilichopigwa kiwi kikang'aa.
Basi nikawa natembea, putu! Putu! Putu! Putu! huku nikiwaangalia nao wakiniangalia hao wanafunzi wa Chimbaunye. Nikawaona wakiwa wamezubaa wakinitazama kwa macho ya kusaminisha. Niliwaona wakitazama viatu vyangu, kisha wakapanda kwenye soksi, kumbe waliona na saa yangu ya mkononi, hapo nikaziona nyuso zao zikihamasika. Kila walichokiangalia nami nilikiangalia kutoka kwao. Aghalabu! Walipoangalia shati langu jeupe pee kama barafu nami nikaangalia mashati yao.
Yalikuwa mashati machafu jamani, sijawahi kuona, alafu hayakuwa na vishikizo, ni kwamba walikuwa kifua wazi licha ya baadhi ya sehemu ya shati zao kubanwa na pini. Basi nyuso zao zilifadhaika mno pale walipoona nimeona mambo hayo.
Vikamptura vyao navyo, Mmmh! kwenye Flaizi kulikuwa kumeachia. Niliona Chululu zao zikinitazama, kumbe hata nguo za ndani walishindwa kuvaa. Visichana navyo hali haukuwa mbali na wavulana. Usije ukafikiti sikuangalia viatu walivyokuwa wamevaa. Looh! Wapo waliokuwa wamevaa malapa, usifikiri ni malapa mapya. Yalikuwa malapa yaliyoshonwa kila mahala. Wapo waliokuwa wamevaa Yebo Yebo, nyingi zilikuwa zimeisha upande kama sio kutoboka katikati na chafu zilizofubaa. Wapo niliowaona wamevaa katambuga, hawa niliona kama wapo comfortable kiasi, walikuwa ni watu wa shari. Nilishtuka kuwaona waliokuwa pekupeku, walikuwa wamepauka jamani. Angalau wanafunzi wawili tuu ndio walikuwa wamevaa viatu. Mmoja alivaa Buti aina ya Bunango, na mwengine alipigilia Buti la Jeje jamii ya Lakuchumpa Lakumparama.
Walinizunguka kila mmoja akinitazama, kila mmoja alitamani niwe rafiki yake. Waliliona Begi langu la mgongoni la kisasa kabisa, huku wao wakiwa na mifuko ya nailoni hao waliheshimiwa sana, lakini wengi wao wakiwa wamebeba madaftari yao mikononi yakiwa yamechanika chanika bila ya kibebeo. Hawa walikuwa kundi kubwa.
Sikumbuki jinsi nilivyoona nywele zao, nashindwa kuelezea namna zilivyokuwa chafu, zikiwa rafu kama safu za vichaka vya porini. Walikuwa wamepauka, wachache sana walikuwa wamepaka mafuta ya kula, hali iliyowafanya wang'ae vipande vipande vya uso.
Pua zao zilikuwa zinamakamasi, huenda yalisababishwa na vumbi. Looh!
Basi tukaingia Darasani, ndilo hilo Darasa la Tano C. Darasa lile lilikuwa na madawati kumi na tano. Wakati sisi wanafunzi tulikuwa wanafunzi mia moja ishirini. Tuljaa mpaka tukafurika.
Hewa ilikuwa nzito kwa kanuni ya Density= Mass Over Volume. Harufu ilikuwa imetapakaa kwa Difuisheni na kuzijaza pua zetu kwa inhalation. Wengi walikuwa hawajaoga zaidi ya wiki mbili. Wasafi niliowashuhudia walikuwa wameoga siku saba zilizopita kwa makadirio. Hawakuwa wanapiga mswaki hivyo haikupendeza waongee ongee kwani midomo yao ilikuwa inanuka sana.
Mimi pekeangu ndio nilikuwa nanunikia, si nimetoka Mjini, nimetoka shule za kikurugenzi, shule za wajumbe.
Basi wattukutu wa Darasa walikuwa wakicheza chandimu ndani ya darasa kabla mwalimu hajaingia. Miwingine upande huu na mwingine huu. Walicheza humo huku mpira wakiugombania kila mmoja akitafuta kuwa Ronadinyo. Walivutana mashati kumbe ndio sababu ya vishikio kukatika. Nilipigwa mpira wa mgongo Puu! Hapo ukimya ukatokea, Darasa zima likinitazama na kuangalia mahali mpira uliponichafua.
Nilijisikia vibaya, punde mwalimu akaingia. Alikuwa Mwalimu aliyejulikana kama MUSAHARA MUDOGO.mwalimu wa Hisabati. Uso wake haukuwa mbali na wanafunzi aliokuwa anawafundisha, tofauti ilikuwa mwenye mavazi. Alivalia mavazi masafi lakini usafi ule haukufanya nishindwe kuona uchakavu wa mavazi yake. Kola ya shati alikokuwa amevaa ilikuwa imechanika chanika, Sharti lilikuwa limepauka, na hiyo niligundua nilipoangalia ndani ya mfuko wa shati uliokuwa upande wa mkono wake wa kushoto. Mkanda wake ulikuwa umetoboka toboka wenye nyuzi nyingi. Tayari alikuwa ametoboa matundu matatu kupunguza ukubwa wa kiuno. Ni kwamba alikuja akiwa kanenepa lakini sasa amekonda. Looh!
Sitaki kueleza habari ya suruali na viatu alivyokuwa amevaa, kwani nahisi naweza pata laana. Ninamheshimu sana Mwalimu MUSAHARA MUDOGO sijui kabila lake kweli. Alikuwa mcheshi sana lakini kilichomponza ni sura yake iliyokosa wajihi.
Muda wa kuimba tebo ulifika. Ilikuwa Tebo ya saba. Tulianza kuimba. Saba mara moja saba, hivyo hivyo. Ajabu ni kuwa waliokuwa wakiimba tebo hiyo walikuwa hawadiki ishirini kati ya watu mia moja ushee. Hao wengine waliunda sauti ya mvumo wa nyuki. Hehee hee! Hee heehee! Hee!
Hali hiyo hata kwenye wimbo wa taifa na nyimbo nyingine za shule watia beat walikuwa wakizua mvumo usio na sauti.
Hata hivi leo ukubwani, kundi lile lipo Makanisani, misikitini. Kanisani watu wakiambiwa waimbe wale watu tuliotokea Chimbaunye utatusikia tukizitia Beat kwenye nyimbo kanisani. Hatuimbi bali tunazua sauti;
Waimbaji: Nitembee Nawe e Mungu, Alivyotembea Enoko
Wanachimbaunye: mhuu! Mhu! ... mh! mmmh! mm!
Hata kwenye sala ya Bwana wapo wanachimbaunye.
Baadaye mapumziko nikatoa nikiwa nipo hoi, nimeshaenguliwa kwani nimeshachafuka kwa kushika shikwa na wanachimbaunye. Kwani Dawati moja tunakaa wanafunzi kumi, tumebanana kama ndizi kwenye mkungu. Nimeenguliwa kwani ninanuka jasho la wanachimbaunye.
Sasa kuulizia choo nikaambiwa nizunguke kwa nyuma huko. Kwenda Looh! Nililakiwa na kundi la nzi waliokuwa wamezingira magimba huku na huku. Ilikuwa ni Meza kuu ya nzi wa Chimbaunye. Looh! Hata pakukanyaga nikakosa.
Nikaenguliwa nisijisaidie. Kurudi Darasani Looh! Nilikuta nimeshaenguliwa kwenye begi langu. Nimeibiwa begi na daftari zangu. Hata Compass zangu nazo zilienguliwa, hakuna kilichosalimika. Looh!
Darasa la Tano C kutoka Chimbaunye, wazee wa Kuengua wenzenu Mungu anawaona.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300