Njooni tujifunze kwa bakhresa!
1.ANZA MAPEMA, Acha kukawia (Show up early)
Fanya kile unachodhani unaweza kufanya, fanya mapema iwezekanavyo, acha kukawia. Usisubiri hadi muda wa kila kitu kuwa sawa, huo muda hautatokea na utajikuta umechelewa. Salim said awadh bakhresa akiwa na umri wa miaka 14 aliacha shule baada ya kugundua kuwa haikuwa njia yake sahihi na kwenda kutafuta elimu ya fedha.
Baada ya kutaabika sana akiwa muuzaji wa viazi, mwishowe alianzisha mgahawa mdogo(small restaurant) hapo ilikuwa ni miaka ya 70's na ndio hatua yake kubwa kuelekea mafanikio yake. Mengine ni historia.
2.JIANDAE KUSONGA MBELE MUDA WOWOTE (Be prepared to move anytime)
Usisimame na jambo moja, usisimame na wazo moja, tembea na wakati, msome bakhresa alichofanya.
Miaka ya 1980's uzalishaji wa nafaka nchini Tanzania ulikuwa mkubwa sana, bakhresa akaanzisha machine ya kusindika nafaka, hii ilifanya malengo yake kuwa bora zaidi na kwa sasa Rwanda inategemea mashine za bakhresa kuwazalishia zaidi ya toni 120,000 kwa mwaka. Hata wewe unaweza kufanya vizuri zaidi ya bakhresa.
3.FIKIRI VEMA (Think big)
Kutoka kuwa muuzaji wa viazi hadi kuajiri watu zaidi ya 2000 inahitaji ndoto makini sana. Kama unafikiria kutengeneza pesa ili kuondokana na umaskini unaokukabili basi ndoto yako ni ndogo, fikiri kujenga ngome na himaya kubwa ya biashara kama Azam na utajikuta umaskini wako umepukutika na pia utajikuta unapukutisha hadi umaskini wa wengine katika jamii kwa njia ya ajira.
4.KUWA SAMAKI MKUBWA KWENYE DIMBWI KUBWA (Be a big fish in a big pond)
Tazama, bakhresa amewekeza Afrika mashariki na kati lakini bado hajakunja mikono yake na kuweka mfukoni. Ana mashine kubwa ya ngano nchini Uganda, nafaka nchini Msumbiji na Malawi, kampuni ya usafirishaji nchini Tanzania, kampuni ya bidhaa za vyakula nchini Tanzania, Utalii baharini nchini Tanzania; bila shaka bakhresa anakupa changamoto katika hili.
5.THAMINI WATENDAJI/WAFANYAKAZI WAKO (Value your workforce)
Kuna makampuni mengi zinawatendea ndivyo sivyo wafanyakazi wake, ila kwa bakhresa hali ni tofauti kidogo yeye anajua muda gani atakuwa mkali na muda gani atakuwa mpole kwa wafanyakazi wake. Anatumia zaidi ya dola 3400 kwa mwezi kwa ajili ya matibabu ya malaria kwa wafanyakazi wake; hata hivyo katika maeneo ya biashara zake kuna misikiti kwa ajili ya kuwafanya wafanyakazi wake wawe karibu na Mungu.
6.NGUVU YA WANAFAMILIA (The power of family members)
Ingawa kuna wataalam nyuma ya mafanikio yake, bakhresa ndie bingwa nyuma ya hizo fikra za wataalam. Tazama, Mohamed Said Bakhresa ndie Mkurugenzi Mtendaji wa mashine/kiwanda cha nafaka huko Uganda, Omar Said Bakhresa ndie Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya usafirishaji hapa Tanzania, Yusuf Said Bakhresa ndie Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni za vyakula hapa Tanzania.
Kila la kheri!
TheDealer!