Darasa lolote huwa halikosi watu kama hawa✔

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
7,147
Reaction score
14,699
Darasa lolote (hasa vyuoni) lazima liwe na wanafunzi wafuatao:


1. Mrembo wa darasa.


2. Playboy/playgirl - Hawezi kutembea na msichana/mvulana mmoja mara mbili.


3. Group ya marafiki watatu. Kila mara wako pamoja.


4. Mtu mwenye maswali ya kuudhi/kukera.


5. Msongolist kimeo - Huyu huwa anasoma sana but hana bahati ya kufanya vizuri. Yani msuli tembo lakini matokeo sisimizi.

6. Mlafi - Huyu huwa hakatai offer.


7. Mtoro wa kudumu - Haji darasani hata kama hana sababu.


8. Mchelewaji wa kudumu - Anakuja kipindi kiko katikati au kinakaribia kuisha.


9. Miss/Mr. Misifa - kila mara ataeleza jinsi nyumbani kwao walivyo matajiri.


10. Less talkative - lakini kiwembe. Jamaa mkimya lakini unakuta ametembea na karibu wasichana 15 hapo class.


11. Handsome boy - Huyu hana mpango na wanawake.


12. Chips addicted - Hawa wanaweza kula chips asubuhi mchana na jioni. Jumatatu hadi Jumatatu.


13. Back benchers - Hawa huwa watundu sana na ni watu wa jokes. Huwa hawajibu swali, laini wanasubiri wakati wa kushangilia waongeze bezi.


14. Wambea - Hawapitwi na kitu darasani na washazoea kufeli.


15. Mchungaji/Mtumishi wa Mungu,


16. Waimbaji/Wasanii


17.Walevi


18. Mabishoo.


19. Team popo - Hawa wawe na hela wasiwe na hela wanakesha club


20. Mwenye aibu kusimama mbele za watu. Wakati wa Presentation anakimbilia kusimama nyuma ya wenzie


21. Viherehere - Hawa mara nyingi hutokea kupendwa sana na waalimu.


22. Wanaosoma ili kushindana kwenye GPA.


23. Kupe - Huyu ‘boom’ likitoka atawaganda wenzie hadi ziishe, halafu yeye anaanza kula zake alone.


24. Wise man/woman - Huyu huwa ni mtu anayeaminika na kila mtu darasani. Hutumika sana kushauri pale mambo yanapoenda mrama. Mara nyingi huwa ni mtu mzima.


25. Mpenda supu – Yeye hata ya nyani atakunywa tu.


26. Fix man - Huyu atakuomba jero, akafuatilie dili la milioni kumi town, kumbe hana hela ya chai.


27. Photocopy machine - Huyu ukimuonesha majibu kwenye mtihani anaweza kucopy hadi jina lako.


Usiposema wewe uko namba ngapi mwingine atakusema… 😀 🙂 😀 🙂 😀 🙂
 
Kumbeee!!!!
Tusiosoma hatuyajui hayo na memkwa haipo tena aaahhh
 
27 inanihusu msemakweli mpenzi wa mungu
 
Hahaha umenikumbusha Darasa la 7B...wazee wa back benchers
 
Umenikumbusha hyo no 21. Afu wabovu kinoma class
 
Namba 11 inanihusu
 
Dah no. 8 ilinipa shida Makongo high school 2010-2012 nimeruka kichura chura, push up zakutoshaaa kisa uchelewaji tena wakudumu...
 
kuna baadhi yao shule za vijijini hamnaga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…