Darasa Zima Wapata Mimba Waacha Shule Kenya, Abaki Mmoja tu

Darasa Zima Wapata Mimba Waacha Shule Kenya, Abaki Mmoja tu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
2995150.jpg


Friday, September 04, 2009

Ni mwanafunzi mmoja tu wa kike katika shule moja ya sekondari nchini Kenya amebaki darasani baada ya wanafunzi wenzake wote 24 wasichana kuacha shule baada ya kupata mimba. Mwanafunzi mmoja wa kike katika shule ya sekondari ya Marinyn Secondary School iliyopo katika mji wa Kericho nchini Kenya, amelazimika kujisomea mwenyewe baada ya wanafunzi wenzake wote 24 wa kike kuacha shule kwasababu ya ujauzito.

"Hali inasikitisha sana " alisema Samuel Njora mkuu wa wilaya ya Kericho.

"Katika wasichana 25 walioanza form one mwaka huu, wasichana 24 wameacha shule baada ya kupata mimba".

"Hivi sasa wamebakia jumla ya wasichana 20 tu shule nzima na wasichana wengi wa madarasa ya juu wameacha shule baada ya kupewa mimba na wafanyakazi wa mashamba ya chai", alisema mkuu huyo.

Maafisa wa serikali wanalaumu umbali wanaotembea wanafunzi hao kwenda shuleni wakikatiza mashamba ya chai ya James Finlay kuwa ndio chanzo cha wasichana hao kupewa mimba na wafanyakazi wa mashamba hayo.

Njora alisema kuwa shule hiyo ya sekondari inabidi iwapatie usafiri wanafunzi wake wa kike kutoka majumbani mwao na kuwarudisha majumbani mwao ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanaopata mimba.

Alisema kuwa wasichana wa form one wanakabiliwa na hatari ya kupata mimba kutokana na kuhadaiwa na wavulana na wafanyakazi katika mashamba ya chai wakati wa safari yao ya kuelekea shule.

Gazeti la The Standard la Kenya lilisema kuwa elimu kwa wasichana ni kama ndoto ya kutisha nchini humo.

Wasichana wengi hulaghaiwa na kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi yanayopelekea wapate mimba zisizotarajiwa.

Matokeo yake wasichana hao huacha shule na kuanza maisha ya kama wazazi.


Chanzo: nifahamishe.com
 
Hii tena kali naona kama sababu ya msingi haijawekwa kutembea kwenye mashamba ya chai ndo iwe sababu tosha ya wao kupata mimba?
Mi naona hapa huenda sababu za kiuchumi ndo zinasababishwa hawa mabinti kupata hizi mimba ambazo ndani yake huenda siziwe mimba tu maana hawajapimwa afya zao.
Wawe wanatembea na ile mipira kama au wagawiwe na shule inaweza ikawasaidia hao waliobaki.
 
Ni kubwa kuliko.
-Umbali kutoka nyumbani
-Kupita katikati ya msitu
-Wakati ukipita watu unaokutana nao ni wanaume tu
-Umasikini; kiasi unakwenda shule ukiwwa na njaa
-Ujinga unaowasumbua teenagers wakidhani huo ndio wakati wao wa kuyafurahia maisha
-Mwisho ni UFATAKI tu wa NYAMAUME.
Ila kwa kweli hii ni hatari kuliko hatari yenyewe.
 
Kwa spidi hii UKIMWI utakwisha kweli?
 
Tusiangalie mimba tu, je wamepimwa kujua kamba wapo salama? Hao waliojamiiana nao salama kweli? huenda hao wanaume wameshakata tamaa ya kuishi hivyo wanasambaza virusi kwa watoto.

Nawaombea salama tu.
 
Back
Top Bottom