Darassa: Nyimbo zangu za ujumbe zilibuma

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Darassa amedai mwanzo alikuwa akitoa nyimbo zenye ujumbe lakini zilikuwa zikionekana za kawaida.



Muimbaji huyo ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye nyimbo za ujumbe ndio akaangalia ni kitu gani mashabiki wanataka akaamua kubadilika.

“Mwanzo nilikuwa nikitoa nyimbo zenye vionjo vyenye ujumbe wa kutosha lakini hazikuwa zikipokelewa sana ila nilipokaa na kufikiria zaidi, nikatambua nini mashabiki wanataka na ndiyo maana muziki wangu upo juu sana tofauti na zamani,” amesema.

Rapper huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa ‘Muziki’ uliogeuka kama wimbo wa taifa kwa sasa.
 
Hebu wekeni hiyo nyimbo hapa maana nimeishia tuu kuisoma huku kama nnavyoisoma namba kule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…