Darfur na utekwaji nyara

gmwansasu

Member
Joined
Apr 23, 2008
Posts
43
Reaction score
5
wasalaam

Napenda kuwatoa hofu ndugu watanzania popote mlipo, hasa wale wanaofuatilia habari za Darfur kwa karibu. Kama mnakumbuka siku mbili zilizopita TBC walitangaza kuwa kuna utekaji nyara wa walinda amani wawili wa umoja wa mataifa, na kwamba mmojawapo ni mtanzania.

Napenda kuwahakikishia watanzania wote kuwa hakuna mtanzania yoyote anayehusika, bali waliotekwa nyara ni Mnaijeria na Mzimbabwe.

Tuwaombee wote wanaojitolea maisha yao kulinda amani katika dunia hii tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…