Dark days 17/03/20...



[emoji28][emoji28]
Kwingine huwa tuko pamoja ila kwa hapa, nakataa.

Mambo mawili
1. Mliokuwa wafuasi wa JPM. Niondoe humu kabsaaa sina ufuasi wa aina yoyote na siasa na wanasiasa wa Tz, ila naumizwa na uonevu wa aina yoyote ile.

2. Hawezi kuuwawa, kwa mtu kama JPM aliyekuwa anajihami kiasi kile. Kujihami sio kushinda ufedhuli wa wanadamu. Kikulacho ki nguoni mwako, hapo hapo unapojihami ndipo unachapika.

Maraisi wangapi wameuwawa tena wakiwa madarakani? Je walikuwa hawajihami? Hawakuwa na ulinzi mkali.

In every strength their is/are weakness(es).
 

Samahani mkuu.

Umesema hautaki kwende deep kuhusu ishu ya gas.

Please can you code your story kwa namna ambayo tunaweza kupata chochote…?!

Nimekuwa interested sana.
 
Hawezi kuuwawa, kwa mtu kama JPM aliyekuwa anajihami kiasi kile. Kujihami sio kushinda ufedhuli wa wanadamu. Kikulacho ki nguoni mwako, hapo hapo unapojihami ndipo unachapika
Wewe umesema kikulacho ki nguoni mwako.... Ila watu wanadai ni Old CEO plus wapinzani na mabeberu. Hivi kweli ukiwa nje ya system unaweza muua Rais? Hizo nchi ulizotaja wengi wa Marais waliuwawa kwa inside job ila huwezi mtu kama Mbowe au JK akumaliza wakati hata hajui presidential protocol iliyopo zamu.
Mliokuwa wafuasi wa JPM. Niondoe humu kabsaaa sina ufuasi wa aina yoyote na siasa na wanasiasa wa Tz, ila naumizwa na uonevu wa aina yoyote ile.
Kumradhi mkuu
 
Lakini alikudanganya kwamba hasafiri Ili kubana matumizi na ulisifu na kuabudu heti ni uzalendo
 
Mkuu kama hujazima kidude cha data basi utakuwa umeishiwa bado, nchi yetu pamoja na vyanzo vyake umeme ambao ni affordable ni wa maji, na hyo unayosema 60% ni gesi but ipo kwenye karatasi tu na ukiiweka kwenye uhalisia itageuka kuwa ya ghali zaidi,

Tuwe wa kweli linapokuja swala la maisha ya watu, nchi hii kuna mtu alitufundisha kuwa inawezekana ila kunawatu wanachepusha ukweli kwa kutuambia kuwa haiwezekani,

Kwa nn in 6yrs hatukuwa na hizi ngonjera? Au zimetoka wapi ghafula? The man alikuwa na mapungufu yake bt likija swala la how to take action , the man was fit, ukweli ubaki mengine yanaweza kuendelea

Hakuna muwa mtamu usiokuwa na pingili
 
Kinachofurahisha zaidi ni yale aliyoyasema yanakwamisha alipo yaondoa ndiyo hayo yakawezekana, sasa yanarudiahwa ndiyo matokeo yanakuwa kama alivyotuambia, cha kujiuliza nani mwongo kati yake na hawa ambao wanafanya yale aliyoyakataa kishawanashindwa kutupa yale aliyotupa sisi wakati huo?
 
Ila OLD CEO mambo yake aliyoasisi pale nishati na madili yanaendelea kulindwa hebu piga hesabu umeshauza gesi kwa kampuni ambayo wewe umejikabidhi kama mteja mkuu.Anakuja mtu anakuambia nahamisha nawekeza kwenye umeme wa maji ni ni nafuu,huku wewe ulisha plan gesi ifike bagamoyo pasipo na chochote.ila ahadi ya bandari.
Halafu pale IPTL palipozimwa na maisha yakaendelea wanalipwa Bil Kadhaa za madai yao.
Kaingia mtu mwengine anadai tubadilishe nyaya kwa tril kadhaa kana kwamba nchi ndio inaanza kujengwa.
 
Mkuu sijui kama mr culture alivyokuwa anamzungumzia old ceo, alisema mwenyewe kwamba old ceo alikuwa na uthubutu wa kufanya maamzi kwenye kampuni, na hapo ndipo ukweli ulipo...
 
He was murdered. Hakuna Siri tena. Ushahidi wa Mazingira unaonyesha. Kuna wanafamilia walitaka kukanusha kwamba mzee hakuwa na Tatizo la Moyo washauri wakapiga stop kwa Usalama wao. Magu alikuwa na Afya imara Sana hata wewe unajua
 
He was murdered. Hakuna Siri tena. Ushahidi wa Mazingira unaonyesha. Kuna wanafamilia walitaka kukanusha kwamba mzee hakuwa na Tatizo la Moyo washauri wakapiga stop kwa Usalama wao. Magu alikuwa na Afya imara Sana hata wewe unajua
Si kweli, alikuwa mgonjwa. Hata kwenye kampeni si uliona vile vifaa vya kumsaidia kuhutubia kwa muda mrefu? Pia siyo mara moja taarifa zilisikika kuwa hawezi kukaa kwenye ndege kwa muda mrefu kutokana na tatizo la moyo.
 
Kuna wanafamilia walitaka kukanusha kwamba mzee hakuwa na Tatizo la Moyo washauri wakapiga stop kwa Usalama wao
Sure? Wanafamilia Gani hao mkuu maana msemaji anadai alikuwepo siku JPM anafariki na hakukanusha kuwa haumwi.

Magu alikuwa na Afya imara Sana hata wewe unajua
Sidhani, kampeni mbona alishindwa kufanya kama alikua na afya njema?


He was murdered. Hakuna Siri tena.
Interesting, unaweza tusaidia aliuwawa vp?
 
.Anakuja mtu anakuambia nahamisha nawekeza kwenye umeme wa maji ni ni nafuu,huku wewe ulisha plan gesi ifike bagamoyo pasipo na chochote.ila
If that's the case, why wouldn't the old CEO abandon the Nyerere Dam now that the late CEO is gone? It really doesn't add up if at all, that was a sole reason to assassinate the deceased CEO.
 
Tuwe wa kweli linapokuja swala la maisha ya watu, nchi hii kuna mtu alitufundisha kuwa inawezekana ila kunawatu wanachepusha ukweli kwa kutuambia kuwa haiwezekani
Mfano kipi kiliwezekana? Mbona alikua anakopa kwa mabeberu pia.
nchi yetu pamoja na vyanzo vyake umeme ambao ni affordable ni wa maji, na hyo unayosema 60% ni gesi but ipo kwenye karatasi
Hapa hatuongelei affordability tunaongelea capacity. Huyo anadai mabwawa yanahujumiwa watu wauze majenereta. Ndio nikamuuliza kwanini wahujumu mabwawa yanayozalisha only 30% ya umeme wa Tanzania alafu wasihujimu Bomba la gesi linalozalisha zaidi ya 60% ya umeme?

Kwa nn in 6yrs hatukuwa na hizi ngonjera? Au zimetoka wapi ghafula?
Ngonjera zipi Mkuu? Mbona NIDA ilimshinda mpaka anaondoka anafariki hatukupata vitambulisho. Mbona suala la wamachinga lilimshinda same to Bandari. Bado sijaongelea korosho Hadi akaogopa kufanya kampeni kabisa huko kusini.

Nadhani anakuzwa sana na media ila failures ni nyingi mnoo
 
Hakuna kitu kama hicho, hayo mambo ya kujiongezea muda yalipigiwa chapuo na watu waliokuwa na agenda ya kumchafua ili aonekane alikuwa na tamaa ya madaraka lakini naamini asingeongeza hata sekunde moja ya utawala.
We jamaa mwongo sana. Yule mzee alikuwa na tamaa ya madaraka kuliko fisi akiona mzoga.

Tumwombee Mungu amrehemu madhambi yake lakini kwenye hili hana utetezi wowote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…