Emanueli misalaba
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 1,769
- 2,523
Mkuu, Nguruvi3 , tayari tumepewa ruhusa ya kuendelea kujadili masuala haya Muungano na mengine muhimu kwa nchi yetu.[emoji736]
Kabla ya kuungana mwaka 1964 Tanganyika ilikuwa na mipaka yake.Gharama za kuihudumia Zanzibar na gharama za kulinda mipaka ya baharini ipi gharama kubwa??
Tanganyika ina mipaka yake ya baharini hata kabla ya kuungana na Zanzibar, je gharama za kulinda mipaka ya bahari ya Tanganyika nje ya Muungano na gharama za kuhudumia Muungano ipi gharama zaidi?Kabla ya kuungana mwaka 1964 Tanganyika ilikuwa na mipaka yake.
Sijaona hoja hapa labda unifafanulie zaidi tafadhali
Hakuna gharama itakayoongezeka au kupungua. Mpaka kabla ya Muungano ulianza Tanga hadi Mtwara ukiwa na visiwa vya Mafya na bahari kuu. Baada ya Muungano ukashirikisha visiwa vya Zanzibar mbele.Tanganyika ina mipaka yake ya baharini hata kabla ya kuungana na Zanzibar, je gharama za kulinda mipaka ya bahari ya Tanganyika nje ya Muungano na gharama za kuhudumia Muungano ipi gharama zaidi?
Sawa kiongozi shukurani, maana niliwahi kumsikia Zitto akisema "kuwa kwenye muungano ni nafuu kuliko kuwa nje ya muungano, gharama za kulinda mipaka ni kubwa"Hakuna gharama itakayoongezeka au kupungua. Mpaka kabla ya Muungano ulianza Tanga hadi Mtwara ukiwa na visiwa vya Mafya na bahari kuu. Baada ya Muungano ukashirikisha visiwa vya Zanzibar mbele.
Vifaa na askari wanaotumika sasa hivi watapunguza wigo lakini si kifaa au rasilimali watu.
mkuu nadhani hoja hapa si ghalama au nani ananufaika au anapoteza hzo ni hoja za nje tu kiini chenyewe kabisa kabisa Cha Zanzibar kuwa sehem ya Tanganyika ni USALAMA,Kwa vyovyote vile Zanzibar inabidi iwe na mikoa maalumu ndani ya Tanzania ili kuwavunja nguvu kabisa ya ubinafsi kuwe na mikoa miwili ya Zanzibar na Pemba kabisa ili kuondoa hii hali ya Serikali mbili ndani ya Nchi Moja, kipimo cha Rais bora ni yule atakayeweza kufanya Nchi kuwa Moja yaani serikali Moja kamili bila fikra za uzanzibari tena maana utanganyika ulishakufa Sasa kazi ya kiongozi hodari ni kuua uzanzibari, bila kuua uzanzibari hakuna Utanzania, hivyo kwa maoni yangu, Uzanzibari ni adui mkuu wa taifa la Tanzania kwa sababu umebeba ubinafsi, uchoyo, dharau, kiburi, majivuno na nyodo dhidi ya watanganyika, Sasa Zanzibar lazima waamue either serikali Moja au waende kivyao.
NB: Anayepoteza nafsi yake kwa ajili ya Mungu (Umoja) ataiokoa (Tanganyika), Anayeiokoa nafsi yake kwa ajili ya ubinafsi wake ( Utengano) ataipoteza (Zanzibar).
Ni maneno tu ya watu katika kubabaisha Umma. Hata sasa hivi tuna vitu hivyo kwasababu bahari ipo na wala haihami asilani. Kitakachotokea ni kwamba Tanganyika italinda mipaka yake kama ilivyo sasa kuanzia kaskazini hadi kusini na bahari kuu na visiwa vyake. Zanzibar ambayo haina gharama za Ulinzi ndio itabidi iwe na vitu hivyo, hapo ndipo watu wanaficha ukweli. Kwamba, Tanganyika haina gharama hata senti tano wala haitapunguza gharama nukta.Sawa kiongozi shukurani, maana niliwahi kumsikia Zitto akisema "kuwa kwenye muungano ni nafuu kuliko kuwa nje ya muungano, gharama za kulinda mipaka ni kubwa"
Kwamba itabidi uwe na Submarine, nyaya za baharini na nyenzo nyinginezo
Sawa mkuu shukurani sana.Ni maneno tu ya watu katika kubabaisha Umma. Hata sasa hivi tuna vitu hivyo kwasababu bahari ipo na wala haihami asilani. Kitakachotokea ni kwamba Tanganyika italinda mipaka yake kama ilivyo sasa kuanzia kaskazini hadi kusini na bahari kuu na visiwa vyake. Zanzibar ambayo haina gharama za Ulinzi ndio itabidi iwe na vitu hivyo, hapo ndipo watu wanaficha ukweli. Kwamba, Tanganyika haina gharama hata senti tano wala haitapunguza gharama nukta.
Zanzibar itakuwa na mipaka , jeshi na vifaa jambo ambalo sasa hawana ndio maana wanaweza kulipa Wazee pensheni hata kama hawakuwahi kufanya kazi.
Kwa wakati huo lakini si usalama wa Tanganyika tu bali pia usalama wa Zanzibar kama tutakavyoona baadayemkuu nadhani hoja hapa si ghalama au nani ananufaika au anapoteza hzo ni hoja za nje tu kiini chenyewe kabisa kabisa Cha Zanzibar kuwa sehem ya Tanganyika ni USALAMA,
Si kweli kwasababu adui huyo angetumia Rwanda, Burundi , Malawai n.k. Kumbuka Tanganyika ina mipaka na nchi 8maana adui atatumia Rafiki alie karibu nawe kukupiga, tizama vizri kijoografia angalia, mafia, Pemba na unguja nenda mpka juu Pale ramu kama sikosei hivi ni visiwa Vya kimkakati, kwa hyo mwl alipotengeneza hesabu akaona kabisa ili niitawale nchi vzr visiwa vyote hvi viwe chini yake
Hapana! unakosa point, ni kinyume chake. Kwamba Karume alikuwa under pressure ya Umma Party ya Abraham Babu. Kuna wakati Tanganyika ilibidi ipeleke askari 300 na Karume alipoleta jeuri Nyerere akatishia kuondoa majeshi.mwalim alikuwa very interrigent akamsoma vzr karume akaenda na proposal yake akatengeneza ndoa Tena isiyovunjika na mwisho mkataba ukawa Siri Tena uko UN
Kwanini Serikali 3 haiwezekani? Hapa ndipo tunahitaji utusaidie. Kwanini Muundo wa sasa unaosema ni suluhisho bado una matatizo tunayoyaon!mambo ni mengi ila tu serikal 3 haziwezekani Wala 1 ila huu muundo wa sasa ndyo suluhisho, tumetaka au hatujataka.
Si kweli kwasababu adui huyo angetumia Rwanda, Burundi , Malawai n.k. Kumbuka Tanganyika ina mipaka na nchi 8
Smartkahn kuhusu Rwanda kama kuna ukweli fulani, namna ambavyo anaipelekesha Congo hadi unashangaa kabisa.Mkuu kijiografia zanzibar imekaa vibaya zaidi ukilinganisha na majirani wengine. Naona huu muungano waliangalia sababu kadhaa ila shabaha kubwa ilikua ni usalama.
Kuhusu Rwanda mimi nadhani ni suala la muda tu, inawezekana maadui kwa wakati huu hawajaona potential yoyote kwetu, kuna nyakati kama tutapishana saana ideology na ki-maslahi na wakubwa wetu, kunauwezekano zengwe likatokea.
Rwanda mimi hua nahisi ni monitor wa wakubwa kwa ukanda wetu huu wa A. Mashariki na kati, kama ambavyo hua nahisi Israel na Middle East pale.
Ukizingatia hiyo hoja ya zitto ni nzito imejikita kwenye athari zitakazojitokeza baada yakuwa nje ya muungano,,Sawa kiongozi shukurani, maana niliwahi kumsikia Zitto akisema "kuwa kwenye muungano ni nafuu kuliko kuwa nje ya muungano, gharama za kulinda mipaka ni kubwa"
Kwamba itabidi uwe na Submarine, nyaya za baharini na nyenzo nyinginezo
Tuna mpaka mrefu sana na Kenya katika nchi tunazopakana. Tuna mpaka na Msumbiji, Congo, na nchi nyingineMkuu kijiografia zanzibar imekaa vibaya zaidi ukilinganisha na majirani wengine. Naona huu muungano waliangalia sababu kadhaa ila shabaha kubwa ilikua ni usalama.
Tulioishi wakati wa ' frontline states' na mapigano ya kudai Uhuru kwa nchi za kusini mwa Africa hatuoni tishio lolote la nchi jirani. Hata hivyo nakubaliana nawe kwamba 'Intelligence' tuliokuwa nayo si hii ya sasa hivyo kuwa vulnerable na nchi yoyote ni kitu possible. Hapa si suala la mipaka ni suala la 'Intelligence'Kuhusu Rwanda mimi nadhani ni suala la muda tu, inawezekana maadui kwa wakati huu hawajaona potential yoyote kwetu, kuna nyakati kama tutapishana saana ideology na ki-maslahi na wakubwa wetu, kunauwezekano zengwe likatokea.
You never know! Mbona kuna Marine base kubwa sana pale Lamu Kenya? Kwanini usiwe suspiciousRwanda mimi hua nahisi ni monitor wa wakubwa kwa ukanda wetu huu wa A. Mashariki na kati, kama ambavyo hua nahisi Israel na Middle East pale.
Mbona hamuelezi athari hizo? Tusaidieni sisi tuisoona uzito wa hoja.Ukizingatia hiyo hoja ya zitto ni nzito imejikita kwenye athari zitakazojitokeza baada yakuwa nje ya muungano,,
Kwa nini isiwe serikali moja?.Mbona hamuelezi athari hizo? Tusaidieni sisi tuisoona uzito wa hoja.
Tunatishana tishana tu bila hoja, tafadhalini njooni tuzungumze
1. Muundo wa Serikali ya sasa ni 'mzuri'. Tuelezeni malalamiko yanatoka wapi ikiwa ni mzuri?
2. Serikali 3 zina gharama, tuonyesheni wapi gharama zinaongezeka , kwa eneo gani na watu gani!
3. Kuna suala la Usalama, tuelezeni kwa lipi na kwanini isiwe nchi 8 tulizo na mpaka nazo bila bahari
Daaah! Umesoma maandiko yote Nguruvi aliyo andika juu?Kwa nini isiwe serikali moja?.
Kero zitakuwepo tu hata pawe na serikali saba
Taifa la Afrika limegawanywa vipande vipande huku kila kipande kikiwa na serikali yake iliyo tofauti na kipande kingine.
Ikiwa ni moja wote tukaongea lugha moja, tukaelewana ule umoja ambao ndio nguvu ya kushinda ujinga, magonjwa na umasikini utaleta matokeo.
AFRIKA UNITE (You Night)
Ndio MkuuDaaah! Umesoma maandiko yote Nguruvi aliyo andika juu?