Dark days 17/03/20...

Rabbon, Rabonn ,rabon, yupi kati ya hao ulimaanisha.
 

Yaani hii ningeweza kusema ni 97% ya kile nachoamini siku zote. Tungepishana approach tu tena kwa kiasi kidogo.

Hii nchi tunaujinga mwingi sana kwenye mambo mengi. Siku zote ni kuwa na watu wenye kufanya maamuzi potelea mbali yanamuumiza nani lakini ramani inajulikana tunaenda kufikia wapi.
 
ulisha wahi kusikia mtanganyika anajitambulisha kuwa ni mtanganyika? unajua ni kwa nin?
Jibu ni kwamba Mtanganyika alikubali Utanzania. Fahamu kwamba Utanzania unahusu Uzanzibar pia, ndiyo maana Wazanzibar wakitaka kutumia fursa za Tanganyika wanajiita Watanzania. Tunaambiwa Waziri Mbarawa ambaye ni Mzanzibar anafanya kazi ya Uwaziri katika Wizara isiyo ya Muungano kwasababu ni Mtanzania.

Jina si tatizo, tunaweza kuita Tanganyika kama ilivyokuwa kabla ya 1964 au Tanzania Bara. Kitu cha Muhimu ni kwamba hiyo Tanganyika au Tanzania Bara inatakiwa iwe na serikali yake kama ilivyo Zanzibar ndani ya Muungano. J
Uwepo wa Serikali ya Tanganyika utasaidia mambo haya
1. Kuondoa dhana kwamba Tanganyika inaionyonya Zanzibar kwa koti la Muungano!!!
2. Kuipunguzia Tanganyika mzigo wa kujiendesha, kuendesha Muungano na Zanzibar kwa ujumla
3. Kuweka wazi Mchango wa Zanzibar haina katika Muungano
4. Kusaidia Tanganyika kutetea na kulinda masilahi yake kama ilivyo Zanzibar
5. Kuhakikisha Zanzibar inawajibika katika Muungano si kufaidika tu na Muungano
mkuu muundo wa sasa wa serikali ndyo Bora x1000 kuliko muundo mwingine wowote utakao pendekezwa, kama huu haukubariki maana yake Muungano ufe! na ukifa atakae athirika zaidi ni Zanzibar kwa kuwa atalazimika kuwa mkimbinzi kwenye ardhi yake mwenyewe..
Ikiwa muundo wa sasa ni mzuri , malalamiko yanatoka wapi? Wazanzibar wasiobeba gharama zozote wanalalamika. Watanganyika wamechoshwa kubeba Mzigo wao na wa Zanzibar.
Hebu tueleze uzuri wa huu muundo ni upi?
nlisema hapo juu narudia tena hii ndyo ndoa(muungano) pekee duniani ambayo watu wanakuja kujifunza kwetu, kwamba nchi inakuwa na Marais wawili lkn mkuu wa majeshi1,
Hakuna anayekuja kujifunza huu ujinga. Tutajie nchi moja tu iliyokuja kujifunza hapa na kama ipo pengine wanajifunza kwamba Muungano wa aina hii una watu wenye akili za kiwango gani!
Si kweli, Mkuu wa Majeshi si Amri Jeshi Mkuu. Kwa nchi moja kuwa na ''Amir Jeshi'' wawili bila kujua ni yupi mkubwa na kwa wakati gani, inashangaza.

January 12 utaona ''Amir Jeshi Mkuu wa Zanzibar'' akipokea heshima za Jeshi ambalo Amir Jeshi mkuu yupo nyuma yake. Kwamba nchi moja ina Amir jeshi mkuu wawili? au Amir jeshi na Naibu? ! sijui kwakweli .
 
Mwaka huu kimetokea kituko kingine cha Muungano

Waziri wa Madini wa JMT ametiiliana saini mktaba (MoU) na Waziri wa Madini wa Zanzibar.

1Katika nchi moja, MoU inakuwaje na kwa sababu gani? Hivi ''Tanzania'' inaweza kuwa na MoU na Mtwara?

Huyu Waziri wa Madini wa JMT ni wa nchi gani? Anawakailisha serikali ya Rais yupi na wa nchi gani?
Hii Tanzania ni nchi gani tofauti na ile iliyoundwa na Tangayika na Zanzibar?

Kilichotokea, suala la madini si la Muungano. Ili Zanzibar waweze kufaidika nalo lazima washirikishwe kupitia makubaliano (MoU). Tanganyika haina sababu za MoU na Zanzibar kuhusu Madini!

Jambo la kujiuliza, kwanini Wazanzibar waliokimbiza ''gesi na mafuta' leo wanataka MoU ya madini ?

Tangu Muungano uasisiwe hatujawahi kusikia Serikali ya Tanzania ikisaini MoU, kwanini ni kipindi hiki cha SSH?

Utaratbu wa MoU unatoka wapi kikatiba , na kwamba Rais wa JMT ambaye ni mkuu wa nchi ya Tanzania kupitia Waziri wa Madini wa JMT anasaini MoU na Waziri wa Madini wa Zanzibar! Hii ni nchi moja au mbili?

Ni suala gani jingine lenye MoU kati ya ''Tanzania na Zanzibar''?
 
Duh!!!..
 
Vipi kwenye kulipa..? Au analipa aliyekopa sio aliyetumia..?
Kuna mikopo ya Zanzibar, Zanzibar wanakopa wenyewe kwa udhamini wa JMT, ni Zanzibar wenyewe watalipa mikopo hii, ila ikitokea mkopaji akashindwa kulipa, hapa ndipo mdhamini anamlipia.

Lakini ile mikopo ya JMT inayokopa na Zanzibar kupewa asilimia 4.5%, mikopo hii inalipiwa na mkopaji JMT only, kwasababu hiyo asilimia 4.5% anayoopewa Zanzibar, hapewi kama mkopo, anapewa kama her rightful portion na hawajibiki kulipa chochote.
P
 

Mkuu sisi hata tukisema ni maigizo bado hayakidhi sifa za maigizo wala mazingaombwe.

Unashindwa hata kuelewa, hata waandishi wetu nao hawahoji maswali ili kuwagutusha hao watu.

Tunaenda ilimradi jambo limefanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…