Dark days 17/03/20...

Kuna mikopo ya Zanzibar, Zanzibar wanakopa wenyewe kwa udhamini wa JMT, ni Zanzibar wenyewe watalipa mikopo hii, ila ikitokea mkopaji akashindwa kulipa, hapa ndipo mdhamini anamlipia.
Hapa kuna tatizo kwasababu wakienda katika 'default' wanaolipa ni Watanganyika. Ndivyo ilivyotokea kwa Tanesco pia kwamba hawakutaka kulipa. JPM alisema walipe na akawapa nafauu ya kulipa. SSH kafuta deni lote
Maana yake anayelipa ni Mtanganyika kwa ongezeko la bei Tanesco.

JK aliwaruhusu wakakope wenyewe na wala hakuna shida. Kitu gani kinawalazimisha watumie JMT kama mdhamini wakati walikataa jambo hilo?
Lakini ile mikopo ya JMT inayokopa na Zanzibar kupewa asilimia 4.5%, mikopo hii inalipiwa na mkopaji JMT only, kwasababu hiyo asilimia 4.5% anayoopewa Zanzibar, hapewi kama mkopo, anapewa kama her rightful portion na hawajibiki kulipa chochote.
P
Jamani hii 4.5% ni ya GDP tu, kwa mikopo ni zaidi. Kuna mkopo wa WB ulitolewa takribani bilioni 500, Zanzbar walipewa Bilioni 100. Hesababu hazisemi hivyo ni 4.5.

Hakuna formula ya wazi na kama ipo iwekwe hapa. Lakini pia watu wajiulize, ikiwa kuna Formula ya ajira, Formula ya misaada, Formula ya Mikopo! Iko wapi Formula ya kuchangia Muungano?

Swali la kuchangia ni muhimu kwasababu kama Zanzibar inapata sehemu yake, kwanini sehemu ya Tanganyika itumike kuhudumia Muungano?
 
Linapokuja suala la nguvu aliyopewa Rais wa JMT na katiba yetu, halafu Zanzibar ina Rais wake na inalinda maslahi yake, wakati Tanzania Bara haina Rais isipokuwa Raisi wa JMT ambaye anaweza kutokea Zanzibar na katiba inampa nguvu ya kufanya atakavyo na katiba haimuwajibishi. Inashangaza sana jinsi watu wanavyojifanya vipofu, pia kuna uwezekano upande wa Bara watu hawana uchungu na Nchi yao.
 
Kuna hoja za msingi sana umesema

Ipo siku ndani ya Bunge Wazanzibar walilamika kuhusu mambo kadhaa. Waziri wa mambo ya Muungano wakati huo alikuwa January Makamba. Yeye aliwajibu na kusema, wanapata haki tena zaidi. Alitolea mfano wa mgao wa umeme na kusema, wakati Tanga na Dar zina mgao, Zanzibar haikuwa na mgao. Alisema hata shughuli za kiuchumi katika miji kama Tanga zilisimama ili umeme uende Pemba na Unguja.

Kiongozi anayeshughulikia mambo ya Muungano ni VP kwahiyo anajua fika nini kinaendelea

Waziri anayeidhinisha pesa ni Mwigulu Nchemba, anajua fika nini kinafanyika.
Kuna Waziri mmoja Mwanamama aliondolewa Wizara ile kwasababu tu katika ziara na migao hakufurshisha watu

Wabunge wanajua, kwani Ali Kessy wa Mpanda alipokuwa anasema wazi Bungeni wote walimshangilia. Wanajua nini kinaendelea lakini matumbo yao ni muhimu kwa muda huu

Viongozi wanajua nini kinaendelea lakini hawana Uzalendo wa kusimamia masilahi ya '' Mama Tanganyika''
VP ni mteuliwa wa Rais hakupigiwa kura. VP anavizia tu awe mtu mwema ili ikifik wakati naye ateuliwe.
Mawaziri wanaogopa vyeo vyao kwasababu wakienda kinyume anaondolewa

Kuhusu nguvu ya Rais wa JMT ni kweli unachosema. Tazama Wizara zisizo za Muungano wapo! tena kuna Wizara, Waziri na Katibu mkuu wake ni Wazanzibar. Halafu nyuma ya pazia utawasikia wakilalamika mambo ya Muungano kuongezwa. Wakipewa fursa kimyaa. Huu ndio utamaduni wao, Unafiki
 

Malipo hapa hapa duniani
 
mkuu unaishi Tanzania kwel au unamakazi nje ya nchi? maana unachokieleza ni as if kunamtu anakulisha, Kwa Nini nasema hivyo?

Kwa sabb unahisi muungano kuwepo migogoro itaisha wapi ulisikia? hyo ndoa au ushawahi kusikia ndoa ambayo Haina mgogoro?

hata siku 1 mkuu wa majeshi ni mmoja tu na IGP ni 1 tu umependa au hujapenda hao wengine niwasaidizi tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sabb unahisi muungano kuwepo migogoro itaisha wapi ulisikia? hyo ndoa au ushawahi kusikia ndoa ambayo Haina mgogoro?
Una maana Muungano maana yake ni matatizo? Mbona tunakuonyesha matundu hujibu!
1. Tetea hoja yako kwamba Muundo wa sasa ni mzuri. Ikiwa ni hivyo malalamiko yanatoka wapi?
2. Ikiwa Rais ni mmoja, inakuwaje Rais huyo hana mamlaka Zanzibar?
3. Inakuwaje sheria zilizotungwa na Bunge la JMT lenye Wabunge kutoka Zanzibar na Baraza la Wawakilishi, haziwezi kufanya kazi Zanzibar hadi ziridhiwe upya na Baraza la Wawakilishi. Nchi moja inakuwaje na haya?
3. MoU kati ya Tanzania na Zanzibar iliwahi kutokea lini katika Muungano? Huyu Tanzania ni yupi huyo tofauti na yule wa Tanganyika na Zanzibar? Rais wa Tanzania iliyosaini MoU na Zanzibar ni wa kuchaguliwa na watu wa eneo gani?
4. Mchango wa Zanzibar katika Muungano upo wapi? Formula gani inatumika ikiwa tuna Formula za 'mfao'

Hakuna tutazi la kuelelimishana, nipo hapa kujifunza pia. Nisaidie
 
Tatizo la Muungano linasababishwa na mambo mengi ikiwemo 'taboo' yaani mwiko kuuongelea
Muungano hautetewi kwa hoja bali vihoja na viroja. Ni wa pekee, ni tunu, ni muhali n.k.

Watanganyika wakapigwa marufuku kuuongelea kama tulivyoona sakata la Mbowe lililoleta kelele zisizo na kichwa wala miguu. Wazanzibar kama kawaida wakapewa 'free ride' ya kutukana kama tunavyowasikia akina Masoud Othman, Jussa, Duni n.k.

Tunapoonyesha matundu ya Muungano wenye akili timamu watajifunza, wenye uelewe katika umbali wa pua hawatatuelewa. Bila kuuongelea Muungano na yaliyojificha chini ya kapeti ipo siku Muungano utakuwa 'glass' na ikianguka ni kuvunjika papo hapo.

Kituko cha Muungano cha leo.
Wazanzibar wanasema mambo ya Muungano yabaki 11 ya mkataba wa awali.

Ndani ya Bunge kuna Wabunge 393 akiwemo AG. Ukimuondoa AG wanabaki 392 na ukiondoa 80 wa Zanzibar wanabaki 312 wa Tanganyika.

Ikiwa Bajeti ya Kilimo, Mifugo , Afya au Elimu itapigiwa kura na kufungana 156/156 kati ya Watanganyika wa YES na NO, watakaoamua bajeti hizo ni Wazanzibar 80, wale wale wasiotaka mambo ya Muungano yaongezwe.

Wabunge wa Zanzibar wapo kamati za BUNGE za mambo yanayohusu Tanganyika.
Katika kamati hizo Wazanzibar hao wana maamuzi yanayogusa masilahi ya Watanganyika.

Wakirudi Zanzibar wanadai hawataki mambo ya Muungano yaongezwe , mambo yale yale waliyokuwa wanayasimamia katika kamati huko Nkasi, Nyamagana, Kadewele, Isevya na Handeni kusiko wahusu.
 
Consinstency unayo mkuu, Kutetea Jambo moja kwa 13 yrs sio mchezo. Heko!!
Kwa kuwa umekuwepo kwenye mjadala huu wa Muungano mda mrefu naomba nisaidie haya machache.
1.Why TRA wapo zenji ikiwa mapato hayavuki kuja huku?
2. Unadhani why Tuliungana nao, Ikiwa saiv tukifanya analysis tunaona hatuwahitaji.
3. Unadhani watanganyika Tukianza kudai Tanganyika yetu tutaipata? Na tukiipata Kuna mabadiliko yoyote yatatokea kwa maana ya hali ya mtu mmoja mmoja?

4.Je ipi itakuwa hatma ya Wazanzibari waliopo Tanganyika? Watakubali muungano Uvunjwe ili waishi kama raia wa Kigeni?

Nimekuuliza hayo sababu naamini, kwa consinstency uliyonayo kwenye huu mjadala ushawahi jiuliza maswali hayo nnayojiuliza mimi.

Binafsi huwaona wazenji kama ni watu wa Kujitenga na Kulalamikia kila kitu, hata tukiwa Vyuoni walikuwa hivi.
Hivyo judgement yangu haiwezi kuwa sawa kuhusu Wazenji, daima nitakuwa Biased.
 
Consinstency unayo mkuu, Kutetea Jambo moja kwa 13 yrs sio mchezo. Heko!!
Niuruhusu nipitie hoja zako kwa mandiko tofauti

Consistency ni suala la kulielewa jambo na Watanganyika wachache walielewa hili.
Wengi hawakujali sMuungano, waliwakubali Wazanzibar kama Watanzania licha ya Ubaguzi wa Wazanzibar

Watanganyika walikatazwa kujadili Muungano ''taboo' wakiambiwa ni 'Muungano pekee, ni Tunu, n.k.' na kuujadili ilikuwa kama ''Uhaini' Lengo wasijue kwamba wamebeba mzigo peke yao.

Mjadala wa Muungano unajulikana vizuri kwa Wazee kama Warioba, Msekwa, Jenerali kwa uchache wa kuwataja.

Watanganyika wakipigwa marufuku kuujadili kama ilivyoonekana kwa tukio la Mh Mbowe, Wazanzibar waliachwa waseme watakavyo. Siku za nyuma walikuwa na 'slogan' '' kama hamfanyi abcd' tunavunja Muungano.

Wazanzibar wakaeneza uongo kwa kuifanya Zanzibar kama mhanga 'Victim' wa Muungano na si 'mfaidika' Beneficiary. Ikaonekana Zanzibar inaonewa, inanyimwa , inapigwa vita na kauli nyingi za kipuuzi kama hizo.

Kwa mfano, kuundwa kwa tume ya pamoja ya Fedha ilionekana Tanganyika inaficha kitu.
Rais Mwinyi kaweka ukweli waziii akisema mfuko wa pamoja utailazimu Zanzibar kuchangia, itaumia .

Mh Mwinyi alikuwa anamjibu VP OMO wa ACT anayeeneza uongo huo katika mikutano bila aibu! kwa miaka mingi

Kuna Uzi JF wa Zitto (ACT) wa July 2019 ukisema 'eti account ya pamoja' ni ya kugawana mafao ya Muungano.

Zitto anasema tunapaswa kuwalipa Zanzibar Trilioni 7. Uongo mtupu! fedha za Watanganyika ndio mafao ya Muungano? Ni kama vile ARDHI ya Tanganyika imegeuzwa ya Muungano. Zitto hakusema Zanzibar inachangia nini katika mafao ya JMT.

Taratibu tumebomoa uongo wao si kwa uongo bali kwa 'facts' na siku hizi hutawasikia wakisema hovyo .

Kwa kuwa umekuwepo kwenye mjadala huu wa Muungano mda mrefu naomba nisaidie haya machache.
1.Why TRA wapo zenji ikiwa mapato hayavuki kuja huku?
Lengo la TRA NI kukusanya fedha zote za nchi (JMT) halafu kufanya 'remittance' kule Zanzibar kwa kuwa ina 'status' Pili, kurahisha biashara kwamba mzigo ukilipiwa Zanzibar unaingia bara kwa maana ya ku 'harmonise' shughuli na kuondoa viwango tofauti kati ya Bara na Zanzibar.

Wazanzibar wakakataa na kuanzisha ZRB, hilo likaongeza mzigo wa kodi. Kilichofanyika ni kuacha mapato ya TRA yabaki . Hili likaleta ugumu wa biashara ambao Zanzibar walilamika kwamba nchi moja kwanini bidhaa zilipiwe kodi mara mbili.

Marais wote na hasa JPM alikataa bidhaa kutoka Zanzibar zisiingie bila kodi kwasababu Zanzibar kuna tax evasion kubwa na viwango vya tax ni vidogo sana ukilinganisha na Bara, na inatumika kama uchochoro.

Kwa maana kwamba kontena linaloshushwa Dar es Salaam linalipiwa zaidi kuliko kushushwa Zanzibar.

Kama unakumbuka clip ya Mbunge Ali Kessy alisema ' kontena' la pikipiki ni 40Milioni Dar , kule Zanzibar ni 5 Milioni. Kuna taarifa baada ya JPM utartaibu wa kupitisha bidhaa kutoka Zanzibar umerudishwa tena, kufuta kero

Hakuna tatizo TRA kuacha mapato Zanzibar ikiwa Zanzibar watachangia Muungano kwa njia nyingine.
Pili, hakuna bidhaa zitakazoingia kutoka Zanzibar bila kulipiwa kodi kwa kisingizio cha nchi moja wakati Mtanganyika ataumia kwa kodi zaidi TRA isipopata mapato ya kutosha.

Lakini pia kuna kituko cha Muungano.
Wafanyakazi wa TRA Zanzibar wanalipwa na TRA JMT ingawa mapato yanabaki kwa SMZ.
Ni sawa na kituko cha Wafanyakazi wa Uhamiaji kulipwa na JMT mapato yanatokana na Uhamiaji ni mali ya SMZ.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…