Dark wealth, dark path, is the only way to rich

pesakilakitu

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2024
Posts
1,618
Reaction score
2,861
Jipige kifua, bisha sana, toka jasho sana, kua atheist, kua mlokole hadi ukiomba unapiga kichwa kwenye ukuta, vyovyote ila ukweli ndio huo

To be rich, ufalme wa giza, ndio njia pekee ya kuweza kupata utajiri na mali za dunia hii na kama wasemavyo, money is power.

Kama uongo waulize wanaojaza crusade za maombi kisingizio cha mkesha, wafanyabiashara wakubwa, wote hao dark kingdom ndio back up yao.

And am ready to ascend to that kingdom.

"Kisha The Devil akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia."

Akamfukuza..ila ajabu ni kwamba hakumpinga kauli yake kwamba mali na utajiri ni vya kwake.
 
Pesa/Nguvu/ Heshima na fahari zote zilizopo duniani na hata huyo shetani mwenyewe Ni Mali ya Bwana(MUNGU).

Na nguvu ya Utajiri inatokana na nguvu ya kiroho ( nguvu halisi isiyoonekana ifanyayo kazi) ambayo mtu husika amekuwa connected nayo.. nakuitumikia kwa moyo wote.

Uko refer mstari huo wa biblia kwamba ukinisujudia , nitakupa milki zote za ulimwengu huu Kuna maana kubwa lakini Ni sawa na kuchagua kumuomba Mali Yusuf bakhersa na wakati una access na bakhersa mwenyewe.
Mfano tu.

Kila la kheri.
 
Tafuta taratibu utapata, njia ya giza ina utajiri lakini umejaa mateso, mahangaiko na taabu tupu.

Nje utaonekana kama una nuru lakini moyoni kunawaka moto.

Wazazi/walezi wako hawakuwa wajinga kuacha kukutoa kafara ili wawe matajiri.
 
Utalia ww acha ujinga......kafanye kazi kwa bidii katafute maarifa mapya utafanikiwa shetani ni mbaya sana
 
Muulize mlokole kuwa shetani alimpandisha Yesu mlimani na kumuonyesha ufalme wa dunia kuwa ni wake. Kama unasoma Biblia kwa ufasaha inatosha kuelewa kuwa utajiri wa dunia ni wa shetani. Mpigie shetani magoti ili upete hapa duniani, maisha ni haya haya. Waliogundua hilo wala hawasemi, wanasali kiujanja na kula bata.
 
Tafuta taratibu utapata, njia ya giza ina utajiri lakini umejaa mateso, mahangaiko na taabu tupu.

Nje utaonekana kama una nuru lakini moyoni kunawaka moto.

Wazazi/walezi wako hawakuwa wajinga kuacha kukutoa kafara ili wawe matajiri.
Na mimi nikuulize, Sehem za siri za baba yako ni sawa na za kwako? Kwamba urefu na upana..je ni sawa?
 
Upo sahihi mkuu!
Nilikua nasubiri siku moja mtu aseme hiki kitu.
Katika agano jipya watu wamchao bwana baraka walizoachiwa ni za rohoni tu za mwilini watu watazipata kwa shetani.
Waefeso 1:3, Marko 10:23
 
Kijana Soma Biblia....! Utajiri wa Mungu ni Utajiri wa amani na furaha

FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA.

Shalom Taifa la Mungu....

Kilichonifanya niandike hii mada ni kisa hiki....

Siku moja nilikuwa soko fulani maarufu. Nikaingia dukani kwa mfanyabiashara mmoja nikanunua vitu....tukapiga stori mbili tatu akaniambia..." hizi hela na utajiri ni vya shetani kwani hata biblia inaonyesha sehemu ambayo shetani alimwambia Yesu " nisujudie nikupe utajiri "....Mathayo 4:8-9.

Mimi nikamjibu biblia Takatifu inasema FEDHA na dhahabu ni MALI YA BWANA. Hagai 2:8.

Nikamwambia tena biblia Takatifu inasema Ulimwengu na vyote viujazavyo ni MALI YA BWANA. Zaburi 24:1-2;
1 Kor 10:26.

Ikisemwa ni Mali ya Bwana....maana yake mmiliki halali wa fedha na dhahabu ( utajiri) ni Bwana/ Mungu ( na warithi wake)......

Sasa toka wakati huo nikapata maswali mengi sana...baadhi ni haya...

1. Biblia inatuambia Mungu aliumba mbingu na nchi. Mwanzo 1:1....Je, inawezekanaje huyo aliyeumba mbingu na dunia ASHINDWE kuwapa aliowaumba utajiri? .....

Nikapata neno hili...Kumb 8:18...inasema UTAMKUMBUKA BWANA MUNGU WAKO MAANA NDIYE AKUPAYE NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI. Kwahiyo nikajua sababu mojawapo ya umasikini ni KUMSAHAU MUNGU.

2. Najua kuwa shetani hajaumba kitu. Wala hamiliki chochote. Tena biblia inasema yeye ni malaika aliyeasi akafukuzwa mbinguni.( Isaya 14:12-14.)
....sasa anatoa wapi mali za kuwapa watu wanaomwabudu?

Nikapata neno hili
SHETANI NI MWIZI ..
Yohana 10:10
Tena SHETANI NI MUONGO na ni baba wa uongo na asili yake ni uongo. Yohana 8:44

**Hivi ulishawahi kukutana na MWANAUME maeneo ya stendi ya basi anaonekana amechoka kwa ulevi halafu amebeba HERENI za GOLD kama gramu 3@ halafu anakuambia nipe elfu 30 nikuuzie? Ukimuuliza za nani anakujibu.."ZANGU".....

*Utajiuliza wewe mwanaume hereni za kike zako?-uongo

*Utajiuliza mbona huyu mtu haonekani ana uwezo wa kumiliki duka la sonara? Mbona anauza mkononi tena pair moja?--mwizi

*Utajiuliza mbona thamani ya hizi hereni; bei yake na mazingira anayouzia yana
walakini ?- utapata jibu kwamba huyu ni mwizi ama hizi hereni sio gold anataka Kunitapeli

Sasa huyo ndio shetani alivyo. Hajaumba kitu na wote tunajua hilo...hamiliki kitu wote tunajua; lakini anaaminisha wengine kwamba atawapa UTAJIRI KWA NJIA RAHISI......MUONGO; MWIZI; TAPELI....

**Asiye mmiliki wa kitu hawezi kukupa kitu. Kama sina nguo natembea uchi....maana yake hata nguo ya kukugawia wewe sina pia....."U CAN'T GIVE WHAT YOU DON'T HAVE "

Kama wote tunajua shetani hana mali lakini anagawa mali basi tuwe na UHAKIKA kwamba AMEIBA MAHALI...sababu yeye ni MWIZI...na kwa sababu sio chake kihalali anagawa kihasara hasara bila kufuata utaratibu wa mwenye mali....nia yake ni KUKUTAPELI....

Biblia inatuambia nia ya mwizi ni kuiba ; kuua na kuharibu;Yohana 10:10.

Kwa hiyo ukienda kwa shetani kwa sababu yoyote ile iwayo..... nia yake ya ndani ni KUKUIBIA, KUKUHARIBIA na KUKUUA hata kama kwa nje unajiona unapata mali na cheo.....huo ndio utapeli wa shetani.

Tapeli ni mwizi anayejificha kwenye Sura nzuri isiyoonyesha nia mbaya ya ndani kwa urahisi....Ukifanya kazi/ biashara naye mwanzoni unaeza ukaona mafanikio; ukamuamini, lakini mwishoni LAZIMA akulize vibaya.

**Biblia inatuamuru KUMWABUDU MUNGU PEKE YAKE.....Mathayo 4:10,
Kutoka 3,5; kumbukumbu 5:7,9a.

**Tena biblia inatukataza kuwaendea WAGANGA/ MAKUHANI WA SHETANI ili kufanya ibada kwa shetani kwa sababu yoyote ile iwayo.
Walawi 19:31, Kumb 18:10-12.

**Ila siku hizi imekuwa kawaida kabisa kuona MATANGAZO ya UGANGA yakisomeka.....njoo kwa MGANGA XX upate...
-pete ya utajiri/ bahati
-pesa za majini
-mafanikio kazini
-zindiko la kuvuta wateja kwenye biashara.....

***NA KWA SABABU HIYO.....
watu wengi hata WAKRISTO wanaamini Kuwa HUWEZI KUTAJIRIKA BILA KUABUDU SHETANI....

***Ndio maana imekuwa shida- mtu akifanikiwa sana katika jambo lake anahisiwa amejiunga na waabudu shetani...

***Tena imekuwa shida zaidi kwamba watu wengi hata WAKRISTO wanaabudu shetani kwa namna mbali mbali ili tu wapate mali na vyeo.

***Hivi kweli Mungu anaweza kukuumba wewe na ulimwengu wote ashindwe kukupa mali ambazo ni yeye pia kaziumba?

***Hivi kweli ni akili gani inayotumika ya kwenda kuomba mali kwa asiye na mali yoyote ile?

**Ama hatuamini lile neno linalosema kwamba sisi ni wana wa Mungu (kama Yesu) na ni warithi pamoja naye? Rumi 8:16-17. Maana yake sisi ni wamiliki / warithi halali wa mali za Mungu.

Ama tuna mashaka na uwezo wa Yesu wa kutupatia mahitaji yetu katika huo utajiri alionao?
Hebu soma hapa uone:Wafilipi 4:19.

**Hii tabia ya Wakristo kusema kwamba kila mafanikio ni ya kishetani na au kwenda kuomba mali kwa shetani ....NI TANGAZO KWAMBA YESU HAWEZI KUTAJIRISHA WAKRISTO....kwa hiyo tunamdhalilisha Yesu na nguvu zake.

**Tunawahalalishia wengine waendelee kuabudu miungu mingine inayoweza kuwapa mahitaji.

Yaani sisi Wakristo ndio tunakuwa wapotoshaji wakubwa wa imani ya kikristo na uweza wa Mungu.

Tuyachunge sana maneno yetu. Kwa Kuwa hatujui kwa hakika SIRI za mafanikio ya mtu ni vizuri KUNYAMAZA.

Zaidi sana TUSIFUNGE UWEZA WA MUNGU KWENYE MIPAKA YA AKILI ZETU. Maana hakuna neno gumu lolote asiloliweza. Kwa Mungu yote yanawezekana.

Mungu atubariki; TUBADILISHE MTAZAMO wetu juu ya Mungu na uweza wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…