Darsa la tafsir ya qur'an ujiji miaka nenda miaka rudi na Hamisi Hababi

Darsa la tafsir ya qur'an ujiji miaka nenda miaka rudi na Hamisi Hababi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
1103407


Darsa hii ya Tafsir ya Qur'an hapa Ujiji kila Mwezi wa Ramadhani iliasisiwa na Sheikh Swedi Bin Abdallah Silanda miaka mingi iliyopita.

Sheikh Swedi alikuwa mwanafunzi wa Sheikh Khalfan Zindijali al Bulush kutoka Zanzibar.

Katika miaka ile Zanzibar ilikuwa na uhusiano mkubwa sana na sehemu hizi za Tanganyika
hadi kufikia Congo ya Mashariki misafara ya biashara ikiunganisha Ujiji na Bagamoyo kisha
kuvuka kuingia Zanzibar.

Sheikh Zindijali kutoka Zanzibar alikuwa aaliim mkubwa aliyeishi Ujiji na alifundisha wanafunzi
wengi.

Historia inaonyesha kuwa Sheikh Swedi bin Abdallah akiwa kijana mdogo alijiunga na King's
African Rifles (KAR) wakati wa Vita Kuu Vya Pili (1939 - 1945).

Sheikh Swedi mwaka wa 1941 alitoroka jeshi na kwenda Baghdad, Iraq.

Akiwa Iraq Sheikh Swedi aliamua kusoma dini kwa masheikh wakubwa wa Iraq wa wakati wake.

Baada ya vita alirejea Ujiji na akaanzisha madrasa yake na kuanza kusomesha na kila Mwezi
wa Ramadhani alikuwa anasomesha Tafsir ya Qur'an.

Sheikh Swedi alidumu katika kusomesha tafsir kila Mwezi wa Ramadhani hadi alipofariki mwaka
wa 1961.

Kuanzia mwaka wa 1961 madrasa ikawa chini ya Sheikh Iddi Hassan Kiburwa na yeye akaendeleza
kusomesha Tafsir ya Qur'an hadi alipofariki mwaka wa 1977.

Kuanzia mwaka wa 1977 hadi 1979 darsa hili la tafsir likawa linasomeshwa na Sheikh Hilal Swedi
Zimba.

Kuanzia mwaka 1979 Darsa la Tafsir ya Qur'an liliendelezwa na Sheikh Suleiman Jaafar Kiomone
mpaka alipofariki mwaka wa 1989.
.
Tokea mwaka wa 1989 darsa hili la tafsir linasomeshwa na Sheikh Hassan Iddi Kiburwa Sheikh wa
Mkoa.

Hakuna kitu kinachopendwa na Waislam katika Mwezi wa Ramadhani kama kuhudhuria
Darsa la Tafsir ya Qur'an baada ya sala ya L'Asr.

Hii imekuwa kalenda muhimu sana mjini Ujiji na watu wengi hukusanyika hapa msikitini kusikiliza
tafsir ya Qur'an ambayo hutanguliwa na kisomo cha tajwid kisha ndipo sheikh ataanza kusomesha.

Kila miaka inavyozidi kwenda ndivyo jinsi darsa hili la Tafsiri ya Qur'an katika Mwezi wa Ramadhani linavyozidi umaarufu wake na kujaza wasomaji na wasikilizaji wengi kama inavyoonekana katika picha hapo juu.
 
Safi Mzee Mohamed Said, napenda sana historia zako na namna unavyoweza kuwasilisha, sio kama vijana tumejawa Udini kwenye mambo ambayo hayana tija
 
Back
Top Bottom