BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) umesema mwakani unatarajia kuanza ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Kasi (BRT) katika awamu ya nne na ya tano.
Mtendaji Mkuu wa Dart, Dk Edwin Mhede amesema mikakati hiyo inakuja baada ya Serikali kupata mkopo wa Sh650 bilioni kutoka kwa washirika wa maendeleo.
“Benki ya Dunia imeongeza Dola 97.7 milioni (Sh219 bilioni) kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya nne kati ya barabara za Tegeta kupitia Bagamoyo na Ali Hassan Mwinyi na Barabara ya Bibi Titi katikati ya jiji,” alisema Dk Mhede.
“Serikali pia imepata Euro 178 milioni (Sh427 bilioni) kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya tano, utakaoanzia Barabara ya Kijazi, Ubungo kupitia Barabara ya Mandela. Njia hiyo pia itakuwa na tawi la Segerea.”
Alisema ujenzi wa miundombinu hiyo unatarajiwa kufanyika kwa awamu sita nchini, huku zikiwa zimefika tano na kusalia moja ambayo haijaanza utekelezaji wake.
Awamu ya kwanza ilianza kutumika tangu mwaka 2016, wakati ujenzi wa awamu ya pili umefikia zaidi ya asilimia 90 na utekelezaji wa awamu ya tatu unaendelea hivi sasa. Alisema wametangaza zabuni kwa ajili ya kuwapata makandarasi watakaohusika na ujenzi wa awamu ya nne na ya tano.
“Utambuzi wa makandarasi watakaohusika awamu ya nne umekamilika, tunaendelea na awamu ya tano.”
Meneja Mipango wa Usafiri Dart, Mohamed Kuganda alisema awamu hizo mbili zitajengwa kwa wakati mmoja kwa sababu fedha zimetoka kwa washirika wawili tofauti wa maendeleo.
Kazi ya awamu ya nne yenye urefu wa kilomita 25.9 itajumuisha ujenzi wa jengo la abiria la Kivukoni litakalochukua mabasi yaendayo maeneo ya Tegeta, Mbezi na Gongolamboto.
“Barabara itaanzia na kuishia kwenye kituo cha mabasi, kwa hiyo Kituo cha Kivukoni kitapanuliwa ili kuruhusu barabara hizo. Pia, katika awamu ya nne tutakuwa na ujenzi wa vituo viwili vya mabasi,” alisema Kuganda.
Pia, alisema urefu wa Barabara ya Bagamoyo ni kilomita 25.9, huku kilomita nne nyingine zitaongezwa kwa sababu kituo kitajengwa Boko. “Mwanzoni jengo hilo lilitakiwa kujengwa Tegeta Kibo, lakini tumebadilisha mpango na jengo hilo sasa litajengwa Boko karibu na Ofisi za Dawasa kwa kuwa hili ni eneo lenye watu wengi kuliko Tegeta Kibo,” alisema Kuganda.
Pia, alisema Dart itajenga karakana ya awamu ya nne Mbuyuni karibu na makutano ya Kunduchi, wakati karakana ya awamu ya tano itajengwa Temeke Mwisho.
Kuganda alisema wakala huo unatafuta maeneo mengine ya kujenga karakana nyingine zaidi.
Dart inatarajia kuwa watu 889,000 watasafiri kila siku kwa awamu ya tano na wengine 698,000 watatumia miundombinu ya ujenzi wa awamu ya nne kufikia mwaka 2030.
Alisema mabasi 590 yatanunuliwa awamu ya nne baada ya kukamilika, huku magari 240 kati ya hayo yakiwa madogo.
Katika awamu ya tano jumla ya magari 430 (madogo na makubwa) yatanunuliwa katika awamu hiyo.
“Idadi ya mabasi itaongezeka sana ifikapo mwaka 2030 kwa sababu idadi ya wasafiri pia itaongezeka,” alisema Kuganda.
MWANANCHI