Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohammed Mchengerwa amezitaka Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) na Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (Udart) kuhakikisha ifikapo Desemba 2024, mabasi ya mwendokasi yanayotakiwa katika barabara ya Morogoro na ya Mbagala yawe yamepatikana.
Mchengerwa ametoa maagizo hayo Jumatatu Septemba 2, 2024, alipozindua mageti janja na kadi janja kwa ajili ya usafiri wa mabasi ya mwendokasi, jijini Dar es Salaam.
Katika kufanikisha hilo, Mchengerwa amesema hakuna haja ya kuwasubiri wawekezaji kutoka nje ya nchi kwa kuwa wapo Watanzania wengi wanaweza na kutaka wapewe nafasi, wakiwemo wamiliki wa mabasi ya mikoani.
Soma Pia: Amos Makalla: Mabasi ya Mwendokasi yataanza kazi Mbagala Desemba 2024
"Watanzania wamesubiri kwa muda mrefu kupatikana kwa mabasi hayo na sasa inatosha, hatutaki tena kusikia changamoto hii wizarani,” amesema.