Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 208
- 91
Wanafunzi wa shule za kutwa jijini Dar es salaam wanakumbana na changamoto kubwa sana ya usafiri, hii inapunguza morali ya watoto kupenda shule, pia ni moja ya sababu ya matokeo mabaya kitaaluma yanayochangiwa na kuchelewa vipindi, kuchoka sana na hivyo kupunguza umakini wakati wa vipindi na pia kukosa mda wa kutosha kujisomea kwa sababu mda mwingi wanautumia wakiwa barabarani, kubwa zaidi wanafunzi wananyanyasika sana.
Mbali na athari hizo;, hali hii pia inachangia mmomonyoko wa maadili, kwa sababu wakati mwingine wanafunzi wanalazimika kupambana na watu wazima au kurushiana maneno kutokana na kashkash ya kugambonia usafiri, lakini pia hali hii wakati wwingine hupelekea unyanyasaji wa kijinsia/kimaumbile hasa kwa watoto wa kike kwa kujikuta wakishikwa ama kupapaswa sehemu ambazo sio sahihi.
Soma Pia: Mabasi ya mwendokasi yawe suluhisho kwa wanafunzi mikoani
Ninashauri mamlaka zinazohusika kwa maeneo ambayo tayari kuna usafiri wa mabasi yaendayo haraka, yatengwe mabasi maalum kuwasaidia wanafunzi wakati wa kwenda na kutoka shule, hii itasaidia sana kuwapunguzia ghadhabu na usumbufu mkubwa wanaopitia ukilinganisha na umri wao, maana wakati mwingine wanalazimika kutumia nguvu kushindana na watu wazima wakigombania kupata nafasi ya kuingia kwenye gari. Lakini pia itasaidia kuwakutanisha pamoja wanafunzi kutoka shule tofauti na kuweza kubadilishana mawazo na maarifa wakati wa safari.