Darwin Nunez ni Old Trafford au Anfield, kazi ni kwake

Darwin Nunez ni Old Trafford au Anfield, kazi ni kwake

Joined
Oct 16, 2015
Posts
20
Reaction score
56
IMG_0359.jpg
DARWIN NUNEZ NI OLD TRAFFORD AU ANFIELD ,KAZI NI KWAKE .

Kalamu ya Nasri kulemba .

Ngoma bado ngumu kati ya magwiji wawili kutoka katika nchi ya malkia ,, waswahili wanamsemo wao mmoja mwenye kisu kikali ndio hula nyama.

Hii ni hadithi nzuri inayovutia,Nunez ni sawa na mrembo aliyekatikatika ya wanaume wawilli wenye pesa ndefu wenye kushindana kumpata .. embu angalia hii njia walizopitia hawa wanaume kuhakikisha wanampata Nunez.

Manchester United ..

Hii ndio timu ya kwanza kuonyesha nia ya kutaka kumsajili Nunez ,Nini walichokifanya hawa mashetani wekundu .. kwanza United kwasasa si timu iliyo na ushawishi kwa wachezaji kutokana na kile kinachotokea uwanjani ,pili wapo kwenye project.

Sio rahisi kwa mchezaji kijana mahili kama Nunez anayetaka kuwa mkubwa kwenda kwenye timu ambayo inatakiwa kujengwa kwa miaka mitatu ndio iwe shindani na kuchukua mataji au ionekane. Wao United wanalijua hilo.

Walichokifanya Man United ni kwenda kuwasiliana moja kwa moja na wakala wake ,maana kupitia yeye itakuwa ni rahisi sana kumpata Nunez , kwanza ni kumueleza mipango yao , pili ni ushawishi wa pesa kwake na kwa mteja wake.

United wakawasiliana moja kwa moja na wakala ,mazungumzo yameendela mpaka kufikia alasili ya leo. Kwanini United walianzia kwanza kwa wakala …sababu nimeshakueleza hapo juu.

Kwa Upande wa Klabu anayoitumikia Nunez, Benfica wenyewe wameshaweka dau maalumu endapo utamuhitaji Nunez .. Kimsingi wao wanataka pesa tu . kwa hiyo kazi kubwa ni makubaliano binafsi na mchezaji ndio maana United wao waliamua kuanza kwa wakala ambaye ni kama Nunez ,kwasababu kwa Nunez kwao ndio njia ngumu zaidi kuliko kwa Benfica.

Liverpool fc .

Hawa jamaa wenyewe wapo kwenye mafanikio …kimsingi wanaushawishi kama timu .. kwao kila mchezaji mahili kwasasa anahitaji kukipiga katika klabu yao .. wanalijua hili na ndio maana wao waliamua kwenda kuongea moja kwa moja na klabu ya Benfica ..

Waliulizia dau na kisha wakajipima na wakaona wanauwezo wa kumudu ghalama hizo … Kama nilivyokwambia hitaji la Benfica ni pesa; Liverpool wao wameshaafiki kiasi cha pesa ambacho wao wanahitaji.

Kuhusu mchezaji …Liverpool hawana shida kutokana na kile wanachokifanya kwasasa,(wanaushawishi ,wapo kwenye ushindani ). kwa mchezaji kama Nunez hii klabu inamfaa zaidi ili kuwa mkubwa kwa wakati maana imeshajengeka.

Kwa hiyo kwa mchezaji sio tatizo … kazi ngumu kwao ilikua ni kujipima kama wanaweza kufika dau la usajili na wamefika .. kwao njia ngumu ilikua ni kwa benfica kama klabu kuliko Nunez.

Nini kinaelekea kutokea ..

Kwa upande wa Man United wao kama wakiweza kumalizana vizuri na wakala basi ni rahisi kwenda na kupeleka mzigo kwa Benfica …ila watakutana na ugumu maana watakuta Liverpool wamefika kile ambacho wao United watatoa ..Hii inamana watahitaji kubolesha maslahi mengine zaidi kwa Benfica ili wavutike na ushawishi kuliko kile wanachokitoa Liverpool …

Liverpool wao waneshalizana na klabu …kwaiyo wataenda moja kwa moja kwa wakala …hii inamaana wao liverpool watahitaji kubuni kitu kingine zaidi chenye ushawishi kuliko kile walichomalizana kati ya wakala na United .

Darwin Nunez…

Tukio lote hili linamuhusu yeye … ishu kubwa sio kwa klabu au wakala , kwasababu wao wanataka hela … Maamuzi yake ndio yatakayoamua utata huu… Ni wapi ataenda …na kwanini amemaua kwenda atakapochagua … Na je ni pesa au mikakati .. kazi itabaki kwake kwenye maamuzi .

NB: Hii hadithi ni tamu sana …maana kila timu imepita katika njia yake inayoona inafaa ,na hakuna hata timu kati ya hizo mbili iliyo kwenye hatua nzuri kuliko nyingine … hii inshu ipo 50/50 mpaka sasa …. Sio Liverpool au Manchester united.

Lolote linaweza tokea

Tusubili tuone …

Nasri kulemba ..
 
Dogo akiambiwa achague atachagua MUFC ila akienda Liva atakula benchi la kutosha na kama Man U wangedhamiria kwelikweli wasingebabaishwa na uyu Dogo wangeweka mzigo mezani naona ETH kamuweka uyo dogo kama pendekezo la Mwisho tu
 
Dogo akiambiwa achague atachagua MUFC ila akienda Liva atakula benchi la kutosha na kama Man U wangedhamiria kwelikweli wasingebabaishwa na uyu Dogo wangeweka mzigo mezani naona ETH kamuweka uyo dogo kama pendekezo la Mwisho tu
Hivi hiki ulichokiandika umekitafakari?[emoji1787]
 
Back
Top Bottom