DAS wilaya ya Mvomero: Hakuna akili za kurithi kwa mtoto

DAS wilaya ya Mvomero: Hakuna akili za kurithi kwa mtoto

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mvomero, Said Nguya amewasisitiza wazazi kuwa hakuna akili za kurithi kwa mtoto, sababu uwezo wa akili hutokana na lishe bora tangu mama anapopata ujauzito.

Nguya ameyasema hayo Jumapili Septemba Mosi, 2024 alipokuwa akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi kwenye mahafali ya Shule ya Msingi Kwa Muhuzi iliyopo Dakawa wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro.

Nguya amekemea pia tabia ya baadhi ya wazazi kutowahimiza watoto wao kwenda shuleni badala yake huwatumikisha kazi za kulima mashamba ya mpunga.

Soma Pia: Naomba ufafanuzi kuhusu akili na uelewa wa watoto kwenye makuzi yao

Amesema jambo hilo limeendelea kuongeza utoro na kusababisha uote mizizi na baadhi yao kuacha kabisa masomo.
 
Arudi o-level akafundishwe vizuri biology
 
Back
Top Bottom