Data analysis bure!

Data analysis bure!

Exav

Member
Joined
May 6, 2010
Posts
65
Reaction score
18
Habari wapendwa!

Karibu nikufanyie data analysis bure kwa mahitaji mbalimbali.
  • Inawezekana una repoti kazini,shuleni, au chuoni,
  • Inawezekana unataka kujua ufanisi wa mradi wako kwa kadri ya malengo yako,
  • Inawezekana una utafiti wako unaufanyia kazi na unahitaji majibu ya swali kuu,
  • Inawezekana unataka kufanikisha (ma)chapisho lako (publication/paper),
  • Inawezekana una mahitaji mengine yoyote yanayohitaji uchambuzi wa taarifa, au hata ushauri ,
Karibu upate huduma!

Kama una quantitative data utanufaika na yafuatayo hapa chini. Kama una qualitative data, utanisamehe, ila naweza kukushauri!
  • Nitakufanyia basic data cleaning, editing, coding, labeling n.k.,
  • Frequency distribution a.k.a one-way tabulations,
  • Bivariate analysis au cross-tabulations (with chi-square tests, t-tests, ANOVA etc.),
  • Multivariate analysis (*)
Ukihitaji huduma, niandikie hapahapa au inbox. Tutajadili hitaji lako kwanza, tukielewana, utatuma data zako, na utahudumiwa kikamilifu.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Msukumo wa kufanya hivyo:
Miezi miwili iliyopita (Nov 2020), nilialikwa kwenda kanda ya ziwa kuhudhuria mkutano wa wanataaluma fulani (sitataja). Pamoja na mambo mazuri yaliyokuwepo, niliumia sana kuona udhaifu mkubwa sana upande wa takwimu (statistics) katika mawasilisho yao. Mbaya zaidi, wengine walikuwa ni wahadhiri wa vyuo vikuu vyetu hapa nchini. Shida kubwa ilikuwa ni uchakataji duni wa data usiojibu kikamilifu swali lengwa, uwasilishaji mbovu wa majibu, idadi ndogo sana ya wahojiwa (hii ilikuwa inashawishi vinginevyo (naomba nisifafanue)) n.k

Kwa hiyo, nilijikuta najiuliza sana kwamba, ni kwa namna gani naweza kusaidia waTanzania wenzangu, walau kwa kile kidogo ninachokijua. Kwa kuanzia, hivi ndivyo nilivyoamua kuanza. Kwa wengine wenye ujuzi wa aina hii, saidia pale inapowezekana.

Karibuni!

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
*hii itategemea
 
Jambo la maana hili data analysis ni kipengele kwa wengi sana
 
Back
Top Bottom