Data Privacy Day: JamiiForums kwa kushirikiana na Lawyers Hub kufanya Mjadala kuhusu Sera za Akili Mnemba (AI) Januari 28, 2025

Data Privacy Day: JamiiForums kwa kushirikiana na Lawyers Hub kufanya Mjadala kuhusu Sera za Akili Mnemba (AI) Januari 28, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ikiwa kesho Januari 28, 2025 ni Siku ya Faragha ya Taarifa Duniani (Data Privacy Day), JamiiForums kwa kushirikiana na Lawyers Hub wameandaa Mjadala wa Sera za Akili Mnemba.

max 1.jpg

Tanzania na Afrika kwa ujumla inashuhudia mapunduzi makubwa ya Teknolojia ikiwemo Teknolojia ya Akili Mnemba ambapo ulinzi wa taarifa binafsi za watu pamoja na faragha ni mambo ya kuuchukulia kwa uzito mkubwa kutokana na madhara yanayoweza kujitokeza ikiwa hakutakuwa na misingi mizuri ya kuzisimamia.

max.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo atakuwa miongoni wa wazungumzaji wa mjadala huu wenye Lengo la kuhamasisha uelewa wa athari za AI katika faragha Barani Afrika, kutengeneza sera zinazozingatia muktadha wa Kiafrika, na kuimarisha ushirikiano wa wadau. Mdahalo huu pia utaainisha mbinu bora za matumizi ya taarifa na utekelezaji wa Akili Mnemba kwa uwajibikaji, kuhakikisha uwiano kati ya ubunifu na haki za faragha.

max 3.jpg

Tukio hili litawaleta pamoja wadau muhimu kujadili faragha na usimamizi wa teknolojia za AI, hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo masuala ya AI, ulinzi wa taarifa, na haki za kidijitali ni muhimu.

Ili kujisajili na kushiriki kwenye mjadala huo bofya hapa

max 2.jpg
 
Back
Top Bottom