Data za mwaka 2021, Tanzania na mataifa mengine zikionesha kiwango cha nishati ya umeme kilichozalishwa kwa mwaka Tanzania ina kipi cha kujifunza?

ASIWAJU

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
1,938
Reaction score
1,632
Data za mwisho wa mwaka wa 2021 ziki onesha viwango vya kinishati ya umene Tanzania pamoja na mataifa mengine walicho zalisha kwa mwaka.

Data hizo zili tawaliwa kwa taifa la China kwa kuongoza katika uzalishaji mwingi wa nishati za umeme, liki fuatiwa na taifa la marekani baadae India na mataifa mengine yakifuata.

Huu hapa mlolongo mzima wa mwaka 2021 kwa msaada wa Wikipedia kupitia wizara za nishati za mataifa husika.
Screenshot_20221224-093922.jpg
Screenshot_20221224-093922~2.jpg
Screenshot_20221224-093445.jpg
Screenshot_20221224-093643.jpg
Screenshot_20221224-094032.jpg

[ Kwa mwaka wa 2021 taifa letu Tanzania lili zalisha Megawatts 1605.86 ].
Zingatia kuwa:
1 Gigawatts = 1000 Megawatts
Maswali:
1. Je sisi kama taifa tuna jifunza nini kwa hayo mataifa yaliyo tuzidi katika kiwango cha uzalishaji wa nishati ya umeme kwa mwaka ?

2. Je sisi kama taifa ni ipi mipango yetu ipi katika matumizi ya makaa yetu ya mawe katika uzalishaji wa umeme ?

3. Je sisi kama taifa tume ridhia kuwa na hiki kiwango kidogo cha uzalishaji wa nishati ya umeme kwa mwaka huku tuki pambana kutafuta wawekezaji wakubwa ?

4. Je ipi mipango yetu kuhusu madini ya uranium tuliyo nayo na uzalishaji wa umeme ?

5. Je ipi mipango yetu katika uzalishaji wa nishati ya umeme kwa njia ya geothermal,jua,upepo na pia kwa njia ya gesi ?

6. Je sera zetu katika upande wa nishati zina endana na kasi ya dunia kwa sasa upande wa nishati ?
 
Mbona hujaweka hizo units zilizozalishwa na TZN kwa mwaka 2021 ili tujilinganishe?
 
1605.86MW ni installed capacity, sasa kama hii yote ilikuwa inazalishwa kwa mwaka mzima(itakuwa muujiza), inabidi uzidishe kwa masaa ya mwaka mzima ili kujiweka kwenye hiyo list

Nadhani katika siku 365.25, pengine tuseme tumezalisha kwa hiyo full capacity kwa siku 150 tu.

Hivyo, mwaka 2021 tumezalisha 5,781,096 MWh sawa na 5,781.1GWh
 
CCM wamekata tamaa, moto wa kupambana kwa ajili ya maendeleo mioyoni mwao ulizimika siku nyingi, ndio maana akili yao inawaz kukopa na kuomba misada, badala ya kufikiria namna ya kugeuza rasilimali kuwa mali.

Inasikitika kwa namna kiwango chetu cha exports kilivyokuwa chini.
 
High exportation kwa kiwango kikubwa ina tegemea na wingi wa viwanda mlivyo navyo na wingi wa bidhaa vinavyo zalisha na uhitaji wa hiyo bidhaa nje ya mipaka .

Pasipo wingi wa nishati hatuwezi kuwa na wingi wa viwanda vivo hivyo hatuwezi kuwa na wingi wa bidhaa kwa ajili ya hiyo high exportation .

Jambo la nishati ni jambo la kuzingatia kama tuna ihitaji hiyo high exportation.
 
Tanzania ina uwezo wa kuzalisha umeme ama installed capacity ya MW 1600 ila haiwi yote employed at full capacity. Nimewahi kusikia waziri akisema maximum highest demand ya Tanzania ni MW 1300 hivi, bado hata Tanzania wenyewe hatuwezi kujaza full capacity ya MW 1600.

South Afrika ina installed capacity ya MW 60,000 sawa na 50% ya installed capacity yote ya Africa Nzima. South Afrika inazalisha na kutumia karibu nusu ya umeme unaotumika Afrika nzima.

Tanzania inapaswa kufikia 2040 iwe na installed capacity ya MW 10,000 au zaidi vinginevyo tutakua kwenye matatizo makubwa sana ya kinishati.
 
South Africa na Egypt wana jitahidi sana,Lakini bado S.A ina changamoto kubwa sana za kinishati.

Nikwamba S.A nishati bado haijaweza jitosheleza.
 
1605.86MW ni installed capacity, sasa kama hii yote ilikuwa inazalishwa kwa mwaka mzima(itakuwa muujiza), inabidi uzidishe kwa masaa ya mwaka mzima ili kujiweka kwenye hiyo list

Nadhani katika siku 365.25, pengine tuseme tumezalisha kwa hiyo full capacity kwa siku 150 tu.

Hivyo, mwaka 2021 tumezalisha 5,781,096 MWh sawa na 5,781.1GWh
Pia MWh yetu itakuwa ni ndogo sana maana hiyo list ina nchi zaidi ya 200+ lakini taifa letu halipo kabisa katika hiyo list.
 
Nchi karibu zote zinazozalisha umeme mwingi hutegemea non renewable energy sources, umeme WA maji ni WA kiwango kidogo sana uzalishaji mwingi inategemea gesi, makaa ya mawe na nyuklia
 
Nchi karibu zote zinazozalisha umeme mwingi hutegemea non renewable energy sources, umeme WA maji ni WA kiwango kidogo sana
1. Makaa ya mawe tunayo lakini ni kama hatuya zingatiii katika kuzalisha nishati au hatuna wataalamu au haya jitoshelezi ? Mpaka sasa nipo njia panda

2. Gas&Oil vyote tunavyo je haviji toshelezi kwa hili swala ? napo pia sielewi

3. Nuclear energy kupitia madini ya uranium je wataalamu hatuna au tuna puuzia au tuna banwa na sheria za umoja wa mataifa kupitia mazingira ? Sielewi

4. Basi hata wind & solar njia iliyo nyepesi ya renewable energy nayo ni kama vile hatuizingatii, China kupitia solar per year wana zalisha zaidi ya GW 600=600,000MW na kupitia wind wana zalisha zaidi ya GW 400=400,000MW hapa tuna weza tukitilia nguvu kubwa maana kwanza sheria za mazingira za umoja wa mataifa hazita tubana na pia tuna faida ya uwepo wa maeneo makubwa ya kukusanya hii energy inayo potea bure.

5. Vipi pia kuhusu geothermal energy pia tuna unawanda mpana wa kufanya tafiti za kutosha katika hili .
 
Tatizo serikali imejipa mzigo mkubwa kuwa na monopoly kwenye sekta ya umem, china na USA kuna makampuni mengi ya umeme kitu kinachotoa fursa Kwa makampuni kuwekeza kwenye vyanzo vingi vya uzalishaji umeme hata kama serikali haiwekezi huko directly.

Sasa fikiria pamoja na Kwamba tanesco kuwa pekee yake bado inajiendesha kihasara na haiwezi anzisha mradi mpya bila serikali kutia mkono kitu kinachoongeza mzigo zaidi.
 
Serikali kuendesha mashirika ya umma na yakaweza tengeneza faida mfano Tanesco I
ina hitajika:-i, Wasomi wa hali ya juu waliobobea katika hiyo sekta, sisi shirika letu sidhani hata lina wasomi wabobevu wa hali ya juu wakutosha.
ii, Uwajibikaji hili ni tatizo katika sekta zote za hapa nchini.
iii, Uadilifu pia nalo hili ni tatizo katika sekta zetu.
iv, Wabunifu hili ni donda sugu linalo tutesa katika sekta zetu.
v, Mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia, bado shirika letu lina endeshwa kizamani zamani.
Vi, work force/ skiled labor sidhani hata shirika letu lina wafanyakazi wasomi wengi wa kutosha kwa nchi nzima.

Tuna hitaji ushindani wa mashirika binafsi katika nishati, shirika letu lipo taabani haliwezi kubadilika na kutuvusha kule tutakapo. tukiendelea kulikumbatia maana yake tuna taka kuendelea kukumbatia matatizo ya kinishati maisha yetu yote.
 
Data za mwisho wa mwaka wa 2021 ziki onesha viwango vya kinishati ya umene Tanzania pamoja na mataifa mengine walicho zalisha kwa mwaka.

Data hizo zili tawaliwa kwa taifa la China kwa kuongoza katika uzalishaji mwingi wa nishati za umeme, liki fuatiwa na taifa la marekani baadae India na mataifa mengine yakifuata.

Huu hapa mlolongo mzima wa mwaka 2021 kwa msaada wa Wikipedia kupitia wizara za nishati za mataifa husika.View attachment 2456448View attachment 2456449View attachment 2456450View attachment 2456451View attachment 2456452
[ Kwa mwaka wa 2021 taifa letu Tanzania lili zalisha Megawatts 1605.86 ].
Zingatia kuwa:
1 Gigawatts = 1000 Megawatts
Maswali:
1. Je sisi kama taifa tuna jifunza nini kwa hayo mataifa yaliyo tuzidi katika kiwango cha uzalishaji wa nishati ya umeme kwa mwaka ?

2. Je sisi kama taifa ni ipi mipango yetu ipi katika matumizi ya makaa yetu ya mawe katika uzalishaji wa umeme ?

3. Je sisi kama taifa tume ridhia kuwa na hiki kiwango kidogo cha uzalishaji wa nishati ya umeme kwa mwaka huku tuki pambana kutafuta wawekezaji wakubwa ?

4. Je ipi mipango yetu kuhusu madini ya uranium tuliyo nayo na uzalishaji wa umeme ?

5. Je ipi mipango yetu katika uzalishaji wa nishati ya umeme kwa njia ya geothermal,jua,upepo na pia kwa njia ya gesi ?

6. Je sera zetu katika upande wa nishati zina endana na kasi ya dunia kwa sasa upande wa nishati ?
Umekosea mkuu
Kuna tofauti kati ya Megawatts (Mw) na Megawatt hour (Mwh)
Gigawatts (Gw)na Gigawatts hour (GWh)

Hivyo ni vitu viwili tofauti, Hiyo 1600Mw ni kiasi cha umeme kinachozalishwa kwa sekunde moja Tanzania
Kupata kiasi cha umeme kwa mwaka (in MWh)itabidi uzidishe kwa idadi ya masaa ya mwaka mzima

Somo la Physics hílo
 
Sio kwamba nime kosea mkuu ni kuwa data zetu hajizawa converted into MWh ila hizo zengine zipo katika GWh .

Unaweza ukasoma mchango wa mdau hapo juu ameweza kuchambua naye katika mfumo wa MGh na MWh.

Lakini mchango wako ni mzuri kwa members wote tupate kufahamu data zime jitofautisha katika kipengele cha hour ili tusipate kuchanganya mambo.

Asante mkuu.
 
Mm nikiwaambia kuwa jamii ya kiafrika ina matatizo watu wananiona mbaya.
Hebu ona sasa kuna nchi zinazalisha megawatt mpaka mamilioni ila nchi yetu hata megawatt 1600 ni tia maji CCM ilaaniwe.
 
Sio kwamba nime kosea mkuu ni kuwa data zetu hajizawa converted into MWh ila hizo zengine zipo katika GWh .

Unaweza ukasoma mchango wa mdau hapo juu ameweza kuchambua naye katika mfumo wa MGh na MWh.

Lakini mchango wako ni mzuri kwa members wote tupate kufahamu data zime jitofautisha katika kipengele cha hour ili tusipate kuchanganya mambo.

Asante mkuu.
Mkuu hiyo 1600 MW ni rate ya uzalishaji

Ni kama unavyosikia mradi wa maji Ruvu unazalisha lita 1000 kwa saa, ina maana ili kupata lita zinazozalishwa mwaka mzima inabidi uzidishe kwa idadi ya masaa ya mwaka mzima

So kama Rate ya Tanzania ni 1600 MW ina maana kwa mwaka mzima tutakuwa tunazalisha

1600x365 days x 24 hours= 14,016,000 MWh
ambazo ni 14,016 GWh

Ambazo bado ni ndogo sana kama ilivyo pointi ya mada yako

Watts zinapima rate ya uzalishaji au utumiaji wa umeme, hata ukiambiwa pasi yako ni ya 750W ina maana ili upate umeme utakatumika ndani ya masaa 5 itabidi uzidishe kwa masaa

750watts x 5 hours=3750Wh au 3.7kWh ambazo ni unit 3.7
 
USA na China zinazalisha na kutumia zaidi ya 49% ya Umeme wote duniani.

Na uzalishaji hutegemea matumizi, hizo nchi zote zina viwanda vikubwa sana hivyo lazima matumizi ya umeme yawe makubwa pia

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom