Dating sio utamaduni wa mwafrika.

Dating sio utamaduni wa mwafrika.

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
8,323
Reaction score
18,051
Imezoeleka kusikia mabinti wakisema nadate na mtu fulani au fulani anadate na fulani au nataka kudate na fulani.

Kudate ni ile aina ya mahusiano ambayo watu wawili wasio jua hatima yao wanaamua kuwa pamoja wakifanya mambo au kuwa na ratiba as if ni wapenzi lakini sio wapenzi rasmi.

Sisi waafrika mfumo wa mahusiano umekuwa structured maeneo matatu,ya kwanza ni uchumba,pili ndoa na tatu familia baada ya ndoa kukamilika.

1. Uchumba ambao watu wengi huchanganya na kudate ni kile kipindi ambacho kijana anaishi na mwanamke ambaye amekwisha mposa na kujitambulisha kwao kisha familia yake ikalipa mahari na kukubaliwa kuoa binti wa familia. Binti kuanza kuonana na mwanaume baada ya kuposwa na kuvishwa pete ni sahihi sababu tayari familia imeshamtambua kijana na kumpa ridhaa ya kuwa na binti yao.

Kutokana na tamaduni za kisasa watu husubiria send off na ndoa ndipo warasimishe mahusiano yawe halali. Ila zamani ukishalipa mahari baada ya posa hapo hapo inapigwa sherehe unaondoka na mkeo unakwenda kuanza nae maisha kwa uhuru.

2. Ndoa,hapa kila mtu anajua ni aina gani ya maisha. Unaolewa au kuoa then unakuwa ni mume na mke wa mtu. Life style yake imekaa kitumishi. Unajitoa kwaajiri ya mwenzako na yeye anajikana kwaajiri yako. Mnapendana na kushirikiniana katika kila jambo bila kurudishana nyuma. Ndoa ni taasisi. Inalindwa,kusimamiwa,kutumikiwa bila kuchoka,inakua na kuwa familia na kujena faida mbali mbali za kijamii.

3. Familia. Hii pia kila mtu anafahamu. Kumradhi watoto wa masingle mother na mayatima najua mnamtazamo wa tofauti wa neno familia na hapa lazima muelekezwe. Familia ni baba,mama na watoto. Kinyume na hapo huwa tunasema kuna mapungufu na inakuwa ni familia ya dharula ila sio rasmi kwa kutimiza maagizo ya MUNGU. Tutalijadili hili siku nyingine kwa leo tuliache.

Kama nilivyokuwekea hapo juu hizo hatua hakuna sehemu nimesema kuna kudate. Hiyo sio tamaduni ya africans na haipo katika falsafa ya mahusiano ya kiafrika.

Mabinti wengi wanaipenda hii stage sababu ndio stage inayowapa uhuru wa kujiachia na kuwa huru kufanya mambo ambayo in the next 5 to 10 years yanawageukia kuwa sumu ya furaha yao ya maisha.

Kudate ni muda vijana na mabinti wanatoka out na kuingia gharama zisizo za lazima kujenga mahusiano ambayo yanaweza kutodumu hata miezi sita au mwaka au mahusiano yatayokaa muda mrefu wakijiita wachumba (na hawakuchumbiana popote ni kujitoa tu ufahamu) huku wakitumiana na mwishowe kuachana wakiwa wapweke na wasio na matumaini wala malengo ya kuendelea.

Kudate hakujawahi kuwa na matunda mazuri kwa vijana wengi labda tu kwa wale ambao walifanikiwa kudate na kufunga Ndoa ila takwimu zinaonyesha mabinti wengi waliopitia "Dating zone" wamejikuta wanajipaka changamoto au mikosi ambayo baadae inakuja kuwapa wakati mgumu sana kuingia uchumbani na kufanya ndoa serious. Changamoto kama higher number ya "body count", kutoa mimba changa,kuzaa nje ya ndoa,kutumika kama chombo cha mafunzo ya kitandani,kupoteza muda wa kujenga Ndoa, kuharibu mifumo ya uzazi, kupata magonjwa, na kadhalika.

Dating haijawahi na haitakuja kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa kupata mtu sahihi wa mahusiano ya ndoa na familia.

Kama umesimamishwa na mwanaume ni vema kumsikiliza na kupokea wito wake,then sikiliza neno lake, kama atakutoa out au mtasimama chini ya muembe ili akupe mistari yake haina shida. Msikilize kama ataonyesha dhamira ya kukupenda mpatie anuani na location ya nyumbani kwenu kwa wazazi au walezi wako kisha yeye akusanyane na ukoo wake wapange wazee kwenda kuomba ridhaa ya kukuoa na kuishi na wewe.

Wazazi wakibariki then atapangiwa mahari,apeleke then akuvishe pete then kuanzia hapo sasa muanze kutoka out kama wachumba kwenye mahusiano ya mapenzi. Mtakuwa huru kwenda popote na hata kulala kwa mwanaume bila shida hata kununuliana vitu vya gharama sababu sasa huyu ni mchumba wako na ni mwanamke wako halali.

Baada hapo jiandaeni kufanya ndoa ya kiimani rasmi ili mtambilike kijamii baada ya kutambulika katika koo zenu. Anzeni hata kama maisha ni kipato cha chini sana ni rahisi sana kukua mkiwa pamoja mkishirikiana.

Anyways,najua mabinti wa sasa hii haitawaingia kwasababu wamewekeza katika benefits zinazopatikana kwenye mazingira ya kudate na wanaona kama story za kufeli mahusiano na maisha wao hazitawakuta siku za baadae.

Dating sio sehemu salama na rasmi ya kuanzia mahusiano rasmi. Kama unataka kutengeneza changamoto za baadae them komaa na kidate.

Siku njema.
 
Huwezi kushindana na wakati
 
Back
Top Bottom