Datsun kurudi sokoni baada ya kutoweka kwa zaidi ya miaka 30

Datsun kurudi sokoni baada ya kutoweka kwa zaidi ya miaka 30

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Baada ya kutoweka kwa zaidi ya miaka 30, Datsun imerudi tena sokoni.

Gari hiyo ambayo iliwafanya carmakers wa Kjapani kuheshimika Marekani na Ulaya miaka 1970 ilikuwa inasifika sana kwa kubana mafuta.

Model mpya ya Datsun ambayo, ilizinduliwa jana nchini India, imekuwa designed kwa ajili ya first-time care owners.

Inatumia lita 1.2, ina viti vitano (hatchback) na itaanza kuuzwa India mwakani kwa dola 6,670 kabala ya kusambazwa Russia na Indonesia.

Datsun ya zamani.

datsun_510_ad.jpg

Datsun mpya

8923601_600x400.jpg

8-datsun-150713.jpg

datsun-cherry-interiors.jpg

DATSUN_GO_EXT09_off.jpg

New-Datsun-Go-Supermini-1%25255B2%25255D.jpg
 
ngoja wenye hela watumie kwanza then watuletee used tununue
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mzee umenikumbusha mbali sanaaa. Miaka ya 94 nliwahi kumiliki Datsun 1200, na baadae Datsun 120Y. hizi gari zilinitoa sana kimaisha sitazisahau kamwe!
 
na mimi nimekumbuka mbali, nilijua gari zao ni pickup tu, kumbe zipo saloon pia.
miaka hiyo mtu mwenye gari pickup aidha ana toyota hilux pickup au datsun pickup.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Wachaga wameuvamia uzi huu wakidhani ni mapick up. Wachaga kwa Datsun.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
na mimi nimekumbuka mbali, nilijua gari zao ni pickup tu, kumbe zipo saloon pia.
miaka hiyo mtu mwenye gari pickup aidha ana toyota hilux pickup au datsun pickup.

Lazima utakua kizazi cha Yooh yoo whats up ma nigga
 
mzee wangu, mzee change anayo mpaka leo anapaki moshi mjini anakula vichwa kwenda mbele, pickup ya dutsan si mchezo
 
Wachaga wameuvamia uzi huu wakidhani ni mapick up. Wachaga kwa Datsun.

mkuu wacha tu tuuvamie huu uzi,kuna gari ambazo mchaga hatakaa azisahau kizazi chake chote
1- bedford- hii ndio kama fuso ya enzi hizo kabla ya isuzu injection tx hazijaingia, bodi yake ilikuwa ya mbao .sijui kizazi cha fuso kinayajua haya
2- pioget pickup na sedan
3- toyota stauti- dume na jike
4- mandolini- landrover ya handeli- hii unashusha injini unafanya mashine ya kusagia kisha unairudisha unaenda kubebea mbege kibosho
 
Dah Umenikumbusha long mkuu Datsun Gari letu la pili mzee alinunua baada ya kuwasota sana na mgongo wa Chura... Datsun 120Y Warejeshe na Morris pia tumezimiss gari niliyokuwa napenda Maishani
28.jpg
 
Umenikumbusha mbali kweli kweli....
 
Dah Umenikumbusha long mkuu Datsun Gari letu la pili mzee alinunua baada ya kuwasota sana na mgongo wa Chura... Datsun 120Y Warejeshe na Morris pia tumezimiss gari niliyokuwa napenda Maishani
28.jpg

mkuu hiki chombo si mchezo ... mshua wangu (R.I.P) alitaka kunyea debe enzi hizo ... late 70's ... kisa alikuwa mtumishi wa umma na alinunua hii mashine tena ilikuwa used toka kwa mhindi ... yale mambo ya uhujumu uchumi yalitesa sana watu!
 
Dash board ya hiyo Datsun ni sawa na ya micra SE.
Wamebadilisha body tu.
 
mkuu wacha tu tuuvamie huu uzi,kuna gari ambazo mchaga hatakaa azisahau kizazi chake chote
1- bedford- hii ndio kama fuso ya enzi hizo kabla ya isuzu injection tx hazijaingia, bodi yake ilikuwa ya mbao .sijui kizazi cha fuso kinayajua haya
2- pioget pickup na sedan
3- toyota stauti- dume na jike
4- mandolini- landrover ya handeli- hii unashusha injini unafanya mashine ya kusagia kisha unairudisha unaenda kubebea mbege kibosho

hapo sema GURUWE, Kitu cha kubebea watalii enzi hizo.
 
Back
Top Bottom